Fiziolojia
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 815
- 1,080
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani sheria inasema ushahidi uwe direct, yaani shahidi ameushuhudia kwe sensory organs zake.Mfano kuona au kusikia.sasa wewe hiyo risasi ilivyofatuliwa uliona na ilipokata kona uliona?Based on Kifo cha Akwilina, ainisha kosa la kina Mbowe na usafi wa polisi waliopiga risasi juu ikakata kona ikajikuta imeua abiria kwenye gari then tuje tumalizie na la Mayalla!
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa gani?Inawezekana ni mmoja Wa wale jamaa hua simuelewi pascal
Jamaa gani hao?Inawezekana ni mmoja Wa wale jamaa hua simuelewi pascal
Mimi nafikiri angeshitakiwa kwa makosa mabayo yapo kwenye Media Services Act,2006. Hili kuhujumu uchumi na katatisha rupia! Labda wenye mamlaka wanajua alihujumu vipi1.Sio atengwe aliyekuwa anaandika habari bila kufuata weledi na kuishia kutukana rais.
2. Unaposema hakumuita na kumuonya ina maana ye hakuwa anaingia humu jf na kusoma maandiko ya pasco au alikuwa anapuuza?
3. Kisha ndugu zake na mama yake wanapataje shida wakati alikuwa na backup ya watu wengi wakiwemo kina zitto, waende wakahudumie familia. Au anzisheni kapu la kuchangia familia yake.
4. Unapozichokoza mamlaka na kujiona shujaa jua tu utalipia gharama siku moja, ni suala la muda. Hata tundu lissu kalipia gharama. Na akiendelea atalipia tena. Kifupi dunia ina kanuni zake. Hiyo ni principle ya dunia nzima.
5. Lakini pia watz tumshukuru sana Pasco kwa kufichua habari za huyu kinyamkera ambaye ni ant government. Watu hawa wapo nchi nyingi tu. Lakini nadhani habari yake kwisha. Mtapiga makelele baada ya muda mtasahau na maisha yataendelea. Pengine atapelekewa tu tarifa za kifo cha mama yake kwa kukosa dawa. Kina zitto nao baada ya muda watakuwa bize na mambo yao na kumsahau kabisa.
Acha uongo nenda kamsaidie huyo msaliti mwenzio mahakamani. Eti utatuzuia kuingia Kagera sasa sisi tukitaka hata huko Kagera hutafika. Pia kumbuka ni sisi ngosha ndiyo tuliowasaidia kumtoa nduli IDD Amin alikuwa ameshaanza kuwafanya mbaya mpaka akawaachia ugonjwa wa Slim (UKIMWI). Baada ya kusumbuka na Pascal Mayalla mlitakiwa kuhangaika na huyo msaliti Erick aache usaliti la sivyo atanyooshwa.Niombe wasomaji wangu muelewe kuwa sina nia mbaya ninapojaribu kuja na uchambuzi wa namna hii. Lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale taaluma moja ambayo Taifa linawategemea wanaposigana katika jamii nani anayeumia zaidi!
Nakumbuka siku za hivi karibuni gazeti la the Economist lilikuja na habari ambazo Mkuu Pascal aliziita kuwa ni habari za uongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.
Gazeti hilo liliwahi kuja na habari kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewa"
Gazeti hilo baada ya kuchapishwa Pascal Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habari ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.
Alikwenda mbali zaidi akamnukuu Rais wetu kuwa aliwahi kuwaambia wanahabari kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha na kwa hoja.
Pascal Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye Pascal Mayalla ni moja ya wanahabari ambao waliwahi kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.
HOJA.
Kwanza lazma watu mjue kuwa andiko la Pascal kupinga habari ya the Economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufuatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?
Hapa naomba nieleweke, hata watumishi wa idara nyeti walianza kufatilia gazeti hilo baada ya kusoma bandiko la Pascal Mayalla hapa JF, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habari zile na nyeti kupitia gazeti lile ni ndugu yetu Erick Kabendera.
Kwanini walifuatilia, kiukweli kilichoandikwa na mwandishi huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100% ingawa huyu Ndugu Mayalla alikipinga kwa lengo la kujipendekeza kwa msukuma mwemzake.
Je, Pascal Mayalla alijua tangu awali kuwa Kabendera ndie anayeandika habari nyeti na kuziripoti The Economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?
Kimsingi kifungo cha Kabendera nadhani ni furaha kwa Mayalla kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabisa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.
Je, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?
Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu Kabendera awekwe korokoloni hajawahi jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndio kwanza anatafuta makala zote zilizoandikwa huko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.
Andiko la Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa JF linaudhi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.
Nasisitiza waandishi wa habari mtengeni Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabila na wanaoshindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuhofia uhai wao.
Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Kabendera. Tusipomdai kwa kiswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozuia kiongozi yeyote kuingia mkoa wa Kagera mpaka "omwana weitu mumutaishure."
