Papa Francisko amteua Askofu Ludovick Minde kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi

Papa Francisko amteua Askofu Ludovick Minde kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi

Baba Mtakatifu Papa Francis December 2 mwaka huu amemhamisha mhashamu Ludovick Minde (ALCP-OSS) kutoka jimbo Katoliki Kahama kwenda jimbo Katoliki Moshi.

Mhashamu Minde ni Askofu wa Jimbo la Kahama tangu mwaka 2001.

Mhashamu Ludovick Minde alizaliwa December 9 mwaka 1952 Kibosho mkoani Kilimanjaro, alipata upadre mwaka 1986 na uaskofu mwaka 2001.

Jimbo Katoliki Moshi lipo wazi kufuatia aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Isaac Amani Massawe kuhamishiwa jimbo kuu Katoliki la Arusha.
 
Namtakia utume mwema huko aendako jimboni Moshi. Hongera sana baba askofu Minde kwa kuliendeleza vyema jimbo la Kahama, umelifanyia mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo.
 
Katoliki hamna askofu kijana? Ni vikongwe tu.Kazaliwa 1952 Sasa hivi Ana miaka 67 aiseeee
Non sense,najua una chuki kwa vile tu ni mchaga
Napenda kukufahamisha kuwa katika maaskofu Katoliki nchini ambao wapo jumla 34, maaskofu wachaga pekee ni 11 Sawa na 34% pasuka sasa

Pia kwa mapadre wa jimbo,jimbo Katoliki moshi ndio lenye mapadre wengi kuliko majimbo yote Tanzania,Kama hiyo haitoshi mapadre wa jimbo la Moshi ndio walio wengi nje ya nchi(diaspora) kuliko jimbo lolote
 
Nashangaa Pope hajateua Msukuma kuwa Askofu huko Moshi. Nakata rufaa kwa baraza la makadrinali wa Vatican. Moshi lazima apelekwe askofu toka Chato
Hahaha wale haters wanazidi kubaki Domo wazi wanapoona Moshi ikizidi kuinuliwa na Mungu
 
Uru ataenda lini hospitali ikifunguliwa tunamhitaji Huyu jembe avuke kwa miguu kutoka kibosho machare aone shida zetu anayajua mazingira vizuri
 
Experience inaonesha kwamba Jimbo la Moshi huwa gumu sana kwa WASIO WAZAWA>>>
Huyo ni mchagga aliyezaliwa huko kibosho moshi mwaka 1952. Jina lisikutishe. Kasome story vizuri. Ila kama ni kabila lingine ila kwa miaka aliyoishi kibosho na wazazi wake jua damu imeshabadilikana kuwa ya kichaga hiyo mkuu. Hahaha
 
Non sense,najua una chuki kwa vile tu ni mchaga
Napenda kukufahamisha kuwa katika maaskofu Katoliki nchini ambao wapo jumla 34, maaskofu wachaga pekee ni 11 Sawa na 34% pasuka sasa
Pia kwa mapadre wa jimbo,jimbo Katoliki moshi ndio lenye mapadre wengi kuliko majimbo yote Tanzania,Kama hiyo haitoshi mapadre wa jimbo la Moshi ndio walio wengi nje ya nchi(diaspora) kuliko jimbo lolote

Na ndiyo wasomi kupita maelezo na wanaongoza kiuchumi pia katika majimbo yao. Mweleze pia mkuu kuwa hata mapafre wa mashirika wengi ni wachagga na wamejaa huko Ughaibuni. Waendelee kuwachukia wachaaga maana ni wivu kwa TaifaTeule kama Israel. Hakuna mtu anaweza kushindana na Wachagga. Narudia hayupo. Kwa sasa wamewekwa kando na wao wako busy kupambana pesa. Siku wetesi wakinyanyua vichwa watawashangaa maana si kwa maendeleo hayo. Wao wakikazana kupeana vyeo na kutumbuana wachagga wako busy na mambo yao. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
 
Mabeberu wanatuamulia kiongozi, hii si sawa kabisa. Waafrika tufike mahali tuamue mambo yetu wenyewe.Hawa viongozi sisi ndio tunawajua.
Ni mfumo bora kabisa unaendeshwa na Kanisa Katoliki ndio maana hauwezi kusikia migogoro kama kwenye makanisa mengine wanaojichagulia viongozi,makanisa yemekaa kama vyama vya siasa bhana. Lidumu Katoliki Milele.
 
Back
Top Bottom