Pascal Mayalla: CHADEMA watengeneze kwanza Katiba mpya ya chama chao kabla ya kukimbilia katiba ya nchi, wawatendee haki wabunge 19

Pascal Mayalla: CHADEMA watengeneze kwanza Katiba mpya ya chama chao kabla ya kukimbilia katiba ya nchi, wawatendee haki wabunge 19

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwandishi wa habari nguli nchini na mwanasheria Pascal Mayalla amesema Chadema wanapaswa kurekebisha kwanza katiba ya chama chao kabla ya kukimbilia kudai katiba mpya ya nchi.

Pascal amesema Chadema hawana fedha za kuitisha kikao cha kujadili rufaa za wabunge wake wa viti maalumu sasa fedha za kuendeshea " harakati " za kudai katiba ya nchi watazitoa wapi?

Mayalla amewataka Chadema wamwache Rais Samia atengeze uchumi kwanza kwa sababu katiba mpya haiko katika Ilani ya uchaguzi ya 2020/35.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Je, Paskali ana hoja?

Tuanze kwa kuitazama Katiba ya CHADEMA. Inahitaji marekebisho?
Bila shaka, inahitaji Mabadiliko. Katiba ya CHADEMA haielezi ukomo wa Kiongozi kuwa Mwenyekiti wa Chama. Ndiyo, kuna vipindi vya uongozi lakini kiongozi anatakiwa apewe ukomo wa muda wa kuwa Mwenyekiti. Ahudumu kwa miaka 8 aachie ngazi damu mpya zichukue kijiti.

Katiba yao inamruhusu Mwenyekiti aendelee kugombea mpaka atakapoamua mwenyewe kuacha.

Kwa hiyo ni dhahiri katiba yao inahitaji marekebisho.

Juu ya Swala la Wabunge Covid 19.
Paskali ameamua tu kujitoa ufahamu. Ila katika Chama chochote, kilichofanywa na Wabunge hao 19 siyo cha kufurahisha na wala hakipaswi kunyamaziwa. Siyo CHADEMA wala CCM ambaye angekuwa tayari kunyamaza kwa upuuzi uliofanyika.

CHADEMA kwa sasa wangekazania kufuatwa kwa Katiba iliyopo kuliko kuipigia kelele Katiba mpya. Ni swala ambalo linahitaji muda. Na Mh Rais kasema atalifanyia kazi miaka ijayo.
 
Mwandishi wa habari nguli nchini na mwanasheria Pascal Mayalla amesema Chadema wanapaswa kurekebisha kwanza katiba ya chama chao kabla ya kukimbilia kudai katiba mpya ya nchi...
chadema mwambieni mbowe ukweli kwamba mnasimamia misingi ya demokrasia ilio ya kweli, msimuogope! haya mambo ya anaachia ngazi atakapochoka yashapitwa na wakati nyerere alikua wa mwisho kufanya hivi
 
Mwandishi wa habari nguli nchini na mwanasheria Pascal Mayalla amesema Chadema wanapaswa kurekebisha kwanza katiba ya chama chao kabla ya kukimbilia kudai katiba mpya ya nchi

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Pasco huyu huyu mbele ya wajumbe akaishia kupata kura 1 moja ndio unamuita nguli? Afu waambie mataahira, misukule na MATAGA wenzio kuwa katiba sio takwa la sisiemu, ni hitaji la wananchi.
 
Mwandishi wa habari nguli nchini na mwanasheria Pascal Mayalla amesema Chadema wanapaswa kurekebisha kwanza katiba ya chama chao kabla ya kukimbilia kudai katiba mpya ya nchi...
Yaani nimecheka mpaka nikakaa Chini kwa mtu huyu anavyo hangaika ili kupata teuzi.

Moja Pascal national priority ni kubwa kuliko chama Cha siasa. Na hata ukipewa teuzi Basi jua taifa kwanza chama baadae.

Pili, Pascal Kama ni suala la wabunge hewa kuwa bungeni wa kulaimiwa ni Speaker, Time ya taifa ya uchaguzi na serikali kwa kushupaza shingo na sio Chadema walishatoa hukumu yao kwa mujibu wa katiba yao na kuonyesha upungufu wote. Tume imegopa kuweka hadharani barua ya utezi ya Chadema, Bunge limekataa kuitambua barua ya chadema. Pascal ukitaka chadema wafanye Nini? Ukipewa uteuzi fuata utawala wa sheria na sio shinikizo la chama, taifa kwanza chama baadae.

Tatu, Chadema hawana mgogoro ndani ya chama Chao, Wala hakuna aliyelalamikia katiba yao(wanachama). Cha ajabu wasio wanachama ndio wanalalamika, haya ni maajabu ya kuzimu huku duniani. Ukipewa teuzi fuata job description ya cheo chako Wala sio ya mtu mwingine. Taifa kwanza chama baadae.

Mwisho Kuna msemo "kuchamba kwingi...."

Taifa mbele chama baadae
 
Pasco huyu huyu alieonekana takataka mbele ya wajumbe akaishia kupata kura 1 moja ndio unamuita nguli? Afu waambie mataahira, misukule na MATAGA wenzio kuwa katiba sio takwa la sisiemu, ni hitaji la wananchi.
Amesema katiba ya Chadema ni mbovu, tengenezeni mpya!
 
Back
Top Bottom