TANZIA Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88

TANZIA Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88

Kama inakuingia wewe akilini mimi inakataa,mkuu kweli unaamini maneno uliyoandika hapo juu nilipo-bold?

Nisaidie pakuyasoma niongeze maarifa na mimi.
Hili nilisoma miaka ya nyuma sana, ingawq kwa sasa wanakanusha kabisa kwa kusema ni uzushi.

Kwa sasa wanakanusha kabisa na kusema kuwa wanafuata maelekezo ya madaktari

Lakini wale wa zamani walikuwa wanafanyiwa hivyo na kuitwa majina yao mara tatu
Sio maneno yangu bali nilikuwa najua tangu shule
Screenshot_20250421_095234_Google~2.png
 
Haukumuelewa tu,wenye dhambi hawatengwi wenye dhambi unatakiwa ukae nao karibu ili wakuige wewe yale mazuri uliyo nayo na ndicho alichokuwa anajaribu kukisema ila alikosa lugha sahihi ya kukiambia kizazi hiki kinachotafsiri maneno jinsi kinavyotaka ili kipate maana kinayoitaka.

Imani ya kweli ni ku-stick na wale unaohisi wana dhambi ili waanze kubadilika kuja kwenye hali yako unayohisi wewe ni nzuri zaidi yao,kuna haja gani kukaa wote mliokamilika mtasahihishana nini wakati wote mpo perfect?
Tujifunze sheria za Mungu:

“Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni mwanamke. Hilo ni chukizo. Soma Walawi 18:22

“Je, hamkusoma kwamba Muumba tangu mwanzo ‘Aliwaumba mwanamume na mwanamke,’ akasema, ‘Kwa sababu hii, mtu atamwacha baba na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’?”. Mathayo 19:4
 
Jamaa zake wa Tanzania hawana habari, wanapambana kuingiza mtu wao ikulu, hata kwenda kumsalimia aaahhh... Hovyo kabisa
Waende kumsalimia wakati wao pale Vatcan ni nyumbani! Wageni ndio wanaoenda kumsalimia
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amefariki dunia leo April 21,2025 kwenye Jumatatu ya Pasaka akiwa na umri wa miaka 88 ambapo Vatican imethibitisha na kusema Papa amefariki kwenye makazi yake Vatican na taarifa zaidi kuhusu kifo chake zitatolewa.

Papa ambaye alizaliwa mwaka 1936 hivi karibuni amepitia changamoto ya upumuaji hadi kuhitaji mashine ya kusaidia kupumua na amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo maambukizi ya mapafu(nimonia) hadi kupelekea kulazwa kwa wiki kadhaa kabla ya baadaye afya yake kuimarika.

======================================

Pope Francis, the reforming head of the Catholic Church who sought to modernise the pastoral and public priorities of the Vatican, has died at the age of 88.

The Vatican announced the death of the Argentina-born Francis, a ground-breaking and progressive figure on Monday.

He was the first pope to be born or raised outside Europe in 12 centuries, the first from the Americas and the first Jesuit to hold the role.

View attachment 3310884

View attachment 3310870

Source: BBC
R.I.P
 
Kama inakuingia wewe akilini mimi inakataa,mkuu kweli unaamini maneno uliyoandika hapo juu nilipo-bold?

Nisaidie pakuyasoma niongeze maarifa na mimi.
Hapo zamani kabla ya kukua kwa ufahamu wa binadamu hii ilitumika
 
Tujifunze sheria za Mungu:

“Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni mwanamke. Hilo ni chukizo. Soma Walawi 18:22

“Je, hamkusoma kwamba Muumba tangu mwanzo ‘Aliwaumba mwanamume na mwanamke,’ akasema, ‘Kwa sababu hii, mtu atamwacha baba na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’?”. Mathayo 19:4
Usiende mbali, hapa hapa nchini hata miezi minne haijaisha aliyekuwa shoga maarufu nchini ameokoka na ameomba akasomee uchungaji. Hilo ndilo alilosisitiza Ftancis, kuwa hawa watu wasitengwe kwani nao ni binadamu, bahati nzuri kanisa la kilokole limetekeleza kwa vitendo. Je, wewe unachukuliaje kitendo hicho?
 
Rip PAPA Francis 88 imetosha Tutakukumbuka kwa mengi zaid uliwachukia watu wanaodhalilisha viongozi wa Dini bila kujali iman gani anaedhalilishwa !!!

ww mkweli zaid

Lkn sasa zamu yetu wamatumbi tupate PAPA ili kusaidia kupiga vita Ubaguzi wa langi kivitendo sio kimaneno tu.
 
Back
Top Bottom