Umeandika kirefu, nami nitafanya hivyo kwa ufafanuzi:
1. Ni muhimu kutulia, kutuliza mawazo kwanza kutambua kama taifa tumepotea njia (akiita Kolimba dira na mwelekeo), vyama vya siasa hadi mtu mmoja mmoja.
2. Taifa la watu jeuri (akiwaongelea Nyerere) wenye kuhoji aina ya kina Shivji, Lwaitama, Baregu, Chachage, Mpina, Lissu hawapo tena au ndiyo watakapokwisha ondoka, kondoo waliotamalaki sasa watashika hatamu kama ilivyo sasa wakijiona wao ndiyo wao.
3. Kabla ya kuhoji na hata mtu kuzipigania haki zake, imani inakuja kwanza.
4. Mtu akiamini hiki ni haki yàngu atahoji akinyimwa; akikomaliwa, atakomaa.
5. Imani kama hii, jiulize tukwame wapi kwenye ukombozi:
View attachment 2849562
6. Leo hii waliokuwa wanabeza makelele dhidi ya kuuliwa au kupotezwa kin Ben, Lijenje, Azory au jaribio la LIssu, leo wanapiga kelele watanzania wawili kuuliwa vitani si kwa si sahihi wowote kuuliwa popote wanapokuwa Hawana hatia, bali kwa kuwa ni wakristo wanaodhani Gaza kuna vita dhidi ya wakristo!
7. Leo hii kina
FaizaFoxy wana taabu Gaza si kwa sababu ya maonezi kwa wapalestina (ambayo ni kweli), bali kwa sababu wanadhani wanaonelewa ni waislam.
8. Wakristo uchwara wanadhani kumpinga mwisraeli ni kupinga ukristo na kuwa wanaofanya hivyo ni lazima tu wawe mwislamu; wamezidiwa mahaba mshindo!
9. Hapo #8 wanasahau kuwa Mandela, Nyerere, Lissu na wengi hawakubaliani na waisrael Gaza lakini si waislam!
10. Katokea Papa na suala LGBTQ, watu wanashindwa kuona hili ni pilipili usizozila, lisilokuhusu la wale wewe na engine zao kokote liliko sirini huko taabu na wengine tusiohusuka? Uhuru kumbe maana yake nini?
11. Tatizo kubwa ni uelewa na ufahamu kwamba "falsafa" ya nini au nani wanasimamia nini.
12. Bila kujua "falsafa" za vyama, vyama haviwezi kuwa na imani wala misimamo; na hivyo wafuasi; wala nchi ambayo falsafa ya chama tawala ndiyo msingi.
13. Kwenye urojo tuliomo kutowatambua waliobakia wamesimama, tukawa tayari kujifunza kwao na hata kuwa ujasiri wa kuwapa maua yao wanapostahili; ili kama vipi tugute na waliolala waamke, hakutakuwa na maana yoyote kuwapo duniani!
14. #13 hapo ndiyo ulio msingi mkuu wa hoja.
Ni hayo tu ndugu mjumbe.
Imani bila matendo ni bure!