======
Alikuwa anapokea pesa toka kwa mabwana zake na kuzigawa kwa wasaliti wenzie ili kuitukana serikali na Rais wake. Mbaya zaidi alikuwa anakwepa kulipa kodi kutokana na mapato yake hayo kumbuka kukwepa kulipa kodi ni predicate offence ya Money Laundering, this is according to Anti-Money Laundering Act. Nafikiri ndiyo maana ameshitakiwa na ML mkuu!Mimi nafikiri angeshitakiwa kwa makosa mabayo yapo kwenye Media Services Act,2006. Hili kuhujumu uchumi na katatisha rupia! Labda wenye mamlaka wanajua alihujumu vipi
Pascal Mayalla ufataani anao kweli kweli, kwa hilo siwezi mkatalia au mtetea. Tena ni nyoka haswa mwenye vichwa viwili, kimoja mbele kimoja nyuma, kikikukosa cha mbele cha nyuma kinakungoja.
Binafsi nimeshamueleza mara nyingi sana humuhumu JF kuwa yu fataani.
Nnawashangaa sana kuwa ndiyo kwanza mnayajuwa hayo, nikizipata posts nilizowahi kumwambia kuwa yu fataani nitawawekea humu muone kuwa nililiona hilo zamani sana.
Na fataani mwengine na ndumila kuwili ni anaejiita Mzee Mwanakijiji.
Huyu ni P ?Kwani Paschal Mayala ndiye Kabander aliyemfungulia kesi ya utakatishaji.
Najua Paschal ni mbumbumbu katika sekta nyingi na huwa namkabili humu lakini siyo kama unavyotaka tuamini katika hili.
Cc:
Pascal Mayalla
Aliposema habari za TISS kutesa watu kule kigoto Mwanza na kuomba ifumuliwe mbona hamkulaumu! Alikopi na kupaste habari za gazeti la Economist. Kisha kwa uzalendo akasema hili gazeti lina mtukana mtanzania imekuwa kosa!Mbona sijaona ulichoandika hapo kumtuhumu huyo pascal?
What if walidukua mawasiliano ya Kabendera?
Lakini pia kumbuka kashtakiwa kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Wacha due process of law iamue.
Mkuu Hufi Leo, kwanza sikujitokeza kujibu tuhuma hizi kwa kuzipuuzia tuu kuwa kwa vile huu ni uongo na uzushi, uongo mwingine na uzushi ukiuupuuzia tuu utayeyuka na kupita tuu kama upepo hivyo nilipuuza kwa matumaini ni upepo tuu na utapita. Lakini leo baada ya kifo cha mama yake, nimeona nisiendelee kunyamaza hivyo ndio nimejotokeza leo na kukujibu in points format.
Hatua yangu ya kwanza, ni kutuma Salaam maalum kwa rais Magufuli.
Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake
Wanabodi Tangu kukamatwa kwa Mwandishi wa habari za kiuchunguzi Eric Kabendera, na kukamatwa kule kukahushishwa na makala zake, na kwa vile ni mimi niliyekuwa natafsiri makala za majarida ya nje na kuzileta humu jf, hivyo nikatuhumiwa kuwa ni makala za jf ndio zimemchongea Eric Kabendera...www.jamiiforums.com
Kisha nikawaka hoja zako in points format ili kujibu kila hoja
Nampa pole sana Eric Kabendera kwa mapito anayopitia.
- Hukuna uthibitisho kuwa ni andiko langu lilipelekea jarida hilo lifuatiliwe, hakuna uthibitisho wowote kuwa sasa jarida hilo linafuatiliwa na hakuna uthibitisho wowote kuwa Eric Kabendera ndie mwandishi wa makala mimi nilizokuwa nazileta humu.
- Mimi sina uthibitisho wowote kuwa watu wa Idara nyeti walianza kufuatilia jarida lile baada ya bandiko langu humu jf, lakini kwa vile hata sisi humu jf hatujuani nani ni nani, its good to know that na pia sikuwahi kumjua mwandishi wa makala zile, I'm now learning from you.
- Kwenye makala zangu nilikiwa naweka kila cha kweli na cha uongo, niliukubali ukweli na kuupinga uongo na sio kwa lengo la kujipendekeza kwa Msukuma mwenzangu. Kazi ya mwandishi wa habari ni kusema ukweli na kuandika ukweli, mimi ni mkweli, msema kweli na mwandika ukweli bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani au kumchukiza nani.
- Naendelea kusisitiza sikuwahi kumjua mwandishi ni nani, ila hata ningemjua, as long as anachoandika ni kweli, bado nisinge muita mwandishi yoyote kumuonya kwa kazi yake yoyote bali bado ningeendelea kukosoa au na mimi kuandika makala zangu kwenye magazeti yangu ninayoandikia. Hapa nilipo kuna waandishi wengi critical tunafahamiana na kuheshimiana, andiko lolote linajibiwa kwa andiko na sio kwa kuitana.
- Hii ni personal opinion, kuna watu wenye roho za kishetani ambao wanafurahia binaadamu wenzao wanapopata matatizo, very unfortunately mimi sii miongoni mwa watu wa kundi hili, wanaonijua wananijua na wanaonisoma, wananisoma.
- Kwavile tangu mwanzo sikujua kama ni Eric Kabendera wala sikujua nini kitatokea, pia hili sikulijua.
- Hili sii kweli.
- Ungeliweka hilo andiko
- Waandishi wa habari hawawezi kulifanya hili.
- Nimeunga mkono rai yako.
P
KaribuLakini vipi kuhusu kabendera maana Kuna bandiko himu limewahi kukuhusisha na kumchongea kabendera hujawahi kukanusha kwa ufasaha. # binadamu wote ni ndugu zangu.
Sent using Jamii Forums mobile app