MKANDAHARI
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 5,727
- 6,615
Unahusika kwa namna moja au nyingine juu ya kifo cha mama kabendera. Furahi basiMkuu Hufi Leo, kwanza sikujitokeza kujibu tuhuma hizi kwa kuzipuuzia tuu kuwa kwa vile huu ni uongo na uzushi, uongo mwingine na uzushi ukiuupuuzia tuu utayeyuka na kupita tuu kama upepo hivyo nilipuuza kwa matumaini ni upepo tuu na utapita. Lakini leo baada ya kifo cha mama yake, nimeona nisiendelee kunyamaza hivyo ndio nimejotokeza leo na kukujibu in points format.
Hatua yangu ya kwanza, ni kutuma Salaam maalum kwa rais Magufuli.
Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake
Wanabodi Tangu kukamatwa kwa Mwandishi wa habari za kiuchunguzi Eric Kabendera, na kukamatwa kule kukahushishwa na makala zake, na kwa vile ni mimi niliyekuwa natafsiri makala za majarida ya nje na kuzileta humu jf, hivyo nikatuhumiwa kuwa ni makala za jf ndio zimemchongea Eric Kabendera...www.jamiiforums.com
Kisha nikawaka hoja zako in points format ili kujibu kila hoja
Nampa pole sana Eric Kabendera kwa mapito anayopitia.
- Hukuna uthibitisho kuwa ni andiko langu lilipelekea jarida hilo lifuatiliwe, hakuna uthibitisho wowote kuwa sasa jarida hilo linafuatiliwa na hakuna uthibitisho wowote kuwa Eric Kabendera ndie mwandishi wa makala mimi nilizokuwa nazileta humu.
- Mimi sina uthibitisho wowote kuwa watu wa Idara nyeti walianza kufuatilia jarida lile baada ya bandiko langu humu jf, lakini kwa vile hata sisi humu jf hatujuani nani ni nani, its good to know that na pia sikuwahi kumjua mwandishi wa makala zile, I'm now learning from you.
- Kwenye makala zangu nilikiwa naweka kila cha kweli na cha uongo, niliukubali ukweli na kuupinga uongo na sio kwa lengo la kujipendekeza kwa Msukuma mwenzangu. Kazi ya mwandishi wa habari ni kusema ukweli na kuandika ukweli, mimi ni mkweli, msema kweli na mwandika ukweli bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani au kumchukiza nani.
- Naendelea kusisitiza sikuwahi kumjua mwandishi ni nani, ila hata ningemjua, as long as anachoandika ni kweli, bado nisinge muita mwandishi yoyote kumuonya kwa kazi yake yoyote bali bado ningeendelea kukosoa au na mimi kuandika makala zangu kwenye magazeti yangu ninayoandikia. Hapa nilipo kuna waandishi wengi critical tunafahamiana na kuheshimiana, andiko lolote linajibiwa kwa andiko na sio kwa kuitana.
- Hii ni personal opinion, kuna watu wenye roho za kishetani ambao wanafurahia binaadamu wenzao wanapopata matatizo, very unfortunately mimi sii miongoni mwa watu wa kundi hili, wanaonijua wananijua na wanaonisoma, wananisoma.
- Kwavile tangu mwanzo sikujua kama ni Eric Kabendera wala sikujua nini kitatokea, pia hili sikulijua.
- Hili sii kweli.
- Ungeliweka hilo andiko
- Waandishi wa habari hawawezi kulifanya hili.
- Nimeunga mkono rai yako.
Pĺ
Sent using Jamii Forums mobile app