PAROKO: Tusikae kimya sasa kusubiri Miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari.

Wao kanisa wanaandika lini kitabu cha kujutia kuwa mawakala wa Wakoloni ( Majambazi wa rasilimali) Afrika ?

Kitabu cha kujutia kuratibu mauaji ya Kimbari na Wayahudi kinatoka lini?
Wanazidi kugonga spana tu 😂
Wajibuni kwanza hoja za bandari kisha mlete hizo zenu
 
hata Royal tour tulipinga na kukejeli sana lakini baad ya mafanikio yake tumeufyata …angalau Bagonza juzi amekiri mafanikio ya sakta ya Utalii

msijipe umungu wa kujifanya mmeshaiona 2030!
 
hata Royal tour tulipinga na kukejeli sana lakini baad ya mafanikio yake tumeufyata …angalau Bagonza juzi amekiri mafanikio ya sakta ya Utalii

msijipe umungu wa kujifanya mmeshaiona 2030!
Mafanikio yapi na Dola imekuwa finyu?

Au siku hizi Wazungu na watalii wanakuja na Pesa ya madafu ya TShilings?

Namba hazidanganyi.
 
hata Royal tour tulipinga na kukejeli sana lakini baad ya mafanikio yake tumeufyata …angalau Bagonza juzi amekiri mafanikio ya sakta ya Utalii

msijipe umungu wa kujifanya mmeshaiona 2030!
Takwimu za kubumba kuonesha Royo tua imefanikiwa
 
Kumshambulia Paroko haisaidii, Jibu hoja
Hana hoja ana mitazamo ya kijamaa wakati dunia ni ya ushindani isiyo na huruma hata kidogo.

Huwezi kujitetea unapotaka kuukwepa uwekezaji kwa mawazo ya kijamaa wakati uzembe mwingi kwenye sekta ya elimu ukiendelea kutukosesha sifa za kuajirika kwenye masoko ya kazi kimataifa.

Profesa Assad akisema ukweli anachukiwa na kuishia kufukuzwa kazi, lakini huo ndio ukweli ambao Mzee Lowassa alishausema pale jangwani, kwamba elimu ni kila kitu kwetu sisi haswa katika kufanya mipango mikubwa kama hii wanayoifanya DP World.
 
haya majamaa yana akili sana😂😂

mpaka sasa tunchojua tukimwona mwarabu hapa bandari nu kwamba mama kakataa kushauriwa.
Tukimuona Bandarini tu tunajua Maza amekataa kushauriwa 😂😂
Huko Mbeleni asitudanganye anajutia
 
Wapi walipopinga Uwekezaji
Watu wanapinga Mkataba Mbovu sio Uwekezaji
 
Wanazidi kugonga spana tu [emoji23]
Wajibuni kwanza hoja za bandari kisha mlete hizo zenu
Hoja ipi? ya kusema hawataki kabisa uwekezaji kwa kigezo kuwa tunayo local capacity?…hiyo hoja angeisema Gwajima au Mwamposa ningemuelewa kwa kuwa ana autonomy ya kuongoza kanisa lake 100%, hao wengine kila kitu wanategemea Muongozo kutoka Ulaya halafu wanashangaa Serikali kualika wawekezaji wa nje?

inakuaje huu uchungu wa Bandari hawakuwa nao wakati migodi ikibinafsishwa kwa wazungu?
 
DP World atakapoanza kazi pale bandarini atatafuta wenye elimu awatumie, lakini ipo fursa ya kuwaendeleza wataalam wetu wazalendo kupitia mafunzo ya masuala ya bandari katika vyuo vyetu tulivyonavyo, na tuitumie fursa hii na sio kuishia kulia wivu kila anapotaka kuja mwekezaji fulani.
 
Wapi kwenye TAMKO waliposema wanapinga Uwekezaji?
N.B - Kwani ile gesi ya Mtwara tumeshafaidika nayo kwa kiasi gani?
 
Haya mliyasema wkt wa Uwekezaji wa Gesi kule Mtwara ila hatuoni chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…