Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
WanaSimba tunaendelea kutembea mwendo wa Ngiri meno nje kuhusu hawa Vijana, Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute, kwa kadri wanavyozidi kuimarika na kuwa hatari sana Uwanjani, hongera sana Viongozi, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC, haya ndo mambo tulikuwa tunasubiri, kwa WanaSimba.
Pape Ousmane Sakho huyu kwa sasa ndo kiumbe mmoja hatari sana mwenye kuwang'oa wapinzani meno bila kutumia ganzi.
Kama namuona Luis Miquissone hivi kwa mbali, kwa uwezo wake wa kuondoka na Kijiji huku akiteleza mithiri ya samaki kambale pamoja na ubunifu wake na unyumbulifu uliothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika CAF.
Kwa sasa huyu Sakho ni kiumbe kero namba moja Tanzania, ukiachilia mbali Bernard Morrison wakili msomi mwenye uwezo wa kushinda kesi bila kusimama mahakamani.
Sadio Kanoute huyu ni kiumbe boksi to boksi, kiungo matata sana, mtaalamu mwenye kutembea dimba la kati kwa namna anavyotaka.
Huyu mtu sana, achilia mbali game dhidi ya Azam FC, alichofanya game dhidi ya Majirani Kutoka bonde la Jangwa kila mtu anajua, baada ya jina la Dokta kuzimika baada ya game, kama dawa iliyoisha muda wake.
Sakho na Kanoute haya ndo mambo ambayo tunataka Simba SC, hakika Azam FC wamekutana na dawa ya kuua Wadudu Wanaoruka na Kutamaa na hakika ukichagua Simba SC umechagua furaha Mutawalia, Simba SC Klabu Quality yenye kusakata kabumbu la Viwango vya CAF, Mabingwa wa Nchi, Klabu Kubwa na Bora Afrika.
Peter Banda tunasubiri uje kujibu mapigo haya ya Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute pomoja na kipaji chako cha kusakata kabumbu, bado nafasi unayo na umri unaruhusu pia.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.