Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Hapo ni April 2018. Kwangu nililiona hili kama ni personal vendetta dhidi ya uhuru wa habari na dhidi ya mwandishi mbobezi Bwana Pascal Mayalla japo mpaka leo hajawahi kutujuza ni nini kulikuwa matokeo ya kikao hicho. Tunajuwa kimoja tu kuwa walikukatia biashara zako za PPR kwenye sekta mbali mbali za umma.
Kwangu Mimi niliona yafuatayo;
1. Hukupoa kumkosoa Job Ndugai hata baada ya kikao hicho.
2. Ulitabiri kuwa Job Ndugai asingekuwa Spika 2020-25, na imetokea
3. Wewe ni MSHINDI wa vita aliyoanzisha Ndugai akitumia nafasi yake kama Spika wa Bunge dhidi yako raia usiye na madaraka wala silaha zaidi ya ubongo wako na kalamu.
Mapendekezo;
1. Kusanya nyuzi zako zote, hariri ziwe kitabu. Zitakuja saidia kizazi kijacho kwenye Elimu ya utawala Bora, Udikteta wa Bunge na madhira ya uandishi wa habari
Nawasilisha