Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais

Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais

Hata ingekuwa serkali ni ya Chadema, bado Tume isingeonekana huru kwa sababu mwenyekiti huteuliwa na mgombea au na Rais wa serkali ya Chadema.Aidha time si huru kwa SBB wakurugenzi huteuliwa na Rais ambaye pia ni mgombea,pia ndo Hugo huyo anawapa nyenzo zote za kufanyia kazi.Nadhani hapo ndo penye matatizo.
Hii ni baada ya majibu ya suala alouliza ikulu
 
Paschal, kuna upotoshaji unaendelea kuhusu uhuru wa Tume za Uchaguzi. Uhuru hauko katika kazi zake. Kama ni kazi, taasisi nyingi za serikali ziko huru kiutendaji.

Uhuru unaodaiwa ni kwenye uundwaji wake. Wajumbe kuchaguliwa na Rais (ambaye kimsingi ni mwanachama wa chama cha siasa) sio sawa.

Tume ya Uchaguzi, kwa maoni yangu, ilipaswa kuwa inatokana na uwakilishi wa vyama vya siasa, taasisi za kiraia, taasisi za kitaaluma, makundi ya kijamii. Na kiongozi au mwenyekiti ndio angechaguliwa na wajumbe miongoni mwao!

Kwa sasa kuna wasiwasi mkubwa juu ya namna taratibu za uchaguzi zinavotengenezwa. Huenda ni za chama kilicho madarakani zikitaka kujihakikishia kuendelea kuwa madarakani. Huenda ni za serikali iliyo madarakani zikizuia serikali nyingine kutoshika madaraka.

Hakuna imani na uhuru wa tume kwa sababu ya matendo ya tume zenyewe!! Kufutwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar 2015 ni mfano mmoja.
 
Vijana
Muziki unaimbwa kwa kufuata noti ili sauti ziwe harmonized na muziki

Kama hujui kusoma noti hutaimba off key lkn mkumbuke noti hizo zinabadilika kulingana na ufunguo uliotumika.
 
Huyo jamaa Pascal Mayalla ni MNAFIKI MKUBWA anajikomba kwa dikteta hadi anatia KINYAA. Credibility na reputation yake kama mwandishi wa habari imekuwa ZERO. Hana tofauti kabisa na ZERO BRAIN.

2434814_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg

Mwandishi mkongwe na mwanasheria nguli Pascal Mayalla amesema NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama zilivyo Mahakama na Bunge.

Pascal amesisitiza kuwa Rais wa JMT ndio msingi wa taasisi zote hizo hivyo zote zipo huru kwa namna zilivyoundwa na katiba.

Pia Pascal amempongeza Rais Magufuli kwa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani na amemtaka mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe zamu yake ikifika aende bila kuweka masharti yoyote.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Huyo jamaa Pascal Mayalla ni anajikomba kwa dikteta hadi Credibility na reputation yake kama mwandishi wa habari imekuwa ZERO. Hana tofauti kabisa na ZERO BRAIN.

2434814_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg
Mkuu Bubu Ataka Kusema, BAK, kwanza asante kuchangia uzi wangu, pili asante sana kwa mchango wako. Ubarikiwe sana.
Uwe na siku njema.
P
 
Mi nakataa mahakama na NEC siyo taasisi huru kwa sababu kuna mkono wa Rais kwenye teuzi. Fullstop
Napigilia msumari hivii!!!

NEC ni tume halali isiyo huru.
Maana ya huru sio kwa sababu katiba inatambua bali kuwa huru ni kutoingiliwa kimaamuzi. Kama hata bashiri anaweza kuweka influence itaendelea Kuwa halali lakini sio huru.

Nimeona Paskali kalaiki komenti zote, haya nyanyasa! [emoji849]
 
ibara 74(7) ya Katiba ya JMT ina inasema tume itakuwa huru na itafanya kazi kwa kufuata sheria.
Kwanza Ili tume iwe huru ni lzima iweze kushitakiwa kwa makosa yake ya kiutendaji katika chaguzi.
Pili matokeo yote wanayo yatowa yalalamikiwe mahakamani bila ya kuacha ya Raisi.
Tatu ,M/kiti wa tume na watendaji wakuu wateuliwe na chama kikuu cha upinzani Bungeni.Wateuliwa hao iwe ni kwa mujibu wa uwezo wao baaa ya kutangaaza nafasi za kazi na kudahiliwa kuwa na sifa zinazofaa kikazi.
Jee Tume hii imetimiza angalau moja ya Mashariti haya hapo juu?
Mimi nnaona Inaongozwa na makada wa CCM kama akina JECHA wa ZNZ
 
Mwandishi mkongwe na mwanasheria nguli Pascal Mayalla amesema NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama zilivyo Mahakama na Bunge.

