Panya Road wapuuza karipio la Rais Samia, waendeleza uhalifu kama kawaida

Panya Road wapuuza karipio la Rais Samia, waendeleza uhalifu kama kawaida

Ndio shida ilipo hajui yupo pale kwa shughuli gani.

Alisha tuonyana lakini ni ‘kudra za mwenyezi mungu’.

Inabidi aelezwe kudra za mwenyezi mungu mwisho 2025.
2025 mikopo, tozo, kodi, itatuua ni too late kwa wananchi wengi milioni 60 ya Watz kuongonzwa na mtu asiye na uwezo wowote wa kiungozi.
 
Magufuli aliwakuta wanatamba akawafuta kabisa.

Enzi za JK awa watoto walikuwa wanafunga mtaa na ikasemekana walishindikana.
Si kwel mzee hizi ni theories, yaan jeshi la police liwashindwe panya road? C kwel nadhan ni hatua madhubuti hazijachukuliwa tu, lkn huez sema eti flan alitokomeza wakat hua inakua ni operation ya jeshi!
 
Pamoja na Rais wa nchi kusimama na kutoa kalipio kali kwa vijana wahalifu wa Panya Road.

Wameendeleza harakati zao za kujeruhi watu na kuiba mali.

Inabidi Rais sasa aonyeshe uongozi hii ni dalili mpaka watoto kama hawa ambao hata Makonda aliweza kuwafuta kwenye mitaa hawamuogopi na wanampuuza.

Kipindi hiki ndio uwa wananchi wanalia machozi kumisss uongozi strong wa Magufuli.

Soma: Panya Road wajeruhi 19, Mtongani
Mnahangaika Nini? It is simple. Mkiwaona tena piga simu polisi uwaambie CHADEMA wanaandamana na kusumbua raia !

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
"PANYA ROAD" ni watoto wetu wenyewe. Tunaishi nao tunakula nao na tunalala nao pamoja kwenye nyumba zetu. Na hata wanapoleta mavuno yao ya uhalifu tunashiriki nao katika kufaidi matunda ya uhalifu wao. Hivyo tusijitoe ufahamu kwa kuwa tunawajua vizuri.
Dawa si kwaua kama baadhi wanavyodai. Hapo ndipo umuhimu wa Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii unapokuja. Tujipange vizuri katika maeneo yetu kwani ni rahisi kuwabaini kuwa ni watoto wa nani na wanaishi wapi. Wengine ni majirani zetu na wengine watoto wetu wenyewe. Tusingoje mpaka Polisi ndio waje washughulike nao. Polisi ni wachache sana; ratio ya askari Polisi mmoja kwa wananchi karibia elfu Moja mia nne hivi (1:1400).
Mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe. Hima tuwadhibiti watoto wetu mapema kabla ya 'operations' za Polisi hazijaanza. Hakuna kisingizio chochote kinachokubalika kubariki uovu na uhalifu huu wanaoufanya. Hakuna sababu yeyote ya kiuchumi inayoweza kutolewa kubariki uhalifu huu mbaya, sana sana ni ukosefu wa malezi mema na kukosa maadili. Tusishabikie watoto wetu kutumia njia za mkato (short cuts) kupata utajiri wa haraka haraka. Dawa ni kujituma tu kufanya KAZI iwayo yote ile HALALI kwa bidii sana na maarifa. Tujifunze kubadili Changamoto kuwa Fursa. UHALIFU HAULIPI.
 
Magufuli aliwakuta wanatamba akawafuta kabisa.

Enzi za JK awa watoto walikuwa wanafunga mtaa na ikasemekana walishindikana.
Na sioni ubaya kama tukitumia mbinu zilizofanikisha kuwatuliza enzi za hayati, muhimu ni amani irudi mitaani
 
Kwa uelewa wangu mm hawa ni wale watoto walokosa malezi ya wazazi wao ama kuzembea kwenye ulezi au watoto wa mitaani.
Lakini kubwa ni hili jambo ambalo watu wanaliona ni la kawaida ni jambo la Zinaa au kuzaa nje ya ndoa. hili jambo kiukweli linasababisha street children wengi mno hlf jamii wala haijali kuhusu ilo jambo ndo kwanza linashabikiwa mno.
Watoto wa Mitaani ambao hutelekezwa na Wazazi wao hasa hawa wa nje ya ndoa ndo hua wanaishia hivi lkn Kumbe maangamivu tunayasababisha sisi wenyewe hlf tunakaa tunalaumu Uongozi.Tukitaka kubadilika kwanza tuanze kubadilisha yaliyomo kwenye nyoyo zetu ndipo Mungu nae atatuongoza .

Naomba kuwasilisha mawazo yangu.
 
