Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute' Haya ndiyo mambo tulikuwa tunataka Simba SC

Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute' Haya ndiyo mambo tulikuwa tunataka Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
WanaSimba tunaendelea kutembea mwendo wa Ngiri meno nje kuhusu hawa Vijana, Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute, kwa kadri wanavyozidi kuimarika na kuwa hatari sana Uwanjani, hongera sana Viongozi, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC, haya ndo mambo tulikuwa tunasubiri, kwa WanaSimba.

Pape Ousmane Sakho huyu kwa sasa ndo kiumbe mmoja hatari sana mwenye kuwang'oa wapinzani meno bila kutumia ganzi.

Kama namuona Luis Miquissone hivi kwa mbali, kwa uwezo wake wa kuondoka na Kijiji huku akiteleza mithiri ya samaki kambale pamoja na ubunifu wake na unyumbulifu uliothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika CAF.

Kwa sasa huyu Sakho ni kiumbe kero namba moja Tanzania, ukiachilia mbali Bernard Morrison wakili msomi mwenye uwezo wa kushinda kesi bila kusimama mahakamani.

Sadio Kanoute huyu ni kiumbe boksi to boksi, kiungo matata sana, mtaalamu mwenye kutembea dimba la kati kwa namna anavyotaka.

Huyu mtu sana, achilia mbali game dhidi ya Azam FC, alichofanya game dhidi ya Majirani Kutoka bonde la Jangwa kila mtu anajua, baada ya jina la Dokta kuzimika baada ya game, kama dawa iliyoisha muda wake.

Sakho na Kanoute haya ndo mambo ambayo tunataka Simba SC, hakika Azam FC wamekutana na dawa ya kuua Wadudu Wanaoruka na Kutamaa na hakika ukichagua Simba SC umechagua furaha Mutawalia, Simba SC Klabu Quality yenye kusakata kabumbu la Viwango vya CAF, Mabingwa wa Nchi, Klabu Kubwa na Bora Afrika.

Peter Banda tunasubiri uje kujibu mapigo haya ya Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute pomoja na kipaji chako cha kusakata kabumbu, bado nafasi unayo na umri unaruhusu pia.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.
 
Nyie mikia siku ile ya derby hao wote si mliwatoa nje?na mkaanza kulalamika kua viongozi wamesajiri vitoto...Yanga hii hebu ipe heshima yake ...alaa huna adabu hata kidogo.
 
Ila anatakiwa afanyie mazoezi sana upande wa kupiga pass ndefu, bado anazingua. Kama uliangalia vizuri game ya jana na hata zilizopita(Mimi binafsi huwa napenda kumuangalia kwenye hicho kipengele) bado accuracy yake kwenye long pass ni shida.

Sio mbaya ajifunze kwa Master long pass Jonas Nungunungu Mkude. Akirekebisha na hapo atakua msaada mkubwa sana kwa timu mara 4 zaidi ya sasa. All in all jamaa ni shidaaaaa💪💪💪💪
 
Ila anatakiwa afanyie mazoezi sana upande wa kupiga pass ndefu, bado anazingua. Kama uliangalia vizuri game ya jana na hata zilizopita(Mimi binafsi huwa napenda kumuangalia kwenye hicho kipengele) bado accuracy yake kwenye long pass ni shida. Sio mbaya ajifunze kwa Master long pass Jonas Nungunungu Mkude. Akirekebisha na hapo atakua msaada mkubwa sana kwa timu mara 4 zaidi ya sasa. All in all jamaa ni shidaaaaa[emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
Kwenye kupiga long pass kuna mambo mawili, inaweza kuwa mpokeaji ni wapi pa kupokelea hizo ndefu au mpigaji anapigaje..!

Kwa game ya Azam FC jana Kanoute amepiga long pass ambazo baadhi zilifika kwa Kapombe na zingine zilipotea

Ni wakati Kocha kulifanyia kazi
 
Nyie mikia siku ile ya derby hao wote si mliwatoa nje?na mkaanza kulalamika kua viongozi wamesajiri vitoto...Yanga hii hebu ipe heshima yake ...alaa huna adabu hata kidogo.
Wapi mashabiki wenye maono walilalamika?

Hivi Kanoute alipozima zile tambo za akina Aucho na Faisal pale katikati ya dimba hukuona?

Au lile shuti aliopiga Kanoute golikipa wenu akakata Network na kutibiwa kwa dakika kadhaa hukuona?
 
Huyo jamaa hawezi kukaa hata sub kwenye kikosi cha Yanga
 
Ila anatakiwa afanyie mazoezi sana upande wa kupiga pass ndefu, bado anazingua. Kama uliangalia vizuri game ya jana na hata zilizopita(Mimi binafsi huwa napenda kumuangalia kwenye hicho kipengele) bado accuracy yake kwenye long pass ni shida. Sio mbaya ajifunze kwa Master long pass Jonas Nungunungu Mkude. Akirekebisha na hapo atakua msaada mkubwa sana kwa timu mara 4 zaidi ya sasa. All in all jamaa ni shidaaaaa[emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
Hapana jna nilimhesabia nipasi ndefu 3 tuu ndizo alizopoteza

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kila kitu lazima mjifananisha na Simba?
Sasa watafanyaje na wao kila kitu wanataka kutoka kwa Simba SC.

Kumbuka kuna wakati Yanga tulikuwa tukiwaita Yanga ni Simba B kwa rundo la wachezaji kutoka Simba.

Na sasa Viongozi, kutoka Simba kwenda Yanga, Senzo, Msemaji na sasa wanamtamani CEO.
 
WanaSimba tunaendelea kutembea mwendo wa Ngiri meno nje kuhusu hawa Vijana, Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute, kwa kadri wanavyozidi kuimarika na kuwa hatari sana Uwanjani, hongera sana Viongozi, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC, haya ndo mambo tulikuwa tunasubiri, kwa WanaSimba...
Hii thread naenda kuitolea sadaka kanisani
 
Huyo jamaa hawezi kukaa hata sub kwenye kikosi cha Yanga
Sakho ni mchezaji bora wa msimu wa 20/21 kwenye ligi kuu ya Senegal, akiwa na mabao sita na assts 6 kwenye Ubingwa wao Klabu ya Teungueth.

Na saaa yupo kwa Mabingwa wa Nchi na Wawakilishi wa Kimataifa, huko kwenu nani anasifa hizo? Huko alikotoka?
 
Back
Top Bottom