Panya Road wapuuza karipio la Rais Samia, waendeleza uhalifu kama kawaida

Ni upumbavu kutumia msamiati huu wa "Panya Road" na ni aibu kubwa kwa viongozi wakuu wa polisi na serikali kuendelea kutumia neno hilo/msamiati huo. Full stop.

Wahalifu ni wahalifu, Majambazi ni majambazi. Piga shika ua peleka mahakamani ni shauri na dhamana walizokuwa nazo wananchi wenye umakini pamoja na nguvu za polisi na Mahakama. Lakini kutumia lugha na maneno/ msamiati huo ni kujidhalalisha.

Aluta Continua.
 
Pole, pamoja na kukamata wahalifu hata utumie miguvu namna gani, kama chanzo hakitatibiwa panya road watakuwa wanajirudia. Mengine ni ushabiki wako, baki nao.
 
Kagame kafanikiwaje?, Dola lazima itishe, mbona Rwanda husikii huo ujinga
Ndugu pole, dola sio lazima itishe. Kinachotakiwa ni ufumbuzi wa kweli na wa kudumu. Hata huko kwa Kagame kama nae mtindo ni miguvu peke yake, basi panya road wa huko watakuja rudi, tena vibaya zaidi kuliko hata mauaji ya kimbari.
 
Unataka panya road wapewe ajira? Au wewe ndo Mwenyekiti wao umekuja kupima upepo wa mitandaoni? Kawaambie kuwa serikali iko imara na hakika watapukutika sana!!
Wahalifu wakamatwe na kuchukuliwa hatua, lakini pawepo pia na ufumbuzi wa kudumu. Ama sivyo watakuja rudi tu Kama hivi Sasa. Ndugu kelele za jazba hazikusaidii wewe wala mtz mwingine yeyote.
 
Hao watoto wanapokamatwa na Polisi kwa nini wasikamatwe na wazazi au walezi wao ili washitakiwe kwa pamoja?
Haiwezekani wazazi au walezi wa hao wanaoitwa panya road wasijue matembezi na maisha ya watoto wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…