Ndugu,
Panya road ni mwanadamu kama wengine, anaweza kupewa ajira itakazomwezesha kupata kipato kilicho halali na kwa usalama HATA wa kwake kibaka mwenyewe, akatulia.
Hata Magufuli angekuwa MKWELI, kwenye takwimu za fursa na ajira alizokuwa anadai kutoa/kutengeza, tatizo hilo lingeweza kuendelea kupungua.
Unataka panya road wapewe ajira? Au wewe ndo Mwenyekiti wao umekuja kupima upepo wa mitandaoni? Kawaambie kuwa serikali iko imara na hakika watapukutika sana!!
 
Pamoja na Rais wa nchi kusimama na kutoa kalipio kali kwa vijana wahalifu wa Panya Road.

Wameendeleza harakati zao za kujeruhi watu na kuiba mali.

Inabidi Rais sasa aonyeshe uongozi hii ni dalili mpaka watoto kama hawa ambao hata Makonda aliweza kuwafuta kwenye mitaa hawamuogopi na wanampuuza.

Kipindi hiki ndio uwa wananchi wanalia machozi kumisss uongozi strong wa Magufuli.

Soma: Panya Road wajeruhi 19, Mtongani
Lile halikuwa kalipio Mkuu lilikuwa Ombi. Na Ombi linamawili kukubaliwa au kukataliwa. Waliombwa waache wanaweza kuumia( panya road)
 
Ili kuweza fanikisha mapambano dhidi ya hawa Panya Road lazima turudi katika taratibu za malezi ya miaka ya nyuma. Tunapaswa kuwajibika katika malezi ya watoto wetu kuanzia ngazi ya familia. Wazazi, walezi na ndugu tunapaswa kuwa karibu sana katika kuwalea vema kwa kuwafundisha tabia njema na maadili mema tangu utotoni. Hii ni pamoja na sisi wenyewe kuishi kwa kufuata sheria na kutenda matendo yaliyo mema kuwaonyesha mfano bora. Aidha, majirani, viongozi wa dini na Walimu katika ngazi zote nao wanatakiwa kuchukua nafasi zao stahili katika malezi ya watoto wetu.
Inapotokea mtoto kashindwa kurekebishika katika ngazi hiyo hapo ndipo msemo wa 'Asiyefundishwa na mamaye, basi atafunzwa na Ulimwengu' utajidhihirisha.
Huo ndio wakati Mfumo wa Haki-Jinai (Criminal Justice System) utachukua nafasi yake. Mtuhumiwa atakapothibitika ametenda uhalifu basi hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake bila kupepesa macho. Hizo ni pamoja na hatua za kutoa adhabu ili iwe fundisho kwake mhalifu na wengine ambao wangependa kuiga matendo kama hayo ya kihalifu, na pia hatua zingine za Urekebishaji zitachukuliwa.
Ushauri kwa Jeshi la Polisi ni kwamba ni vema wakawa na Mpango Mkakati endelevu. Wasingoje kutenda kwa matukio (Zimamoto). Tunajua kuwa sasa Polisi wako mpaka kwenye Kata. Wawe na utaratibu wa kuwafuatilia kwa karibu sana watoto watukutu na waliopo katika mgogoro na sheria na kuwachukulia hatua kali za kisheria bila kuwasahau wahalifu wa aina zote. Wazingatie sana 'Broken Windows Theory' kwani WASIPOZIBA UFA WATAJENGA UKUTA.
Kwa utaratibu huu bila kuwa na muhali na wahalifu tutafanikiwa kuwatokomeza 'PANYA ROAD' na hata kupunguza kea kiwango kikubwa aina nyingine zote za uhalifu.
 
Polisi wanacheza na hawa watoto na kingine watoto wamejua aliyeko juu ni mtu mpole mwenye huruma.

Leo hii Sirro akitoa amri kwa watu wake Panga road ni makaratasi dakika moja wameisha tunazika.

Mama akicheka na kima atavuna mabua
Nadhani sirro nae kama kaamua kukaa kimya tu ili mama wa mipasho aamue atakachoamua
 
Magufuli aliwakuta wanatamba akawafuta kabisa.

Enzi za JK awa watoto walikuwa wanafunga mtaa na ikasemekana walishindikana.
Hizi ni akili ndogo mnoo zilizojaa mahaba na mtu flan! System za usalama ndizo hushughulika na masuala ya kiusalama! Eti wanafunga mtaa 🤣🤣🤣 kwahiyo Jeshi la polisi walizidiwa nguvu na panya road? Acheni mahaba kwa marehem, ni muda kudili na walio hai!!
 
Hizi ni akili ndogo mnoo zilizojaa mahaba na mtu flan! System za usalama ndizo hushughulika na masuala ya kiusalama! Eti wanafunga mtaa 🤣🤣🤣 kwahiyo Jeshi la polisi walizidiwa nguvu na panya road? Acheni mahaba kwa marehem, ni muda kudili na walio hai!!
Mswahili bila fimbo haiendi,magu alichapa fimbo watendaji wake nao wakaenda.
 
Back
Top Bottom