Pascal Mayalla alimtabiria Paul Makonda kuwa mgombea urais wa CCM 2025. Je, unabii wake utatimia?

Kwa vile 2025 bado, tuendelee kusubiria, ila sasa kuna tatizo hili
Asante Sana kwa taarifa hii, naomba Mimi Mwanajeiefu mwenzenu, niwe mtu wa kwanza kuwajulisha kuwa hii vita ya kutaka kumdhalilisha mpakwa mafuta wa Bwana, Paul Makonda, sasa ndio mwanzo WA mwisho wa hasidi huyu!. Karma ndio itamaliza kila kitu. Simaanishi Makonda ni malaika, bali, ni binaadamu kama binadamu wengine, hakuna mkamilifu, hivyo na yeye kuna makosa ametenda na tayari karma imeisha mshughulikia, hivyo kwa maonevu anayotendewa na hasidi huyu, ni Mungu, Baba ndiye atamlipia.
Kwanza mafanikio yake ni kutoka kwa Mungu. Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Kisha, Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Hivyo, hata kampeni batili ya kutaka kumpora kiwanja, ni upepo tuu na utapita.

Watu kumfanyia fitna na majungu, Makonda, hawakuanza leo Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .

Yote haya yatapita, na Makonda atasimama.
P
 
Kugombea ni jambo moja na kupata kura ni jambo jingine. Lakini sio kwa CCM hii ya wanafiki ambao huwa wanampa kura Rais kwa asilimia 💯. BTW huyo bwege asahau kabisa.
 
Mkuu Yohana Mbatizaji, johnthebaddest , hii ngoma bado iko very valid!
Mkuu Lord denning , you might be right kwenye yote hayo, kwasababu hakuna mkamilifu, ila human beings are not static, they are dynamics and hence, they change with time. Kwa mapito aliyoyapitia amejifunza humility, he will be the best of the best!.

Ili kumjua vizuri, anzia hapa Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Kisha Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Akawa RC wa DSM na akafanya makubwa ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwenye tanuri la moto kupikwa akaiva kisawasawa

Kwa wale mnaopenda kujua mapito aliyo yapita karibuni pande hizi
Najua kuna watu bado hawaamini hili linawezekana, naomba kuwathibitishia, lisilo wezekana kwa binadamu, kwa Mungu linawezekana!.
P
 
Yule naye ni bendara fuata upepo
 
"Neno litasimama
Neno litasimama
Neno litasimama
Mambo yote yatapita
lakini Neno litasimama!."

Hii ni chorus ya wimbo fulani!.
P
 
Labda
 
Labda mgombea Urais wa wasukuma!
 
Unaweza kutimia
Wanabodi, kwenye bandiko hili Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... nilishauri
Hata baada ya kuteuliwa kuwa Mwenezi wa CCM, Paul Makonda bado anapigwa vita na wasiomtakia mema, wasioitakia mema CCM na wasio itakia mema Tanzania.

Japo Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mamlaka kuu ya nchi ni wananchi, kupitia katiba, serikali ya CCM ilifanya mabadiliko ya katiba kinyume cha katiba na kupoka ukuu wa mamlaka kuu ya wananchi, na kuikakabidhi kwa chama cha siasa, ambapo sasa mamlaka Kuu ya nchi ni chama tawala, CCM ndio imeshika hatamu kuongoza serikali, hivyo katika ukuu wa chama, CCM ndio kila kitu, hivyo Makonda kama msemaji wa CCM, kikao cha CCM kinaweza kumwagiza Rais wa JMT atekeleze jambo lolote lililoelekezwa kwenye ilani ya CCM, Katibu Mwenezi ndie msimamizi wa ilani ya CCM, ana mamlaka yote ya kumuamrisha hadi Rais wa JMT, atekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo Makonda yuko very right kumuamrisha Waziri Mkuu na kumpa ultimatum ya miezi 6 kumaliza migogoro yote ya ardhi ya nchi hii.

