Papa Sylvester alisoma madrasa. Alifuzu somo la hesabati

Papa Sylvester alisoma madrasa. Alifuzu somo la hesabati

Ni heikima za Allah za kukuzindua akina wewe.
Ni kweli hakujua kusoma wala kuandika lakini kwenye Qur'an kuna mahesabu ambayo hata walimu wake lazima wapewe semina kwanza kuweza kuzielewa
Hizo hesabu ndizo zilizofanyiwa kazi na waislamu na kugundua mambo mengi ya kisayansi mpaka yakamfikia akina Papa Sylvester.
Imani ni shambulio la akili
 
Wajerumani walipoingia Tanganyika hawakupata watu wa kuandika mahesabu ya kodij isipokuwa watu wa madrasa.
Statement yako inafikirisha sana, kwamba hawakupata watu wa kuandika mahesabu ya kodij isipokuwa watu wa madrasa...hii inamaanisha kuwa kulikuwa na watu wa aina mbili au zaidi, je ni watu gani hao ukiwaondoa watu wa madrasa? Hizi dini jamani.
 
Pure propaganda.
Kama kuna wajinga wa hesabu basi madrasa ndio kisima cha hao wajinga. Yaani mtoto akishaanza kupenda madrasa na hesabu huenda zitamkaa maisha yake yote. Kwanini? Watoto kule madrasa huwa wanaenda kukaririshwa nukuu za kiarabu zilizopo kwenye msahafu, wakati hesabu haikaririwi.
Hesabu mzee wangu mpaka za chuo kikuu ni uvumbuzi wa waislamu.
Zimeendelezwa na kubadilika kulingana na wakati lakini muhimu nyingi zimebaki kama zilivyokuwa.
 
Hesabu unazozijua wewe zimeanza madrasa na papa naye alijifunza huko huko
Zikafia wapi hizo hesabu kwenye madrasa maana sasa hivi tunaona tu maustaadhi wakiwa na viboko wakikarorisha watoto aya za kuruani tu za kiarabu
 
Sasa kwa nini huko madrasa hizo fani hazipo sasa hivi?
Nani kakwambia hazipo.
Na nimekwambia wajerumani walipoingia Tanganyika walikuta watu wa madrasa peke yao ndio wanajua mahesabu na kuandika
 
Nioneshe mwalimu wa madrasa anayejua hesabu nami nitakuonyesha maelfu ya watoto wa kiislamu wanaotandika F kwa kwenda mbele kwenye mtihani wa hesabu wa kidato cha nne.
Mimi ni mmoja wa hao walimu wa madrasa na hesabu zipo kichwani.
 
Chuo kikuu kikongwe zaidi duniani ambacho kinaendelea kutoa elimu ni kile kilichopo barani Afrika, nchini Morocco na ambacho kilianza msikitini(masjid) na kuendeshwa kwa mfumo wa madrasa.

Chuo kikuu hicho kilijengwa na bi Fatma kikiambatana na msikiti wakati wa ukhalifa wa Abbasiya ambao ulitawala mashariki ya kati, Ulaya na Afrika. Ukhalifa huo na watangulizi wao walitilia umuhimu mkubwa masuala ya elimu na hivyo kurithisha fikra hizo kwa kila watu wa eneo fulani.

Miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho ni papa Sylevester (2).Somo lililomvutia zaidi ni hesabu wakati huo Ulaya ikiwa haijui hata kuhesabu machungwa.

Mfumo wa kuhesabu hasa kwa kutumia kifaa cha Abacus alichojifunzo kutoka walimu wa chuo cha Alqarawiyen ulimfanya aonekane kama ni mchawi na hiyo ikawa ndiyo sababu ya Ulaya nzima kujifunzo na kuanza kuhesabu kutoka kanisani kwake.

Mahesabu mengine magumu na elimu ya astronomy alichukua kutoka dola ya kiislamu ya Andalasia.

Hakuna sehemu yoyote huyu pope aliwahi kwenda Moroco kujifunza hisabati za kihindu-Arabic.

