Panya Road wavamia Bunju Magengeni, maduka yafungwa kwa kuhofia usalama

Panya Road wavamia Bunju Magengeni, maduka yafungwa kwa kuhofia usalama

Boko na Bunju kumejaa viongozi na majeshi yote yana kambi huku. Kama doria za Polisi zinashindwa waombe msaada wa majeshi mengine kufanya operation mtaa kwa mtaa.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Sawa lakini Polisi au Wanajeshi mpaka waje anzeni nyie mkinukishe haswa watakapokuja hao polisi au wanajeshi basi walao wakute mizoga walau 5-7 au zaidi. Wakiwauliza nyie semeni hivi: "Wameuawa na watu wenye hasira kali"
 
Yaan momepita hapo Bunju B Kama do 10 zilizopita, nimeona heka heka, defender na police wengi, aisee... Amani ni kitu muhimu Sana.
Hivi kumiliki Bastola masherti yake ni yapi?
Aaaah! Mjomba, Mpaka uje kuimiliki hiyo bastola kwa urasimu uliopo; hao panya watakuwa wesha sepa. Ww anza hata na panga, rungu, nondo, mshale, gobore n.k. twanga wapuuzi hao.
 
Nipo mianzini hapa,sekeseke lilipo tokea nilikuwa naangalia mpira ghafla watu wakaanza kukimbizana name nilikimbia nikadandia daladala,kurudi maeneo ya mjini,pindi nilivyo fika Boko chama nikaona gari za polisi zikielekea huko ikanilazimu nishuke baada ya vituo kadhaa ili nirudi maana simu na gari niliacha sehemu husika,now hali ni salama pia hata hapa mianzini hawakufika ila wananchi walikuwa na hofu na mashaka,nipo mianzini hali ni salama salmini.
Mmmh yaani ulikimbia mpaka ukaacha na gari yako ukadandia daladala!!! Yaani nyinyi ndio mnaosababisha sisi ngosha wa Dar tuitwe wanaume wa Dar! Tena walikuwa hawajafika hata hapo Mianzini!!? Wewe ni mwanamke au!!???
 
Unaangalia sana taarifa ya habari. Panya road ni vijana wenye fujo, sio watoto, watoto dar ni chini ya miaka tisa, kutoka kumi anabaka hata dada yako na hakuna kitu utasema. Na anabaka mbele yako. Mwana jamii forum, punguza mihemko.
Ukisikia panyaroad ni vijana wamejizatiti, hata umoja wenu wa wanaume wa mikoani na serikali zenu, bado mnaweza chambishwa.
Hivyo ni vitoto tu. NIni maana ya Dar kuwa kanda maalum? Kama hivyo vitoto vimejipambanua hivyo inamana wanaosimamia usalama wa raia na mali pamoja na silaha zao wameshindwa kazi
 
Pigaa risasiii wakafiee hukoo aiseee hakuna kesi ya Ujambazi ni kupoteza mudaa
 
Mmmh yaani ulikimbia mpaka ukaacha na gari yako ukadandia daladala!!! Yaani nyinyi ndio mnaosababisha sisi ngosha wa Dar tuitwe wanaume wa Dar! Tena walikuwa hawajafika hata hapo Mianzini!!? Wewe ni mwanamke au!!???
KhaKhaKhaa; Polepole jamani. Huyo alikuwa anainusuru nafsi yake kwanza. Gari si atanunua nyingine ila sio roho yake. Panya rodi wapo pia wanawake au ???.
 
