Panya road wanauawa kwa risas. Je, wezi wa mabilioni ya kodi za Watanzania wanabakije salama?

Hii nchi bhana yaani watu hawajui wanataka nini, wakati panya road wanakamatwa na kutoka watu waluongea jeshi la police dhaifu sasa hizi wanawaweka chuma mnalalamika dah, ila mimi wawatandike chuma wote hakuna wa kwenda jera wote vyuma tu
 
Tofauti hao wanaiba kwa kalamu, wale wanaiba kwa kutumia nguvu
 
Mkuu ushasikia fisadi amekata mtu mapanga? Au kumuua mtu live kisa aibe hela. Hii story ndo headline ya panyarodi., yani wakikushika lazima wakutie kilema.
Hilo ndio tatizo lao kuu. !! Inaonyesha hawana chembe ya huruma. !!
 
Mtu anakuchana chana na sijui nyembe, panga mara bisibisi ili akunyang'anye simu ya laki hana maana.
Nilishawahi kukamatwa mara tatu na zote sikua nahusika, si watetei panda Road ila kunawengine uenda muonekano wao ukawapoza na kupoteza maisha bila hatia
 
Wale waliojenga kibanda Kwa ml 11 mbona hawakuuwawa???
 
Alafu Cha ajabu watu wa aina utakuta wanalalilia ben saanane kuwaawa alafu hao hao wanawatetea panya road
 
Nilishawahi kukamatwa mara tatu na zote sikua nahusika, si watetei panda Road ila kunawengine uenda muonekano wao ukawapoza na kupoteza maisha bila hatia
Pole boss. Ni kuwa na umakini wa kutofanana na panya kipindi hichi.
 
Umenifanya niifikirie nchi ya China mkuu.
 
Waingereza wamebahatika kuwa na lugha nyepesi, once ukishaielewa, it speaks for itself. Hii mada yako dhaifu, unalinganisha panyaroad na wezi wa makanikia, sawa. Hii ya panyaroad inaeleweka, wanamkaba mke wako wanamtishia bisibisi wanamnyanganya hereni zake, inauma, inaeleweka. Hii ya makanikia inaanzia dhahabu ya Chunya au Buyulang'hulu, wachimbaji weusi. Wamiliki ni wazungu wakisaidiwa na weusi wenzetu, wengi tu, wanaofahamika zaidi ni fatmakarume na tundulissu. Ni mafundi kupindisha sheria. Watendaji serkalini, Wizarani au STAMICO au TRA, kwa kutumia nyaraka za kitaalanu za fatmakarume, wanaiba billions and billions. Hawa ni hela nyingi na inaumiza wengi zaidi (kuliko mkeo peke yake kwa panyaroad), lakini Waingereza husema mada yako ni FAR-FETCHED. Ni nani utamkamata? Panyaroad yule unamuona na bisibisi zake na nondo, unamkamata. Lakini tundulissu na Barrick na BP utawashikaje? Ni wataalamu, wasomi, wanajua kujitetea. CONCLUSION? WEWE NDIYO UNATETEA WAOVU, PANYAROAD NI WABAYA LAKINI UNAWATETEA KWA KULINGANISHA NA FATMAKARUME? Utaanzia wapi?
 
Nilishawahi kukamatwa mara tatu na zote sikua nahusika, si watetei panda Road ila kunawengine uenda muonekano wao ukawapoza na kupoteza maisha bila hatia
Lakini askari mara nyingi wanavyo vyanzo vyao vingi vya kupata taarifa wanazozihitaji japo wakati mwingine makosa ya kibinadamu yanaweza kujitokeza !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…