Huyu alisoma Spain na hakuwahi kwenda huko madrassa. Kama una ushahidi kuwa aliwahi kwenda Moroco tuwekee hapa.
 
Enzi zipi hizo unazokumbuka wewe? Kwenye fani uliyosoma unamkumbuka Mwislam yupi ambaye ulijifunza principles zake?
Mimi namkumbuka Alhwarizm ambaye ndiye muanzilishi wa quadratic equation na ambaye matumizi yote ya aljebra kwenye hesabu yametokana na jina la hesabu zake.
 
Hesabu unazozijua wewe zimeanza madrasa na papa naye alijifunza huko huko
Hesabu zilizanzia Misri ya kale miaka mingi sana kabla Yesu hajazaliwa na kabla Mtume hajafikiriwa kuwepo. Hesabu zilizkuwepo mianka mingi sana kablka ya Ukristo na uislamu. Yale Ma-Piramid yalijengwa miaka mingi sana kabla ya uislamu na ukristo na hesabu zilitumika kufanya calculation.
 
Chuo kikuu kikongwe zaidi duniani ambacho kinaendelea kutoa elimu ni kile kilichopo barani Afrika, nchini Morocco na ambacho kilianza msikitini(masjid) na kuendeshwa kwa mfumo wa madrasa.

Chuo kikuu hicho kilijengwa na bi Fatma kikiambatana na msikiti wakati wa ukhalifa wa Abbasiya ambao ulitawala mashariki ya kati, Ulaya na Afrika. Ukhalifa huo na watangulizi wao walitilia umuhimu mkubwa masuala ya elimu na hivyo kurithisha fikra hizo kwa kila watu wa eneo fulani.

Miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho ni papa Sylevester (2).Somo lililomvutia zaidi ni hesabu wakati huo Ulaya ikiwa haijui hata kuhesabu machungwa.

Mfumo wa kuhesabu hasa kwa kutumia kifaa cha Abacus alichojifunzo kutoka walimu wa chuo cha Alqarawiyen ulimfanya aonekane kama ni mchawi na hiyo ikawa ndiyo sababu ya Ulaya nzima kujifunzo na kuanza kuhesabu kutoka kanisani kwake.

Mahesabu mengine magumu na elimu ya astronomy alichukua kutoka dola ya kiislamu ya Andalasia.

Ikawaje sasa wazungu wakaja kuwazid waarabu na mpaka leo
 
[emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23] maana hata muanzilishi wa dini hakujua kusoma wala kuandika,hivyo vingine unajitungia tu kujifurahisha
Quran 4:11
Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho kiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alicho kiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.

Hayo mahesabu yaliyopo hapo ambayo Mtume Muhammad aliwafundisha waislam karine 6

Wewe jinsi ulivyo kilaza ukipewa Mbuzi 70 uwagawanye Kwa hayo maelezo hapo hauwezi

Hesabu za Alijebra ulizosoma shule msingi wake ndio upo hapo katika hiyo aya

Aliyeandika na kufundisha hizo hesabu alikuwa anaitwa ALLY JABIRi wazungu wakaziita hesabu za Aljebra Ili kuondoa chembechembe za uislam katika somo la hesabu Ili waendelee kuwadanganya vilaza kama wewe
 
Hesabu zilizanzia Misri ya kale miaka mingi sana kabla Yesu hajazaliwa na kabla Mtume hajafikiriwa kuwepo. Hesabu zilizkuwepo mianka mingi sana kablka ya Ukristo na uislamu. Yale Ma-Piramid yalijengwa miaka mingi sana kabla ya uislamu na ukristo na hesabu zilitumika kufanya calculation.
Ni kweli kabisa.
Muhimu hata hizo habari za Pyramid na maajabu yake zilianza kuelezwa na waislamu ndipo akina nyie mkaelewa.
Na kumbuka kuwa uislamu haukuanza na Muhammad saw.Twataraji hata hao wamisri wa kale walikuwa waislamu.
Mtu wa mwanzo kuzichambua kumbukumbu hizo za kale ni Ibn Yussuf.
Ukiacha hilo.Hesabu za wamisri wa Kale zimefanyiwa ukarabati na waislamu na tukapata hizi zinazotumika leo dunia nzima na ndizo alizosoma papa Sylvester na kuwapelekea wakristo wa Ulaya.
 
