Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge

Hii iishie humu humu jf, ikitoka tuu nje, ikachapishwa na gezeti lolote, jiandae kuitwa Dodoma!.
Usije kusema hukujua, niulize mimi mwenzio, yalinikuta yepi?.
P
 
 
Mkuu MADOTTO, asante kunianzishia thread. Mtu aliyepitia mapito kama haya, akaja ku emerge victoriously akitokea akapata uongozi, atakuwa ni kiongozi mzuri sana, maana amepikiwa kwenye tanuru la moto!.
P
 
Pascal ana hoja.
Mkuu Arushaone , sio tuu nilikuwa na hoja, bali nilikuwa na hoja ya msingi!.
Ni kweli kuwa muhimili wa bunge unaingiliwa sana. Mfano halali ni pale mkuu wa kaya alipomwambia spika awashughulikie wapinzani ndani ya bunge, wakitoka nje ana deal nao. Ile ni kama amri na imeingilia madaraka ya spika.
Haya naomba tuyaache!.
Tanzania inapotea kidemokrasia
Ilipotea sasa inarudi kwenye mstari.
P
 
Pascal Mayalla najua wewe ni akili kubwa,
kila la heri kwenye mahojiano
Mkuu Obama wa Bongo, kwanza asante, naomba niwe mkweli ili nisilewe sifa, mimi sio akili kubwa!, mimi ni akili za wastani!. Akili kubwa ni wale Ph.D holders!. Ila sio kila kitu ni lazima akili kubwa!. Tumeshuhudia mambo ya Blaza wangu akili kubwa compared to sasa akili za wastani!
Niombee tuu hili jambo langu la sasa lifanikiwe!.
P
 
Kila la kheri Pascally, mateso yako yanaweza kuwa thamani kubwa kwa kizazi kijacho na wanao pia, bila shaka utawaambia ukweli bila kuficha lolote.
Mkuu sifongo, thanks for this, I believe this, hata yule YEYE, ni kwa kupigwa kwake, sisi tuliponywa, hivyo haya mapito niliyopita kuna watu wataponywa!. Ni vile tuu sijatoa mrejesho wa hili in public lakini kiukweli nimelisaidia sana taifa hili kupitia Bunge hili, sasa nataka kwenda kulisaidia taifa kule!.
Mungu nisaidie!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…