Uchaguzi 2020 Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Uchaguzi 2020 Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Jamaa yangu Pascal Mayalla lazima amwagwe kwa kishindo uchaguzi maoni CCM Kawe baada ya kujiita KITIMOTO eti kwa vile aliendesha kipindi cha KITIMOTO miaka zaidi ya 20 iliyopita wakati wengi walikuwa hawajazaliwa miongoni mwa wapigakura humo ukumbini.

Nani mshauri wa huyu mtaka ubunge aliyempotosha? Mayalla asije ambulia kura 2 akatulilia hapa JF
Mwanakulitafuta huyo
 
Duuh hakika wajumbe wa kawe ni wanafunzi wa O level kama miaka 20 hamukuzaliwa
Hata kama walizaliwa isingewezekana waache lufuatilia katuni wafuatilie kipindi cha KITIMOTO cha akina JOSHUA MWAITUKA , halafu Pascal atakuwa kaleta uongo ili kupata kura za huruma , kile kipindi hakikuwa chake yeye alilipwa ujira wake kwa kuwa mshereheshaji tu , mimi ni miongoni mwa waliohudhuria kipindi kile.

Kama jambo dogo vile analitengenezea uongo je akipewa ubunge ?
 
Paskali umetuangusha,ungeomba ushauri humu tukupe vitu vya msingi ungetoa kama ahadi-

1. Ungesema kwamba wakazi wa kawe wangepewa vipaumbele kupangisha yale majengo ya NHC.

2. Ungefufua Tanganyika Packers ili watu wauziwe Nyama kilo Tsh elfu 3 na kutengeneza ajira kwa wakazi wa kawe.

3.Kawe Ukwamani ungeipima yote ile na kulipa watu fidia.

4.Ungejenga kituo kikubwa cha daladala cha kisasa Kawe.

5.Ungejenga kwa kiwango cha lami barabara zote kubwa zinazounganisha wilaya moja na nyingine...eg Mbopo-Msumi-Kimara

6.Utajenga Mwendo kasi kuanzia Mwenge hadi Bunju Sokoni.

Hizo ni ahadi tu sio lazima ziwe kweli au uzitekeleze hata kama wewe hausiki lengo ni kutoa ahadi hata kama ni hewa kama alizotoa Mh mil 50 kila kijiji,latop kila mwalimu etc
 
Kumbe Mbunge ndio hujenga hayo madude ?
 
Jamaa yangu Pascal Mayalla lazima amwagwe kwa kishindo uchaguzi maoni CCM Kawe baada ya kujiita KITIMOTO eti kwa vile aliendesha kipindi cha KITIMOTO miaka zaidi ya 20 iliyopita wakati wengi walikuwa hawajazaliwa miongoni mwa wapigakura humo ukumbini.

Nani mshauri wa huyu mtaka ubunge aliyempotosha? Mayalla asije ambulia kura 2 akatulilia hapa JF
Zamani alikua akijinasibu kuwa yeye yupo neutral sio mwanachama wa chama chochote ila nashangaa sikuhz anaonesha uhalisia wake
 
Miaka 20 iliopita wapiga kura walikuwa hawajazaliwa?
Hawajafikisha hata miaka 18 walau kipindi hicho cha ya kujua kipindi chake cha kitimoto ni nini.Katumia wrong strategy.

Tulimuuliza humu aseme anagombea chama gani akawa anaficha ficha kuogopa kupopolewa mitusi na Chadema ambao humu Jamii forums alikuwa akiandika mada zinazowafurahisha furahisha akajisahau kujipanua wazi ajionyeshe yuko upande gani akatuachia Ya CCM tupambane wenyewe akina sisi ambao hakuna asiyetujua kuwa ni CCM HUMU JAMII FORUMS.
 
Ni kweli hili unalosema? Hao wajumbe kwa hiyo wana miaka 19 kushuka chini, sio?
Wajumbe hapo ukitaka wakuelewe vibaya taja miaka hiyo 20 iliyopita unayoongelea kinachowajia wajumbe kichwa ni kuwa huyu mayala ni kibabu kizee kinaongelea mambo ya miaka 20 iliyopita kizee kikongwe hiki watakunyima kura .Hakujiandaa.

Halafu nimefuatilia mitandaoni hicho kipindi kilifutwa sababu Mayala alikuwa akialika watu wanaiponda serikali ya CCM.MZEE MENGI AKAAMUA KUKIFUNGA ASIGOMBANE NA SERIKALI
 
Pasco nimekupa ajenda 6 in my previous comment, zitumie utashinda Kawe na hata ukipoteza Kawe tulia kama Mwigulu usikashifu wala kulalamika manake sote tunajua fitna na figisu za siasa zetu za majitaka wana JF tunaamini tayari wewe ni mbunge material nae Mkulu atakupa viti Maalum na uwaziri wa Habari manake Makyembe tayari kifo cha mende huko Kyela miguu juu!!

Mkulu anajua unavyopigania maslahi ya chama na taifa mtandaoni bila malipo nawewe ni kada mtiifu kwake na kwa chama chetu this time tunamuomba Mh Rais Magufuli kalamu yake ya uteuzi wa uwaziri ikupitie ni haki yako na vile njaa imetukaba sisi wote pamoja nawewe wewe ukipata wana JF nasi tumepata!

kumbuka Pasco zile ajenda 6 ni swagga tu za wewe kujiuza mbele ya wajumbe si lazima uzitekeleze zote ukipata ubunge kwa kuwa utakutana na changamoto million na kuna watu watakukwamisha!!

Jiite vile unapenda Pasco aka ‘Kwa maslahi ya taifa’ sio Kitimoto, namimi ni meneja wako wa kampeni for free unasemaje?
 
Hawajafikisha hata miaka 18 walau kipindi hicho cha ya kujua kipindi chake cha kitimoto ni nini.Katumia wrong strategy.

Tulimuuliza humu aseme anagombea chama gani akawa anaficha ficha kuogopa kupopolewa mitusi na Chadema ambao humu Jamii forums alikuwa akiandika mada zinazowafurahisha furahisha akajisahau kujipanua wazi ajionyeshe yuko upande gani akatuachia Ya CCM tupambane wenyewe akina sisi ambao hakuna asiyetujua kuwa ni CCM HUMU JAMII FORUMS.
Exactly... kwenye threads zake zote alikua anaanza na declaration of interest kuwa yy sio mwanachama wa chama chochote,yupo neutral kama professional ya uandishi wa habari inavyotaka...sasa muda ni mwalimu mzuri sana imeshajulikana unafiki na uzandiki wake
 
Kawe ameenda tu ali aje kuwasimulia wajukuu wake kwamba naye alishawahi kugombea ubunge. Anajua kabisa hawezi kupata.
 
Back
Top Bottom