Parachichi moja Ufaransa Tsh 6000

Parachichi moja Ufaransa Tsh 6000

Je hii taarifa umeitoa wapi?
Je unafahamu GDP ya ufarasa? (Hapa ili uelewe elewa huu mfano: Hapo Zimbamwe parachichi moja lauzwa Milioni 20)
Je unafahamu gharama halisi za kulifikisha sokoni hilo parachichi moja?
Acha sigara! 6000 anayozungumia ni 6000 kwel yaan kama $2.25 hv sio huo uchafu wa zimbabwe ambao ukibadilisha inaweza isifike dola moja.
 
Sio tu parachichi ukaliona pale Njombe au Mbeya lina sifa za kwenda Ulaya

Kuna vigezo vingi vinahusika mpaka lipate qualifications za kuingia Ufaransa

Kuna mwamba alipambana sana afikie vigezo ili auze Ulaya, kikaja kumwangusha kugezo kimoja tu mwishoni jinsi alivyoyachuma kutoka kwenye miti yake wakamkataa akafeli akaishia kuyauza hapahapa Bongo
 
Hahaaa!! Asilimia 90 ya parachichi zinazoliwa Tz, hazina sifa ya kuliwa ULAYA!! tambua hilo.
sio kweli mkuu, kuna parachichi aina ya hass na wesso ni parachichi pendwa huko ulaya ambapo tanzania inazalisha kwa wingi na madalali wakubwa ni kutoka kenya.
 
ni kweli kwa tanzania urasimu wetu ndo unatupa shida huezi amini sisi tunazalisha mara 10 ya kenya ila kenya ndo anaitwa mzalishaji na exporter wa parachichi sababu ya process ndogo sana grading(ubora,ukubwa) na urahisi wa ku export jamani na kenya anatoa maparachichi mengi tanzania mwisho wa siku yeye ndo anachukua tittle ya producer mkubwa http://files.eacce.org.ma/pj/[1569600032]Kenya.pdf. ....sujui lini tutafungua macho kama kwenye tanzanite tz tunatumika vibaya sana sababu ya viongozi wetu kukosa maono na kurahisisha urasimu wakupeleka vitu nje mwisho ....mungu atusaidie
Hakika mkuu viongozi wetu bado ni changamoto sana Aisee
 
Parachichi zinazoliwa Tanzania ni zipi na zinazoliwa ulaya ni zipi?
Ulaya parachichi ni hivi vidogo vidogo vyenye ngozi yenye ''ukurutu''. Yanachukuwa muda mrefu kuiva. Haya makubwa sijawahi kuyaona kwa wingi na sijui sababu ni kuiva haraka au kuna sababu nyingine
1718033561004.jpeg
 
Back
Top Bottom