Uchaguzi 2020 Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Uchaguzi 2020 Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Tatizo la kujazana li chama li moja kutoboana ugali wakati kuna options kibao za kimaisha, sasa bado tunaisubiri AIBU ya mchunga kondoo wa bwana !!
 
Jamaa yangu Pascal Mayalla lazima amwagwe kwa kishindo uchaguzi maoni CCM Kawe baada ya kujiita KITIMOTO eti kwa vile aliendesha kipindi cha KITIMOTO miaka zaidi ya 20 iliyopita wakati wengi walikuwa hawajazaliwa miongoni mwa wapigakura humo ukumbini.

Nani mshauri wa huyu mtaka ubunge aliyempotosha? Mayalla asije ambulia kura 2 akatulilia hapa JF
Huyo na Stive Nyerere, Mpoki na Kingwendu hawana tofauti na usishangae akaibuka na kura 0
 
Ametia nia, akikosa sidhani kama ni dhambi, kaonyesha ukomavu kujipima kwa wana ccm wenzake wa Kawe anakubalika kwa kiasi gani.
 
Tumia akili kidogo basi! Kama kipindi kilikuwepo 1994 ni miaka 26 iliyopita. Mwenye miaka 36 hajui hata maudhui ya kipindi kile maana walikuwa na miaka 10 tuu, jee umeelewa? Maana nimesema zaidi ya miaka 20
Huo mwaka 1994 ndipo ITV ilipoanzishwa, na hata baadhi ya mikoa ilikuwa haikamati. Vipindi kuanza kuchanganya (kikiwamo KITIMOTO) ni miaka mingine mbele ya 1994. Umeteleza kusema miaka 20, kubali tu haukuwa na hoja pale
 
Jamaa yangu Pascal Mayalla lazima amwagwe kwa kishindo uchaguzi maoni CCM Kawe baada ya kujiita KITIMOTO eti kwa vile aliendesha kipindi cha KITIMOTO miaka zaidi ya 20 iliyopita wakati wengi walikuwa hawajazaliwa miongoni mwa wapigakura humo ukumbini.

Nani mshauri wa huyu mtaka ubunge aliyempotosha? Mayalla asije ambulia kura 2 akatulilia hapa JF
Huyu jamaa ni wa hovyo. Maana kipindi chake hicho kilisaidia sana kuibomoa NCCR-MAGEUZI.
 
Pasco akizidiwa kura na Mashinji au Mwijaku nitacheeeeka!

Uchaguzi huu umeonyesha ni jinsi gani watu walivyo na njaa.

Jofrey Mizengo Pinda na yeye ameshakarishwa chini na mwanamke huko Katavi.

Kumbe mzee Pinda zile siiifa zote kwa mkulu ilikuwa ni kumtafutia ulaji mwanaye Jofrey.

Yajayo yanahuzunisha.
 
kama kweli Pasco ndio gia yako hiyo mkuu kujiita KITIMOTO umetuangusha!! WAJUMBE waislam ushawakwaza!! kwanini hakutuambia wanajukwaa tukupe agenda balozi wetu JF?
1.Ajira kwa raia wenye hali ngumu Kawe hasa vijana
2. Mikopo ya Bodaboda kwa masela
3.Mikopo ya biashara kwa kinamama yenye masharti nafuu
4.Kodi zipunguzwe kwa wafanyabiashara za maduka kutwa wanafunga wakisikia TRA wako mtaani kwao
5.Kushawishi serikali kuweka bajeti kubwa jimboni kwake huduma za jamii
6. Hiyo yake ya kugawa mil 10 kila kata
Ukiwa mwanasiasa wa ccm jua unatakiwa usiwe na akili.
 
Back
Top Bottom