Wakuu nimepata taarifa kuwa Bunju hali mbaya, Kuna Panya Road wanaharibu magari na kukata watu mapanga huko Bunju Magengeni

Nasikia hali mbaya, Hofu imetanda sana, Nipo Mbezi Beach naelekea huko lakini hali ni tete sana

Eneo la Magengeni hali ni mbaya sana kwa mujibu wa taarifa
----




===
Jeshi la Polisi mkoani hapa lina washikilia watu wanne kufuatia tukio la vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa kundi la Panyarodi kuvamia makazi katika eneo la Bunju B Mtaa wa Idara ya Maji saa 8 usiku wa kuamkia leo Februari 10, 2023.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dr es Salaam, Jumanne Muliro amesema kundi la watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya wanane, walifika kwenye mtaa huo wakipiga kelele za mwizi, mwizi, ambapo nyumba zilizokuwa zinafungua wakifikiri ni wezi walikuwa wakivamiwa na kujeruhiwa.

“Ni kweli tukio kama hilo lipo, kikundi cha wahalifu walivamia kwenye mtaa huo, kama unavyojua nyumba moja ya kupanga iliyokuwa na familia zaidi tano ndio ilivamiwa, kwa hiyo sio nyumba nyingi zilizovamiwa kama wanavyoeleza.

“Kwa wale waliofungua walijeruhiwa huku wakiwaamuru watoe fedha na wale wasiotoa walijeruhiwa maeneo mbalimbali ya na kusababisha watu nane kupata majeraha ambapo waliikimbizwa hospitali,” alisema Muliro.

Kamanda Muliro amebainisha kuwa pamoja na watu kujeruhiwa vijana hao walisababisha uharibifu ikiwemo kupasua runinga kwa watu wasiokuwa na fedha.

“Baada yaku kupiga kelele vijana hao walichukua bajaji na kukimbia lakini baadae walikimbizwa na bodaboda, walipofika njiani waliruka na kukimbia, polisi walifika na kuanza msako ambapo vijana wanne walikamatwa, ingawa wawili walijeruhiwa vibaya.

“Upelelezi wa awali unaonyesha vijana hao wametoka Mkoa wa Pwani tunaenelea na uchunguzi. Tunawashauri viongozi wa mitaa hiyo kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi,”alisema.

Mmoja wa majirani, Grace John ambaye nyumba yake haikuvamiwa alisema wavamizi hao walikuja majira ya saa 7 hadi saa 8 za usiku na walivamia nyumba za watu na kuwapiga mapanga.

“Tulisikia kelele za watu usiku, lakini hatukutoka nje, lakini baadaye tumeona majirani wakiwa wameumia kwa kushambuliwa na mapanga,” alisema.

Kwa upande wake mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Mama Munuo amesema watu hao walivamia majira ya saa 8 usiku na walivunja milango ya nyumba na kuingia na kuanza kukata watu mapanga.

Baadhi ya majeruhi katika tukio hilo wamelazwa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Kinondoni.

Chanzo: Mwananchi
Ila watu wa Dar bwana!! Kwahiyo hao vijana 8 tena wameshika bisibisi ndio wakuwajadili kweli?
 
Hivi hawa ni panya road au kuna kikundi cha uhalifu kikubwa kinapoozwa kwa kuitwa 'panya road'? Kwa ninavyojua mimi, sidhani kama kuna kijana wa kitanzania ambaye wataji organise wawe na mapanga bila nguvu ya kundi kubwa la kihalifu nyuma yao.
 
Mmmh yaani ulikimbia mpaka ukaacha na gari yako ukadandia daladala!!! Yaani nyinyi ndio mnaosababisha sisi ngosha wa Dar tuitwe wanaume wa Dar! Tena walikuwa hawajafika hata hapo Mianzini!!? Wewe ni mwanamke au!!???
Usiwe kiazi babu ndo maana nyie mnaitwa wa shamba,kitendo cha kutoka na gari me binafsi sikuona usalama zaidi kwa watumiaji wengine wa barabara,watu wanakimbia hovyo alafu niwashe gari unanitakia nini mimi na watu wengine huoni kama yangekuwa maafa,kuna watoto wadogo ambao nimesaidia mpaka wapande daladala kabla ya kupost fikiria,na hapo unaona kundi kama la watu mia linakimbia wewe usikimbie pia kimbia lakini usilete madhara kwa watu wengine
 
Back
Top Bottom