Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Umesema kwanini Pascal Mayalla hakumuita na kumuonya,inamaana nawewe unakiri kwamba alikosea? Tz wengi tunapenda kusisitiza uhuru wa maoni ila hatupendi kusikiliza mawazo ya wengine wanayotoa
 
Hahaha Aiseee chalii yangu ndio nimerudi Ghetto sasa hivi. Juzi kati nilimkonyeza mmoja mbibi yeye hakuvaa kininja ni buibui tu akatabasamu na kutingishika kichwa
Kuwa makini mkuu, naskia nyie mnaoishi huko mnaitwa diyasipora na Membe mara atakapoapishwa 2020 eti nyie mtakuwa watu mhimu kwenye uchumi wetu, hakikisha unatunza hizo senti unazopata baada ya kazi ngumu ya box.
 

Wewe unaona alifanya sawa alivyoitukana nchi na rais wetu kipenzi kwa vipande vya shekeli kutoka kwa mabeberu!!?
 
Umesema kwanini Pascal Mayalla hakumuita na kumuonya,inamaana nawewe unakiri kwamba alikosea? Tz wengi tunapenda kusisitiza uhuru wa maoni ila hatupendi kusikiliza mawazo ya wengine wanayotoa

Kwanza kusema tu economist imemtukana Rais tayari ilikuwa virtually kaonywa kama mwandishi alikuwa mtanzania.
Pasco aliandika naamini alifikiri mwandishi ni beberu, nia ya Pasco ilikuwa kupambanisha na beberu kumbe beberu ikatokea kuwa ni Erick. Ha ha ha ha.

Mbona Pasco amekuwa akiwafuatilia Akasha na Barick na makala zao mbona hamusemi kawachongea akasha? Yani uuibe wewe ule wewe wakushike huko lawama apewe mwingine?
 

Inabidi tujiongeze kidogo na lazima tupate muda wa kusumbua akili kuliko kufanya conclusion kwa kile alicholeta mleta uzi kuonekana ni sahihi kwa 100%.

Hivi Pascal ni mfanyakazi wa TRA au ofisi wa ofisi ya mwendesha mashtaka hadi tufikie anatuhumiwa alienda kumchonganisha Kabendera kwa hizo taasisi?
 
Kujaribu kumhusisha Pascal Mayalla na masaibu anayoyapata mwandishi Eric Kabendera ni utovu mkubwa wa uaminifu katika uchambuzi wa habari. Na hii ni sawa na ramli chonganishi!

Alichokifanya Pascal ni kuhabarisha jamii kuhusu makala za jarida la Economist zilizokuwa zinamkosoa Rais Magufuli na, of course, kuongeza maoni yake katika ile style yake ya uandishi kwa kutumia kejeli (sarcasm). Hakukuwa na tatizo hapo.

Tatizo kubwa hapa ni mleta mada kujaribu kutumia tukio la kushtakiwa kwa Kabendera kama silaha ya kumtisha Pascal ili asitoe maoni yake kwa uhuru. Hii haikubaliki hata kidogo. Uhuru wa kutoa maoni ni lazima uheshimiwe.

Nilisoma makala husika za Economist na zikuwa na ukosoaji wa kawaida tu ambao ulipaswa kutolewa majibu (rejoinder) na msemaji wa serikali katika jarida hilo hilo. Hii ingekuwa njia rahisi na ya kisayansi zaidi kwa upande wa serikali kuliko kumsaka na kumshtaki mwandishi wa makala.

Katika miaka ya 70 na 80, gazeti la serikali la Daily News lilikuwa na safu iliyokuwa inaitwa What They Say About Us ambayo ilikuwa makhsusi kwa ajili ya kuchapisha makala na stori kutoka vyombo vya habari vya nje zilizokuwa zinakosoa serikali ili wananchi wazisome.

Ingekuwa wakati huo, Daily News ingechapisha makala zote husika za jarida la Economist.

Hivyo kama serikali inatekeleza sera zake kikamilifu na kwa uaminifu, kamwe haiwezi kuogopa kukosolewa. Na ukosoaji ujibiwe kwa hoja. This is how politics works.
 
Nakubaliana na wewe mkuu.


Au kwanini awakumshauri aandike na MWANDISHI WETU badala ya ERICK KABENDERA
 
Hapa kuna maswali.

1. Kwanini MSAMBAZA UONGO Pascal hajashitakiwa. Yaani nikiandika uongonna wewe ukausambaza basi na wewe unakuwa umetenda kosa.

2. Ni ushahidi upi kwamba mwandishi wa huo UONGO alikiwa ni KABENDERA. Tunaomba kujua hili.

3. Kwanini kabendera hajashitakiwa kwa kosa la kisema aj kuandika UONGO
 
Erick
Kama alikuwa anaandika makala na hao economist wanamlipa pesa, hapo kosa ndo lilipo. Nikosa kufanya kazi nchi nyingine ukiwa nchi nyingine, hilo hata nchi yoyote ya kibeberu wanakutia nguvuni(tax invading)

Pia kama hao economist walitia mwamala wa aina yoyote hapo, lazima wamtie nguvuni, ya kufanya kazi na kukwepa kodi. Hapo huyu mwandishi atakuwa na hali ngumu sana, kama kwa namna yoyote alilipata mwamala kutoka nje.
 

Tax invading!!!? Malkia njoo huku uone lugha yako inanajisiwa!
 
Upo sahihi mimi nilisoma na kuona Mwandishi Mtanzania na yupo Tanzania sikumuelewa pascal nilipita tuu nikajua anawapa watu taarifa kijanja sana...amefanikiwa ila alichokifanya sio kitu kizuri kabisa...
 
Huyo Mayala Pascal yn hadi kawaumiza ndo munalalamika wenye akili tuligundua anacho fanya humu jamii forum mulimushangilia bila kufikiria

Huyo Pascal ni mkabila mara elfu hana nia njema na waandishi wenzake
Hilo kuwa angemuonya limetoka wapi? Acheni ujinga yy nani?
Huyo pascal ni mutafuta fursa na ipo tayari

Yote aliyo kuwa anaandika yalichonganisha waanfishi wenzake na siyo kujenga

Jifunzeni kwa nyakati kwnn kipindi aanze kuandika
Mara eti jamaa kabadilika huyu Mayala kipimo cha kumuita Raisi kabadilika je alijua vipi kama sio munafiki huyu

Naunga mkono huyu jamaa atengewe hadi kabendera atoke nje.musicheke na joka hili linalo itwa Mayala
Ataanza mafumbo kwa mtu mwingine naye Atakamatwa soon
Mwenye kura nyama ya mtu haachi

Eti wasukuma si wakabila je anakipimo gani kujua kabila lipi lina ukabila na lipi halina ukabila, acha kugawa watanzania wewe mayalaNjaa itakuua

Lyamba lya mufipa
 
Pasco huwa anaandika kutokana na utashi wake,sioni kama ana kisa/ukabila/upendeleo kama walio wengi walivyo tafsiri maandiko yake.
Nimekuwa nikisoma maandiko yake mengi kwa kipindi kirefu sasa,namwona ndio style yake ya uandishi.
Humu ndani kila moja aheshimike kwa jinsi anavyo shiriki.
 
Kumbe kumpa like zangu kote kumbe huyu ni ndumila kuwili?? Sishangai makala zake zote akiandika huwa anauma huku na huku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…