Panya Road wavamia Bunju Magengeni, maduka yafungwa kwa kuhofia usalama

Panya Road wavamia Bunju Magengeni, maduka yafungwa kwa kuhofia usalama

Ila hii nchi watu hatupo serious. Kama jeshi la polisi limeshindwa wawape go ahead wanachi wajilinde wenyewe.

Huu upumbavu hauvumiliki. Raia na mali zao kutokuwa salama ni upuuzu wa hali ya juu. Toeni tu go ahead japo nayo ni mbaya maana wasio na hatia pia wanaweza kuwa targeted.
Raia wana wajibu wa kujilinda wakisaidiana na vyombo vya dola.
Pale unapoona kuna hatari iondoe kama una uwezo, halafu toa taarifa polisi kwa hatua zaidi.
Uzalendo ni pamoja na kujilinda wewe na pia raia wengine unapoweza.
 
Hivi hakuna hata kambi ya jeshi karibu huko, naona kama polisi kazi ya panyaroad imekuwa ngumu kwao...

Polisi wetu wanafatilia madeal ya fedha tu ,ukikuta wana patrol na magari yao yale yenye namba za ajabu ajabu basi ujue wanafatlia madeal tu ,Hapo Boko Magengeni kama 2km kuna Kambi ya Jeshi 836 KJ Mbweni JKT ,tena kuna Boko Magereza kama 2km.

Mimi naona askari wanawachekea hao panya road ,wafanye kama walivyowafanya panya road wa mwembe yanga/tandika ,dawa ya jambazi na panya road ni chuma tu ,hao watu hawatakiwi kucheka nao ,mkicheka nao mtavuna mabua ,si umeona ujambazi ulivyokomeshwa? Inatakiwa Panya Road wale vyuma.
 
Wakuu nimepata taarifa kuwa Bunju hali mbaya, Kuna Panya Road wanaharibu magari na kukata watu mapanga huko Bunju Magengeni

Nasikia hali mbaya, Hofu imetanda sana, Nipo Mbezi Beach naelekea huko lakini hali ni tete sana

Eneo la Magengeni hali ni mbaya sana kwa mujibu wa taarifa
Nipo mianzini hapa,sekeseke lilipo tokea nilikuwa naangalia mpira ghafla watu wakaanza kukimbizana name nilikimbia nikadandia daladala,kurudi maeneo ya mjini,pindi nilivyo fika Boko chama nikaona gari za polisi zikielekea huko ikanilazimu nishuke baada ya vituo kadhaa ili nirudi maana simu na gari niliacha sehemu husika,now hali ni salama pia hata hapa mianzini hawakufika ila wananchi walikuwa na hofu na mashaka,nipo mianzini hali ni salama salmini.
 
Wanaume wa Dar mmeshindwa kabisa kuwadhibiti hivyo vitoto, lakini kuwa na michepuko au kuoa wake wawili na kufanya nao show off kwenye media mnaweza
Unaangalia sana taarifa ya habari. Panya road ni vijana wenye fujo, sio watoto, watoto dar ni chini ya miaka tisa, kutoka kumi anabaka hata dada yako na hakuna kitu utasema. Na anabaka mbele yako. Mwana jamii forum, punguza mihemko.
Ukisikia panyaroad ni vijana wamejizatiti, hata umoja wenu wa wanaume wa mikoani na serikali zenu, bado mnaweza chambishwa.
 
Wananchi wa Dar es Salaam wachukue hatua gn?
Waoga, wabinafsi, Wajuaji.
Mnaishi kama vile mko New York kumbe mko Dunia ya tatu, uswahilini.
Sasa watu zaidi ya 30 na mapanga wakivamia eneo dogo mtafanya nini? Bunju ni kubwa sana na hawa wanavamia eneo ambalo kwao ni rahisi kudhibiti. Bahati mbaya wanapofanikiwa inawapa ujasiri wa kufunga eneo kubwa zaidi.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Polisi wetu wanafatilia madeal ya fedha tu ,ukikuta wana patrol na magari yao yale yenye namba za ajabu ajabu basi ujue wanafatlia madeal tu ,Hapo Boko Magengeni kama 2km kuna Kambi ya Jeshi 836 KJ Mbweni JKT ,tena kuna Boko Magereza kama 2km.

Mimi naona askari wanawachekea hao panya road ,wafanye kama walivyowafanya panya road wa mwembe yanga/tandika ,dawa ya jambazi na panya road ni chuma tu ,hao watu hawatakiwi kucheka nao ,mkicheka nao mtavuna mabua ,si umeona ujambazi ulivyokomeshwa? Inatakiwa Panya Road wale vyuma.
Boko na Bunju kumejaa viongozi na majeshi yote yana kambi huku. Kama doria za Polisi zinashindwa waombe msaada wa majeshi mengine kufanya operation mtaa kwa mtaa.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu nimepata taarifa kuwa Bunju hali mbaya, Kuna Panya Road wanaharibu magari na kukata watu mapanga huko Bunju Magengeni

Nasikia hali mbaya, Hofu imetanda sana, Nipo Mbezi Beach naelekea huko lakini hali ni tete sana

Eneo la Magengeni hali ni mbaya sana kwa mujibu wa taarifa
Wamerudi tena
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Poleni

Tafuta siraha ya moto uishi kwa aman
Asante , siwezi hata kuua panya achilia mbali kumiliki silaha! Nipo nyumbani na watoto wangu wawili baba yao yupo nje ya Dar..
 
Boko na Bunju kumejaa viongozi na majeshi yote yana kambi huku. Kama doria za Polisi zinashindwa waombe msaada wa majeshi mengine kufanya operation mtaa kwa mtaa.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app

Kabisa hao wapuuzi wenye mapanga butu ndiyo watishie amani,si kweli ,ni ndani ya 2hrs tu wanasahaulika kwenye ulimwengu wa dunia....Hao Panya road wameanza tangia j5 vurugu zao na wizi...Nadhani wanatoa meseji ya kuvunjiwa vibanda vyao kuanzia mwenge hadi bunju.
 
Back
Top Bottom