Papa Francisko amteua Askofu Ludovick Minde kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi

Papa Francisko amteua Askofu Ludovick Minde kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi

Na ndiyo wasomi kupita maelezo na wanaongoza kiuchumi pia katika majimbo yao. Mweleze pia mkuu kuwa hata mapafre wa mashirika wengi ni wachagga na wamejaa huko Ughaibuni. Waendelee kuwachukia wachaaga maana ni wivu kwa TaifaTeule kama Israel. Hakuna mtu anaweza kushindana na Wachagga. Narudia hayupo. Kwa sasa wamewekwa kando na wao wako busy kupambana pesa. Siku wetesi wakinyanyua vichwa watawashangaa maana si kwa maendeleo hayo. Wao wakikazana kupeana vyeo na kutumbuana wachagga wako busy na mambo yao. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
Acha sifa za kijinga, wamissionari walikaa sana moshi ndio maan wapo wengi
 
Ni mfumo bora kabisa unaendeshwa na Kanisa Katoliki ndio maana hauwezi kusikia migogoro kama kwenye makanisa mengine wanaojichagulia viongozi,makanisa yemekaa kama vyama vya siasa bhana. Lidumu Katoliki Milele.
Unaonaje mfumo huo huo ukatumiwa kwenye SIASA watuwawe na demokrasia ndio maana huwezi kabisa kusikia VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE HUKOUINGEREZA NA MAREKANI?
 
Sikuwahi kujua kama Papa anatuteulia hadi maasikofu wa wetu...
 
Sikuwahi kujua kama Papa anatuteulia hadi maasikofu wa wetu...
Sema sikujua "Beberu" anatuteulia mpaka askofu!
Nddio maana bora haya makanisa ya kilokole wanafanya uchaguzi wao wenyewe, wanachaguana na wakatoliki hawapendi hiyo demokrasia wanataka amtu ateuliwe na mabeberu maana WANA AMINI MABEBERU WAPO KARIBU NA MUNGU ZAIDI.
 
Non sense,najua una chuki kwa vile tu ni mchaga
Napenda kukufahamisha kuwa katika maaskofu Katoliki nchini ambao wapo jumla 34, maaskofu wachaga pekee ni 11 Sawa na 34% pasuka sasa
Pia kwa mapadre wa jimbo,jimbo Katoliki moshi ndio lenye mapadre wengi kuliko majimbo yote Tanzania,Kama hiyo haitoshi mapadre wa jimbo la Moshi ndio walio wengi nje ya nchi(diaspora) kuliko jimbo lolote
Unafiki!! majungu !!!rohombaya!!!uchonganishi vinalitafuna kanisa!! wakatoliki tubadirike!!!
Kwa mipango alokuwa nayo kahama kulikuwa hakuna sababu ya kumuhamisha!!!
 
Non sense,najua una chuki kwa vile tu ni mchaga
Napenda kukufahamisha kuwa katika maaskofu Katoliki nchini ambao wapo jumla 34, maaskofu wachaga pekee ni 11 Sawa na 34% pasuka sasa
Pia kwa mapadre wa jimbo,jimbo Katoliki moshi ndio lenye mapadre wengi kuliko majimbo yote Tanzania,Kama hiyo haitoshi mapadre wa jimbo la Moshi ndio walio wengi nje ya nchi(diaspora) kuliko jimbo lolote
Upo sahihi kabisa
 
Hahahahhaaaaa askofu wa Tanganyika anateuliwa na barua toka italia!
 
Acha sifa za kijinga, wamissionari walikaa sana moshi ndio maan wapo wengi
Historia umekupita sana. Kweli walikuwa Moshi wakazalisha Wakristo wengi. Na pia iko mikoa mwingine walikuwa Wamissionari pia. Kinachoongelewa hapa ni wingi wa mapadre na watawa kutoka Moshi wako wengi duniani wengi na wanaongoza maeneo mbalimbali. Tatizo watu anti kanda ya Kaskazini hasa wachagga hamuwapendi kwa sababu ya maendeleo yao. Wale jamaa wanajielewa sana.
Mpaka sasa wametengwa lakini hawajatetereka. Subiri ifikee 15th December ndiyo utawaelewa. Mipango yako iko palepale
 
