Papa Francis, Lissu, machampioni halisi wa haki, usawa na uhuru duniani

Papa Francis, Lissu, machampioni halisi wa haki, usawa na uhuru duniani

Tufike mahali tuvunje ukimya:

1. Kuzitambua jitihada za kupigiwa mfano za watu wengine ni jambo la kistaarabu.

2. Vita vya kupigania haki, usawa, uhuru, demokrasia na maendeleo ni vita vya kudumu.

3. Nani asiyeyapenda au kuyahitaji matano hayo?

4. Manne ya mwanzo ni ya msingi zaidi duniani, wakati maendeleo ni ya mtu na taifa moja moja.

5. Matano hayo ndiyo agenda kuu katika chaguzi zote za waliostaarabika duniani.

6. Nchi isiyo amini katika matano hayo haina mchango wowote katika dunia hii.

7. Kiongozi yeyote asiyeamini katika matano hayo hatufai!

8. Chama kisichokuwa na imani yoyote kwenye matano hayo ni cha hovyo.

9. Tumekuwa na vyama vya hovyo visivyokuwa na imani yoyote inayojulikana kuyahusu.

View attachment 2849448

View attachment 2849401

10. Kiongozi, chama au taifa lisilokuwa na imani zozote zinazojulikana litakuwa na msimamo gani kwenye nini?

View attachment 2849434

11. Imani huzaa misimamo isiyoteteleka:

(a) "Heko Papa Francis, Tundu Antipas Lissu na wengine kwa kuiweka misimamo yenu wazi kuhusu Palestina, Gaza, Israel na hata haki za LGBTQ."

(b) Haipo shaka hata msimamo wa wawili hawa kuhusu Ukraine hauwezi kuwa rojo rojo au kuwa kama wa wasiojitambua

12. Hapo #11; kwa hakika ninyi ni viongozi na hazina kwa dunia kama wale wenye kufuzu zawadi za Nobeli.

Nyetere ni mfano mwingine wa kuigwa:

Palestine, Julius Nyerere and international solidarity – Middle East Monitor
Palestina palestina.

Unakera
 
Naona hapo kwenye namba saba na nane ndipo kwenye kiini cha hoja yangu ya mwanzo.

Hasa pale nilipozungumzia upimaji wetu wa haki na kuzidai tunaufanya kwa kutazama kipimo cha either itikadi zetu au imani zetu, bado hatujawa na uwezo wa kusimama na kudai haki zetu, hata kwa wale wa nje ambao nao wanapigania haki zao.

Inapofikia hatua hiyo tunaanza kutazama interest zetu kwa wanaodai haki, au wanaowanyima wengine haki zao.

Hapa kuna wakati utakuta sababu zinazotumiwa na wengi ili kukwepesha kundi fulani la watu kupata haki zao hazina mashiko, tena wakati mwingine hufika mbali mpaka kutengeneza picha za uongo ilimradi kutimiza malengo yao, unajiuliza hii yote maana yake nini?

Kwanini tunakuwa wagumu wa kukiri fulani yuko hivi au vile, kama hatuwezi kukiri hilo ambalo kwangu ni sawa na ule msemo wa boriti na kibanzi jichoni, hivi tutakaa kweli tuje kujikomboa hapa tulipo na haya madai yetu ya kila wakati?!

I doubt.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

1. Mkuu niliandika uzi huu:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

nikiugulia hizo #7 na #8 mawazoni mwangu kwa maana yake kamili.

2. Ya kwamba:

Kama Maji Maji au Mau Mau ilikuwa halali, iweje lawama kwa wapalestina?

Huu nao ukiwa Uzi mwingine wenye mauzui hayo hayo!

3. Ni aibu kuwa tumejikita kuwa waumini wa dini na watu badala ya kuzijua haki zetu na kuwa waumini nguli wa "usawa, uhuru na demokrasia."

4. Inatia moyo kuwa wakristo na waislam wanaiiishi imani yao kuhusu mambo ya LGBTQ kiasi kuwa kwenye hili wako pamoja, hata dhidi ya Papa kama kina Bujibuji Simba Nyamaume (bila kujali dini) wanavyo jitanabaisha; bila kuwa na hofu!

5. Kama #4 hapo ni hivyo kwanini sisi tusiwe na misimamo yetu madhubuti na hata kuwakabili Lissu, Mbowe au samiana hata kuwakemea au kuwataka kupisha njia au hata viti, kama wakithubutu kutaka kutanga mbali na misingi yetu imara ya imani?

6. #5 hapo siyo kuwa kIna allen kiwelella, Erythrocyte, JokaKuu, Retired, imhotep nk watakwambia unataka kuonja sumu kwa ulimi na kusimama dhidi ya wenye uthubutu huo?

7. #5 hapo, kulikoni kuwaacha viongozi wetu au awaye yote kukiuka misingi yetu ya uhuru, haki, usawa, au demokrasia Kwa kujua au kutokujua, huku tukikenua kwa uchawa chawa tu kama wa akina Lucas mwashambwa, johnthebaptist, au Kamanda aliechoka; kama inavyotokea kwenye mengi uchwara ya kikristo na kiislamu?

8. Kwani ni siri kuwa wakristo brainwashed kama wewe na MK254 labda ni mburula, mazezeta, viazi mbatata kupitiliza labda kuliko hata wale(ISIS, Alshababu nk) wa kiislam wa kufanana nao?

9. #5 hapo kwa nini mawazo ya yeyote yasipimwe kwa hoja za msingi, kiasi hoja za kijinga hata kama ni za Mbowe, Lissu, Papa, Samia au binadamu awaye yote zipimwe dhidi ya hoja za wengine si Kwa sura au nafasi ya mtoa hoja?

10. Tunahitaji uumini mkomavu uliotukuka baina yetu kama huu:

IMG_20231222_042155.jpg


Vinginevyo labda tukacheze gombesugu tu ndugu zangu kwani tunavyofanya sasa kama viongozi wetu wenyewe ni aina za kina Mpaji Mungu na kelele zao za vyura.

11. Imani zajengwa kwa mafunzo yenye kueleweka; kama Mbowe na Lissu wanalipuuza; maoni ya FaizaFoxy kwako kuhusu Haji Duni yasikilizwe!
 
Back
Top Bottom