MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
PhD candidate wa Mchongo University
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwandishi wa habari nguli nchini na mwanasheria Pascal Mayalla amesema Chadema wanapaswa kurekebisha kwanza katiba ya chama chao kabla ya kukimbilia kudai katiba mpya ya nchi.
Pascal amesema Chadema hawana fedha za kuitisha kikao cha kujadili rufaa za wabunge wake wa viti maalumu sasa fedha za kuendeshea " harakati " za kudai katiba ya nchi watazitoa wapi?
Mayalla amewataka Chadema wamwache Rais Samia atengeze uchumi kwanza kwa sababu katiba mpya haiko katika Ilani ya uchaguzi ya 2020/35.
Nawasalimu kwa jina la JMT!
We byembalilwa wee...!, unataka kuizungumzia katiba ya Chadema...Kabla ya kuanza kudai katiba mpya , tunajukumu la kuanza kudai katiba ya chama chetu, hakika hii ya sasa imepitwa na wakati ina mfumo usiotoa uhuru kwa wanachama ,
Kiti cha mwenyekiti imekuwa nafasi ya kudumu , mfumo wa kupata uongozi wa matawi nao umejaa ukiritimba
Katiba mpya ya Chadema ni sasa.
Nimekuelewa ila Pascal Mayala sijamwelewa hata kidogo kile kitendo kilichofanyika kwa Wabunge 19 wa viti maalum si cha kiungwana tusisubiri mpaka watu wafe ndiyo tuanze kuwananga kuwa walikosea,na kama ni uanasheria basi ni uanasheria wa kufaulu mitihani na si uanasheria wa kuzingatia sheria.Je, Paskali ana hoja?
Tuanze kwa kuitazama Katiba ya CHADEMA. Inahitaji marekebisho?
Bila shaka, inahitaji Mabadiliko. Katiba ya CHADEMA haielezi ukomo wa Kiongozi kuwa Mwenyekiti wa Chama. Ndiyo, kuna vipindi vya uongozi lakini kiongozi anatakiwa apewe ukomo wa muda wa kuwa Mwenyekiti. Ahudumu kwa miaka 8 aachie ngazi damu mpya zichukue kijiti.
Katiba yao inamruhusu Mwenyekiti aendelee kugombea mpaka atakapoamua mwenyewe kuacha.
Kwa hiyo ni dhahiri katiba yao inahitaji marekebisho.
Juu ya Swala la Wabunge Covid 19.
Paskali ameamua tu kujitoa ufahamu. Ila katika Chama chochote, kilichofanywa na Wabunge hao 19 siyo cha kufurahisha na wala hakipaswi kunyamaziwa. Siyo CHADEMA wala CCM ambaye angekuwa tayari kunyamaza kwa upuuzi uliofanyika.
CHADEMA kwa sasa wangekazania kufuatwa kwa Katiba iliyopo kuliko kuipigia kelele Katiba mpya. Ni swala ambalo linahitaji muda. Na Mh Rais kasema atalifanyia kazi miaka ijayo.
Katiba lulu wenye wasimamizi feki wasiozingatia sheria na utu wa Mtanzania,useless kabisa.Pasco ametema MADINI YA ALMASI mno.
Chadema ni "The Comedy"..
Katiba yao INAWASHINDA....leo waiweze ya NCHI?
Hivi hawa akina "Jangala" wanashindwaje kuwaiga wenzao CCM wenye katiba LULU?!!!
#KaziIendelee
Rais kumaliza wiki mbili Marekani kujenga uchumi au kubomoa uchumi?....UCHUMI KWANZAAAA!!!
#KaziIendelee
chadema mwambieni mbowe ukweli kwamba mnasimamia misingi ya demokrasia ilio ya kweli, msimuogope! haya mambo ya anaachia ngazi atakapochoka yashapitwa na wakati nyerere alikua wa mwisho kufanya hivi
aya mambo ya ukabila yashapitwa na wakati, apatikane mwingine wa uchagani sio mwenyekiti miaka100Mpaka pale atapopatikana Mwenyekiti wa CHADEMA kutoka kanda ya ziwa hasa hasa Msukuma hapo ndipo mtakatambua kuwa CHADEMA ni chama cha watanzania lakini leo ni cha kihuni kwa vili mwenyekiti si Msukuma.
Ukabila unawasumbua sana ninyi timu Magufuri lakini itafika muda mtaelewa tu kuwa mnachokifanya sasa siyo sahihi.aya mambo ya ukabila yashapitwa na wakati, apatikane mwingine wa uchagani sio mwenyekiti miaka100
Uzalendo wao ni wa kimaslahi zaidi paliponona wanapapenda hata kama pameoza.
johnthebaptist na Pascal Mayalla kwani CHADEMA wanataka katiba ya chama? Vyama vitapita na vingine vitazaliwa lakini Taifa la Taifa litazidi kudumu. Hatuhitaji kuboresha katiba za vyama au koo.
Mwandishi wa habari nguli nchini na mwanasheria Pascal Mayalla amesema Chadema wanapaswa kurekebisha kwanza katiba ya chama chao kabla ya kukimbilia kudai katiba mpya ya nchi.
Pascal amesema Chadema hawana fedha za kuitisha kikao cha kujadili rufaa za wabunge wake wa viti maalumu sasa fedha za kuendeshea " harakati " za kudai katiba ya nchi watazitoa wapi?
Mayalla amewataka Chadema wamwache Rais Samia atengeze uchumi kwanza kwa sababu katiba mpya haiko katika Ilani ya uchaguzi ya 2020/35.
Nawasalimu kwa jina la JMT!
Suala la katiba mpya sio suala la vyama vya siasa bali suala linalohusu wananchi wote...hana hoja kwasababu sio Chadema peke yao wanaodai katiba mpya.
Naunga Mkono.Mnafiki kweli, haki ipi?
Kutoa maoni ni bila malipo, aendelee tu kutoa maoni yake hata kama anachosema hakina tijaMwandishi wa habari nguli nchini na mwanasheria Pascal Mayalla amesema Chadema wanapaswa kurekebisha kwanza katiba ya chama chao kabla ya kukimbilia kudai katiba mpya ya nchi.
Pascal amesema Chadema hawana fedha za kuitisha kikao cha kujadili rufaa za wabunge wake wa viti maalumu sasa fedha za kuendeshea " harakati " za kudai katiba ya nchi watazitoa wapi?
Mayalla amewataka Chadema wamwache Rais Samia atengeze uchumi kwanza kwa sababu katiba mpya haiko katika Ilani ya uchaguzi ya 2020/35.
Nawasalimu kwa jina la JMT!
Vitumaalumu hawa hapaJamaa huyu P M ana njaa balaa siku hizi.