Na baada ya miezi 6, kama Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa atashindwa kuitatua migogoro yote ya ardhi, atakuwa ni ameshindwa kazi, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, itakutana na kumuagiza Rais wa JMT, kumuondoa Waziri Mkuu, kwa kushindwa kazi na kumteua Waziri Mkuu mwingine mwenye uwezo.

Hata ikitokea Rais Samia ameshindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, chama kinaweza kumfuta uanachama na hivyo kupoteza urais!, hivyo Mwenezi wa CCM ni mtu mkubwa sana, kuliko serikali yote ya Tanzania, na hii ndio maana halisi ya Party Supremacy, CCM ndio imeshika hatamu za kuiongoza serikali ya Tanzania .

Hongera sana Mwenezi mpya wa CCM, Paul Makonda, kuiheshimisha CCM, endelea kutoa maagizo na ultimatum kwa viongozi wote kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, wewe ndiye msimamizi wa ilani ya CCM!.

Angalia ilani ya CCM imeelekeza nini kuhusu Bunge la JMT, toa maelekezo kwa Spika with ultimatums, Spika akishindwa kutekeleza Spika anaondolewa!, enzi za Spika Sitta, aliponea chupu chupu kuondolewa, kuna mtu mmoja very powerful ndani ya CCM aitwae "The King Maker" ndie alimuokoa Spika Sitta kwa kumpa maelekezo Mwenyekiti wa CCM, JK, na hii ndio salama yake!.

Makonda angalia ilani ya uchaguzi ya CCM inasema nini kuhusu mhimili wa Mahakama, toa maagizo with ultimatum kwa Jaji Mkuu atekeleze.

Angalia ilani ya uchaguzi inasema nini kuhusu majeshi, ulinzi na usalama, toa maelekezo with ultimatum kwa Amiri jeshi Mkuu na kwa Mkuu wa majeshi, IGP , etc.

Ila kwa nafasi ambazo sio za kichama kama Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, CAG, Mwenyekiti wa NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utawala Bora na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ambao ni wateule wa rais, Paul Makonda anaweza kuwapa maelekezo bila ultimatums kwasababu hawa chama hakiwezi kuwafanya chochote, na badala yake, chama kitampa maelekezo mamlaka yake ya uteuzi ambaye ni Rais wa JMT, awaondoe!.

Kiukweli ninamkubali sana Paul Makonda!, Tangu nilipoanza kumkubali Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
He has never let me down!. Tena niliwahi kushauri Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... ushauri huu still stands, kwasababu miaka hii 4 ya Mama ni kumalizia awamu ya Magufuli, awamu ya baada ya Magufuli inaanza 2025, ila Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo you never know with politics, everything is possible!.

Paul Makonda kanyaga mwendo, chapa kazi, kazi iendelee!.
Paskali.
 
Arusha ni mapito tuu, Nampongeza huyu Mwamba, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha , ambao ni Geneva ya Africa.

Ila kwa maoni yangu, hii teua, tengua, hamish, na tumbua ya Rais Samia, is not healthy at all!, it's a sign of weakness mahali!.

My honest opinion, CCM haina mtu mwingine yeyote ambaye ni the best kwenye uenezi zaidi ya Makonda!.
Ili Rais Samia afanikiwe, asiwasikilize sana wahafidhina wa CCM, sometimes
wanamuingiza chaka!, kama hili la kumuondoa Makonda kwenye uenezi na kumpelekea RChuga , kiukweli kabisa hapa wahafidhina wa CCM, wamemuingiza Mama chaka.

Japo siungi mkono hizi teua leo badilisha kesho, Waenezi 5, ndani ya miaka 5!
1. Polepole
2. Shaka
3. Mjema
4. Makonda
5. The upcoming one!.

Hi sio picha nzuri!, ila nasisitiza kuna tatizo kidogo mahali Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda tuendelee kumpa muda, ata stabilize.

Hongera Paul Makonda kurudishiwa u RC, very soon itathibitika huyu aliyepo kwenye u RC wa Mkoa wetu hawezi!, soon utarudishwa RC DSM, jiji litanyooka!.
P
 
Naunga mkono 100%
 
Wasukuma ndo mambo kama haya yanayowafanya mnaonekana washamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…