Huko Lumumba huwa hamuwazi kitu kingine zaidi ya madaraka? Kwa usije na uzi wa namna ya kuifanya Tanzania Developed country? Vijiji vyote karibia elfu 20 viwe na umeme, maji ya bomba, kituo cha afya kila kijiji, barabara za lami kuunganika kila Kata. Kila kijiji kiwe na sekondari, kila kata iwe na chuo cha VETA, kiwanda cha Sido, Hispita ya Rufaa, TV na Redio ya Kata.... Kwa nini hamuwazi hayo? Ni ufinyu wa akili au ni nini hasa? Yaani hata mwezi hatujamaliza toka tumalize uchaguzi, yaani hata baraza la mawaziri halijaundwa ili waanze kutekeleza ahadi na ilani za uchaguzi, tayari mnawaza next election. Vichwani mmejaza nini?? Funza au ni nini hasa?? Halafu kwa nini usijiwazie wewe mwenyewe kuwa basi huyo rais wa 2025 badala yake unamuwazia mwenzio?? Wewe huna unachokiweza zaidi ya kujipendekeza kwa binadamu wenzio??