Historia umekupita sana. Kweli walikuwa Moshi wakazalisha Wakristo wengi. Na pia iko mikoa mwingine walikuwa Wamissionari pia. Kinachoongelewa hapa ni wingi wa mapadre na watawa kutoka Moshi wako wengi duniani wengi na wanaongoza maeneo mbalimbali. Tatizo watu anti kanda ya Kaskazini hasa wachagga hamuwapendi kwa sababu ya maendeleo yao. Wale jamaa wanaojielewa sana.
Mpaka sasa wametengwa lakini hawajatetereka. Subiri igikee 15th December ndiyo utawaelewa. Mipango yako iko palepale
Tunawachukia kwa kupenda kujisifia bila fact. Nimekwambia wamissionari walibase zaidi moshi na kagera ndio maana kuna mapadri wengi sana maaaeneo. Mim nalijua kanisa katoliki kushinda ukoo wenu wote
 
Ni wacha Mungu pia au ni mapadri wa mshahara tu!!?
Non sense,najua una chuki kwa vile tu ni mchaga
Napenda kukufahamisha kuwa katika maaskofu Katoliki nchini ambao wapo jumla 34, maaskofu wachaga pekee ni 11 Sawa na 34% pasuka sasa

Pia kwa mapadre wa jimbo,jimbo Katoliki moshi ndio lenye mapadre wengi kuliko majimbo yote Tanzania,Kama hiyo haitoshi mapadre wa jimbo la Moshi ndio walio wengi nje ya nchi(diaspora) kuliko jimbo lolote
 
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Ludovick Joseph Minde, ALCP/OSS kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Moshi, nchini Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Askofu Ludovick Joseph Minde alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Kahama. Itakumbukwa kwamba, Askofu Minde alizaliwa tarehe 9 Desemba 1952 kwenye Parokia ya Kibosho, Jimbo Katoliki la Moshi. Ni mtoto wa mzee Joseph Ndasika Minde na Mama Maria Joseph Mukure.

Baada ya masomo yake Seminari Ndogo ya Mtakatifu James, Jimbo Katoliki la Moshi kunako mwaka 1979 alijiunga na Shirika la Mapadre wa Maisha ya Kitume na Kazi ya Roho Mtakatifu ALCP/OSS. Akaendelea na masomo yake ya falsafa Seminari kuu ya Kibosho na kuhitimisha masomo ya taalimungu kwenye Seminari kuu ya Segerea, Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Tarehe 26 Juni 1986 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 24 Aprili 2001 akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 5 Agosti 2001 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, akisaidiana na Askofu Mathew Shija, Muasisi wa Jimbo Katoliki la Kahama pamoja na Hayati Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie wa Jimbo Katoliki la Moshi.

Itakumbukwa kwamba, Askofu Ludovick Joseph Minde, ALCP/OSS ni kati ya Mapadre watano walioteuliwa kwenda Roma kwa masomo zaidi baada ya hija ya kitume ya Mtakatifu Yohane Paulo II nchini Tanzania kunako mwaka 1990. Mtakatifu Yohane Paulo II alitaka kuimarisha malezi na makuzi ya majandokasisi kutoka Tanzania.

Tangu mwaka 1990 hadi mwaka 1995 alikuwa mjini Roma akijifunza Maandiko Matakatifu na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichoko mjini Roma. Ni kati ya wanafunzi waliofanya vizuri sana katika masomo yao kwa mwaka huo.

Katika maisha na utume wake, amewahi kuwa Jaalimu wa Maandiko Matakatifu, Mlezi na Baba wa maisha ya kiroho, Seminari kuu ya Segerea, Jimbo kuu la Dar es Salaam. Itakumbukwa kwamba, Jimbo katoliki la Moshi limekuwa wazi baada ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 27 Desemba 2017 kumteua Askofu Isaac Amani Massawe wa Jimbo Katoliki Moshi, kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo Kuu la Arusha, nchini Tanzania.

Chanzo: Vatican News

Fvck religions
 
Mabeberu wanatuamulia kiongozi, hii si sawa kabisa. Waafrika tufike mahali tuamue mambo yetu wenyewe.Hawa viongozi sisi ndio tunawajua.
akili ako inawaza siasa tu. mfumo wa kumchagua askofu ni wa roman empire system
 
Ni mfumo bora kabisa unaendeshwa na Kanisa Katoliki ndio maana hauwezi kusikia migogoro kama kwenye makanisa mengine wanaojichagulia viongozi,makanisa yemekaa kama vyama vya siasa bhana. Lidumu Katoliki Milele.
Ipo lakini inamalizwa kistaarabu
 
Back
Top Bottom