Hana hoja ana mitazamo ya kijamaa wakati dunia ni ya ushindani isiyo na huruma hata kidogo.
Huwezi kujitetea unapotaka kuukwepa uwekezaji kwa mawazo ya kijamaa wakati uzembe mwingi kwenye sekta ya elimu ukiendelea kutukosesha sifa za kuajirika kwenye masoko ya kazi kimataifa.
Profesa Assad akisema ukweli anachukiwa na kuishia kufukuzwa kazi, lakini huo ndio ukweli ambao Mzee Lowassa alishausema pale jangwani, kwamba elimu ni kila kitu kwetu sisi haswa katika kufanya mipango mikubwa kama hii wanayoifanya DP World.