Pascal amesisitiza kuwa Rais wa JMT ndio msingi wa taasisi zote hizo hivyo zote zipo huru kwa namna zilivyoundwa na katiba.

Pia Pascal amempongeza Rais Magufuli kwa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani na amemtaka mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe zamu yake ikifika aende bila kuweka masharti yoyote.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Hivi kukutana na viongozi wa vyama pinzani ni jambo la kikatiba?
Masuala ya NEC na BUNGE na Mahakanma kuwa huru ni kosa la KATIBA si la Raisi wala CCM kama chama, hili ndilo la kulivalia njuga kuliko kushiriki kwenye chaguzi hizi za uwongo
Na Mkumbuke Hayati Mtikila
aliushauri upinzani upiganie katiba kwanza kabla ya kushiriki kwenye siasa ya Vyama vingi, lakini akapuuzwa hadi Mauti yamemchukua.
 
Mkuu Bubu Ataka Kusema, BAK, kwanza asante kuchangia uzi wangu, pili asante sana kwa mchango wako. Ubarikiwe sana.
Uwe na siku njema.
P

Mkuu, sijui kama nami utanishukuru pia lakini BAK amekuletea makala ikionesha Rais Mkapa akipendekezwa kuundwa kwa tume huru. Umeishia kushukuru kwa kuchangia!

Ukiwa mwandishi au hata mwadilifu tu - unapaswa kueleza jambo hili. Wewe na Rais Mkapa mmetofautiana, labda umueleze BAK Rais Mkapa hayuko sahihi wapi.

Nitasema tena, uhuru wa Tume uko katika muundo wake!! Muundo ndio huleta utendaji kazi. Kama wajumbe wa tume zinazoitwa huru wanakuwa wagombea wa nafasi mpaka ya Urais, ni kipi kitaonesha kuwa utendaji ulikuwa huru (unbiased, uncompromised na untainted)???

Haki si tu inatakiwa itendeke, bali ionekane kutendeka. Je tunayoyaona yanadhihirisha uhuru katika utendaji??
 
Nchi imekosa maendeleo kwa sababu inakosa baraka za mungu kwa kuongozwa na wabunge ambao siyo chaguo la wapiga kura bali ni chaguo haramu za wakurugenziccm, mfano kule jimbo la Ukonga hakuna maendeleo kwa sababu waitara siyo chaguo lao bali ni chaguo la mkurugenziccm.
 
Mwandishi mkongwe na mwanasheria nguli Pascal Mayalla amesema NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama zilivyo Mahakama na Bunge.

Pascal amesisitiza kuwa Rais wa JMT ndio msingi wa taasisi zote hizo hivyo zote zipo huru kwa namna zilivyoundwa na katiba.

Pia Pascal amempongeza Rais Magufuli kwa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani na amemtaka mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe zamu yake ikifika aende bila kuweka masharti yoyote.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu Yohane Mbatizaji, natumaini kwa sasa umeisha anza kukubaliana na mimi, kwa jinsi NEC inavyoshughulikia uchaguzi huu, inathibitisha bila kuwa shaka, NEC sio tuu ni Tume Huru, bali ni Tume Huru yenye Utu, ambayo licha ya mapungufu kadhaa, bado fomu za wagombea wote wa urais zimepokelewa na karibu wote wamepitishwa!.
P
 
Mkuu Yohane Mbatizaji, natumaini kwa sasa umeisha anza kukubaliana na mimi, kwa jinsi NEC inavyoshughulikia uchaguzi huu, inathibitisha bila kuwa NEC sio tuu ni Tume Huru, bali ni Tume Huru yenye Utu, ambayo licha ya mapungufu kadhaa, bado fomu za wagombea wote wa urais zimepokelewa na karibu wote wamepitishwa!.
P
Hakika mkuu!
 
Too far from huru
Pia si kosa la tume na tume hii kama ina maadili inaweza fan ya inayomudu tu.
 
Back
Top Bottom