Papa Francis ana mpango wa kuruhusu mapadri kuoa

Papa Francis ana mpango wa kuruhusu mapadri kuoa

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Papa anadai kuwa takwa la mapadri kutooa lilikuwa ni la muda tu(Takwa hilo lilianza karne ya 11). Anasema hakuna utata wowote iwapo watawa wataoa. Anadai mapadri wa kanisa la mashariki wanaoa na hakuna shida yoyote. Anafanya mpango kureview suala hilo.

======

In a new interview, Pope Francis discussed the possibility of relaxing the discipline of priestly celibacy. Speaking to the Argentinian news website info babe, Pope Francis recalled that in the eastern catholic church, married men are allowed to be.

WION
 
Papa anadai kuwa takwa la mapadri kutooa lilikuwa ni la muda tu(Takwa hilo lilianza karne ya 11). Anasema hakuna utata wowote iwapo watawa wataoa. Anadai mapadri wa kanisa la mashariki wanaoa na hakuna shida yoyote. Anafanya mpango kureview suala hilo.
Hhhhhhhh dini ya mabadiliko hii

Agano jipya part ngapi hili ?
 
Papa anadai kuwa takwa la mapadri kutooa lilikuwa ni la muda tu(Takwa hilo lilianza karne ya 11). Anasema hakuna utata wowote iwapo watawa wataoa. Anadai mapadri wa kanisa la mashariki wanaoa na hakuna shida yoyote. Anafanya mpango kureview suala
Chanzo?
 
Papa anadai kuwa takwa la mapadri kutooa lilikuwa ni la muda tu(Takwa hilo lilianza karne ya 11). Anasema hakuna utata wowote iwapo watawa wataoa. Anadai mapadri wa kanisa la mashariki wanaoa na hakuna shida yoyote. Anafanya mpango kureview suala hilo.
Katika hili, namuunga mkono. Na iwe ni sharti mojawapo la kupata upadri. Na Maaskofu nao waishi maisha ya kifamilia, ya mke na mume. Maisha ya useja yana majaribu mengi. Na bahati nzuri nimeishi seminarini kwa miaka 4! Hivyo ninaongea through experience.

Na wale watawa wa kike na wa kiume nao waruhusiwe kuoa, na pia kuolewa. Mambo ya kukutana kimwili kwa kificho, hayana nafasi kwenye hii karne ya 21.

NB: Kanisa lisiache kamwe msimamo wake wa kupinga utoaji hovyo wa mimba, na pia ndoa za jinsia moja.
 
Kuoa sio dhambi.
Zinaa ni dhambi.

Kutooa ni uamuzi wa mtu Mwenyewe kujiweka wakfu Kwa Mungu Kwa ajili ya kufanya kazi yake Kwa uaminifu mkubwa sana.

Kujifanya kuwa huna mke au huoi halafu unakua mzinifu ni kujidanganya mwemyewe na kumdhihaki Mungu. Lakini pia wachungaji waliooa halafu wakawa wazinifu ni waongo zaidi kuliko wale wasiooa wakazini .

Kumtumikia Mungu katika wakati huu wa Roho Mtakatifu ni ngumu sana mana inahitaji usafi mkubwa sana kiroho na kimwili . Roho Mtakatifu hakai ndani ya mtu mchafu Kwa namna yoyote .

Yesu anataka watakatifu wa kwenda Mbinguni pamoja na yeye kwa ajili ya kuwahukumu watenda dhambi . Hivyo hakuna kitu kichafu kitakachokanyaga Mbinguni. No. Wengine watasubiri kuhukumiwa TU Kwa kupimwa matendo yao Kwa SHERIA. Kama watakavyokuwa Waislam na wanadamu wengine.

Watu wasicjezee nafasi ya kuketi pamoja na Kristo katika ufalme wa Mungu kwani ni jambo kubwa sana na litawahusi wachache sana. Kwani wanouona mlango wa kuingia Mbinguni ni Wachache sana.
 
Huyu papa huyuu ananipa wasiwasi sana, antichrist.. ?
Hivi ni baadhi ya vituko vyake.

1. Kumpiga kibao muumini aliyemvuta

2. Kulike picha za matako ya mrembo instagram.

Sasa kama kweli kasema, angepaswa kujua uimara wa imani unaotokana na rijari kutomwaga, na ajue pale tu mwanamme anapokuwa baba. Mchezo umeisha yale mambo makubwa ya kiimani ndo basi tena. Familia ndio inakuwa jambo kubwa kwake.

Watubwa busara walishasema usimwamini mtu ambaye ni mume.
 
Back
Top Bottom