Papa Francis: Hisani ya Kichungaji itumike wapenzi wa jinsia moja wanapowaomba mapadri baraka

Status
Not open for further replies.
Wahuni hawa ndio maana KIKEKE kawakacha
 
😭😭😭 papa anabariki wapenzi wa jinsia 1 hii nihatari yahali yajuu!! Apinduliwe tuu jmn
 
Why mnapotosha.... ndoa ya jinsia moja na kumuombea mtu anayeshiriki mahusiano ya jinsia moja mbona ni vitu viwili tofauti.

Ni sawa na kusema machangudoa wasiombewe makanisani kisa itakua "umehalalisha".
 
Ukristo ssio dini
 
Suala la ndoa za jinsia moja ni ushenzi na ushetani mkubwa sana ambao haupaswi kuungwa mkono na wanadamu wenye akili Timamu.
 
Majibu ya Papa ya juu mno.

Amesaidia huyo mfasiri.
 
Mara nyingi nukuu za bbc kwa papa uwa zinaleta utata sana
BBC ni shirika la Uingereza nchi ambayo monarch wake (King/Queen) anakuwa kiongozi wa Anglican Church ambayo ilitokana na upinzani dhidi ya Katoliki.

Mfano unategemea shirika la habari la Wasabato limseme vizuri Papa? Unategemea Sputnik iiseme vizuri Marekani, au redio ya serikali ya Rwanda imseme vizuri Rais wa Burundi, au TBC imsifie Mwabukusi?
 
Nimesoma uzi humu unaonyesha amerasimisha ushoga
Ukiona kiongozi Mkuu wa Kanisa lolote duniani anatoka America kaskazini au kusini jua ni shetani pepo kakalia kiti

Lazima avuruge kanisa Papa aliyepo anatoka Bara la Amerika Kusini


Ni wakati wa waafrika kujitenga na makanisa ya bara la Amerika na nchi kama Uingereza.

Wameharibika sana hawafai asilimia kubwa

Hata wao kujiita Wakristo ni aibu na kuchafua kanisa
 

Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomwomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".

"Hatuwezi kuwa majaji ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga," alisema.

Aliongeza, hata hivyo, kwamba Kanisa bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya idadi iliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na mhudumu, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.

Maaskofu katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ubelgiji na Ujerumani, wameanza kuwaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, lakini msimamo wa mamlaka ya Kanisa ulibakia kutoeleweka.

Mnamo 2021, kufuatia ombi kama hilo la ufafanuzi, ofisi ya mafundisho ya Vatikani iliamua kutoruhusu zoea hilo.
Akijibu ombi la hivi punde zaidi, Papa alisema kwamba Kanisa linaelewa ndoa kuwa "muungano wa kipekee, thabiti, na usioweza kutenganishwa kati ya mwanamume na mwanamke" na inapaswa kuepuka "aina yoyote ya ibada au sakramenti ambayo inaweza kupingana na imani hii".
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…