Panya Road wavamia Bunju Magengeni, maduka yafungwa kwa kuhofia usalama

Panya Road wavamia Bunju Magengeni, maduka yafungwa kwa kuhofia usalama

seedfarm

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
260
Reaction score
2,655
Wakuu nimepata taarifa kuwa Bunju hali mbaya, Kuna Panya Road wanaharibu magari na kukata watu mapanga huko Bunju Magengeni

Nasikia hali mbaya, Hofu imetanda sana, Nipo Mbezi Beach naelekea huko lakini hali ni tete sana

Eneo la Magengeni hali ni mbaya sana kwa mujibu wa taarifa
----

Habarini za usiku huu, wakazi wa Bunju tupo kwenye sintofahamu ya kuvamiwa na hao vijana wanaojiita panya road, leo ikiwa ni mara ya tatu, ya kwanza ilikuwa wiki liyopita usiku wa kuamkia jumamosi.

Mara ya pili ni usiku wa kuamkia jana ambapo pia wamejeruhi watu vibaya, leo tena usiku huu walikuwa Bunju A wakikimbiza watu na kutishia maisha ingawa polisi wameshafika maeneo hayo na wanawakimbiza hao vijana ambao ni kundi kubwa mno.

Nipo nyumbani tena ndani,sina raha na sijui kama nitaweza kulala, msidai picha maana sina....!

Huu mwandiko uacheni tu....

===
Jeshi la Polisi mkoani hapa lina washikilia watu wanne kufuatia tukio la vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa kundi la Panyarodi kuvamia makazi katika eneo la Bunju B Mtaa wa Idara ya Maji saa 8 usiku wa kuamkia leo Februari 10, 2023.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dr es Salaam, Jumanne Muliro amesema kundi la watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya wanane, walifika kwenye mtaa huo wakipiga kelele za mwizi, mwizi, ambapo nyumba zilizokuwa zinafungua wakifikiri ni wezi walikuwa wakivamiwa na kujeruhiwa.

“Ni kweli tukio kama hilo lipo, kikundi cha wahalifu walivamia kwenye mtaa huo, kama unavyojua nyumba moja ya kupanga iliyokuwa na familia zaidi tano ndio ilivamiwa, kwa hiyo sio nyumba nyingi zilizovamiwa kama wanavyoeleza.

“Kwa wale waliofungua walijeruhiwa huku wakiwaamuru watoe fedha na wale wasiotoa walijeruhiwa maeneo mbalimbali ya na kusababisha watu nane kupata majeraha ambapo waliikimbizwa hospitali,” alisema Muliro.

Kamanda Muliro amebainisha kuwa pamoja na watu kujeruhiwa vijana hao walisababisha uharibifu ikiwemo kupasua runinga kwa watu wasiokuwa na fedha.

“Baada yaku kupiga kelele vijana hao walichukua bajaji na kukimbia lakini baadae walikimbizwa na bodaboda, walipofika njiani waliruka na kukimbia, polisi walifika na kuanza msako ambapo vijana wanne walikamatwa, ingawa wawili walijeruhiwa vibaya.

“Upelelezi wa awali unaonyesha vijana hao wametoka Mkoa wa Pwani tunaenelea na uchunguzi. Tunawashauri viongozi wa mitaa hiyo kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi,”alisema.

Mmoja wa majirani, Grace John ambaye nyumba yake haikuvamiwa alisema wavamizi hao walikuja majira ya saa 7 hadi saa 8 za usiku na walivamia nyumba za watu na kuwapiga mapanga.

“Tulisikia kelele za watu usiku, lakini hatukutoka nje, lakini baadaye tumeona majirani wakiwa wameumia kwa kushambuliwa na mapanga,” alisema.

Kwa upande wake mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Mama Munuo amesema watu hao walivamia majira ya saa 8 usiku na walivunja milango ya nyumba na kuingia na kuanza kukata watu mapanga.

Baadhi ya majeruhi katika tukio hilo wamelazwa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Kinondoni.

Chanzo: Mwananchi
 
Wakuu nimepata taarifa kuwa Bunju hali mbaya, Kuna Panya Road wanaharibu magari na kukata watu mapanga huko Bunju Magengeni

Nasikia hali mbaya, Hofu imetanda sana, Nipo Mbezi Beach naelekea huko lakini hali ni tete sana

Eneo la Magengeni hali ni mbaya sana kwa mujibu wa taarifa
Mbunge wa kawe na madwani wanasemaje?
 
Ila hii nchi watu hatupo serious. Kama jeshi la polisi limeshindwa wawape go ahead wanachi wajilinde wenyewe.

Huu upumbavu hauvumiliki. Raia na mali zao kutokuwa salama ni upuuzu wa hali ya juu. Toeni tu go ahead japo nayo ni mbaya maana wasio na hatia pia wanaweza kuwa targeted.
 
Serious unasubiri Police wakwambie wameshindwa!??
 
Wakuu nimepata taarifa kuwa Bunju hali mbaya, Kuna Panya Road wanaharibu magari na kukata watu mapanga huko Bunju Magengeni

Nasikia hali mbaya, Hofu imetanda sana, Nipo Mbezi Beach naelekea huko lakini hali ni tete sana

Eneo la Magengeni hali ni mbaya sana kwa mujibu wa taarifa
Hali ni mbaya huko bado hawajashkw
 
Mimi nimesikia ni Bunju kwa baharia na watu wamefunga maduka. Vyombo vya dola chukueni hatua! Hili tishio linaelekea pabaya sana.

Wananchi wakiamua kujilinda damu zitamwagika pande zote na mbaya zaidi raia wema ndio wahanga wa mwanzo.

Tukubaliane hili swala soon litagusa watu nyeti ndio tuamke maana kuna dalili linakomaa sasa.

Inasemekana hawa wahalifu sio usiku tu hata mchana wanavamia.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Alafu kuna mmoja humu anasema eti Tetesi
 
Back
Top Bottom