Ikawaje sasa wazungu wakaja kuwazid waarabu na mpaka leo
Hakuna walipozidiwa.walizubaa kidogo na wakazubaishwa.
Iran pekee ndio kaamka na anajuwa thamani ya elimu ya waislamu.
Huwezi kumzuia kumiliki chochote wakati wavumbuzi wake wote wametokea maeneo yake na jirani mfano Baghdad
 
Si ndio huo uzubaifu. Huwez ukasoma elimu ahera ukamzid aliyesoma elimu Dunia utatawaliwa tu. Iran mwenyewe ananunua teknolijia urusi na North Korea
 
Hakuna sehemu yoyote huyu pope aliwahi kwenda Moroco kujifunza hisabati za kihindu-Arabic.

Huyu alisoma Spain na hakuwahi kwenda huko madrassa. Kama una ushahudi kuwa aliwahi kwenda Moroco tuwekee hapa.
Hili la kuwa alikwenda Morocco bado kuna mjadala.Na uwezekano upo mkubwa
Kuhusu kusoma madrasa na hata wewe umekubali kwa sababu Spain enzi hizo iikuwa ni madrasa tupu ambazo zilikiwishakuzwa na kuwa vyuo vikubwa vya elimu ya juu.Wakiristo na wakazi wa Ulaya walihimizwa na waislamu na wenyewe wakaona umuhimu wa kusoma wakaenda huko.
Mahesabu na maajabu yake katika mfumo tuliourithi mpaka kutufikia sisi yalianza karne kadhaa nyuma Baghdad.
Chuo kikuu cha Alqarawiyen cha Morocco ni sehemu moja wapo zilipopitia elimu za waislamu katika utawala wa Ummawiya na baadae Abbasiya na zikaaingia kwenye madrasa za Spain.
Kwa kifupi papa Sylvester alisoma madrasa na elimu ya madrasa ya chuo kikuu cha Fez ndiyo iliyompaisha naye kuonekana msomi katika kanisa lake.
Nionavyo mimi ikithibitika alikwenda Morocco basi ndio itakuwa unampa hadhi zaidi papa wako na kuonesha wakristo walithamini elimu kuwaiga waislamu ambao ndio waliofuata na kuhamisha elimu pole pole karne kwa karne.
Ukishikilia hakwenda basi itakuwa kinyume chake kwamba elimu ya wakristo ni ya kivivu vivu na hawajafanya juhudi yoyote kuitafuta.walisubiri waletewe kwenye sahani na waislamu.
Weka wazi unachopinga.
 
Ni heikima za Allah za kukuzindua akina wewe.
Ni kweli hakujua kusoma wala kuandika lakini kwenye Qur'an kuna mahesabu ambayo hata walimu wake lazima wapewe semina kwanza kuweza kuzielewa
Hizo hesabu ndizo zilizofanyiwa kazi na waislamu na kugundua mambo mengi ya kisayansi mpaka yakamfikia akina Papa Sylvester.
Tunashukuru ukitutajia hesabu za kwenye Qur'an zinapatikana kwenye aya gani nasi tufanye mrejesho.
 
Ni kweli kabisa.
Muhimu hata hizo habari za Pyramid na maajabu yake zilianza kuelezwa na waislamu ndipo akina nyie mkaelewa.
Na kumbuka kuwa uislamu haukuanza na Muhammad saw.Twataraji hata hao wamisri wa kale walikuwa waislamu.
Mtu wa mwanzo kuzichambua kumbukumbu hizo za kale ni Ibn Yussuf.
Ukiacha hilo.Hesabu za wamisri wa Kale zimefanyiwa ukarabati na waislamu na tukapata hizi zinazotumika leo dunia nzima na ndizo alizosoma papa Sylvester na kuwapelekea wakristo wa Ulaya.
Usiruhusu dini ikaongoza akili yako. Badala yake akili yako ndo iongoze dini.
 
Back
Top Bottom