Tatizo sio max, tatizo ni kujibizana na wajinga.. Kuna ID humu kazi zao mama ni kujaribu ku kutafta tu. Na nimesha acha kabisa kuzi entertainNilishtuka tu haupo active mara nikaona wameunganisha accounts kulikoni bwashee ulimkosea nini Max
Exactly.Huwa pasko kuna wakati simuelewi leo yupo hivi kesho hivi, leo amenyoka kesho chawa
Itabidi uwe tolerant mkuu si unajua humu tunakutana vichwa tofauti kwa wakati tofauti tofauti ,sasa imagine unajibizana na mtu anatype huku anakunywa black label 😂Tatizo sio max, tatizo ni kujibizana na wajinga.. Kuna ID humu kazi zao mama ni kujaribu ku kutafta tu. Na nimesha acha kabisa kuzi entertain
Kweli kabisa mkuu..Itabidi uwe tolerant mkuu si unajua humu tunakutana vichwa tofauti kwa wakati tofauti tofauti ,sasa imagine unajibizana na mtu anatype huku anakunywa black label 😂
Kweli kabisa mkuu ,karibu tena tusukume gurudumu la Max✊️Kweli kabisa mkuu..
Ila kama ujuavyo, mtu mwenye chuki na negative energy sio wa kukaribishwa kabisa kwenye space yako
Kwenye hatua ilipofikia nchi hii, kinachotakiwa kufanyika ni mtu asimame ahesabiwe kasimamia wapi, kwa uwazi. Kwa logical consistency.Mkuu Excel VBA, andiko lako limegusa hisia za wana-jukwaa wengi sana ambao kila uchao wanajikuta katika mshangao huo huo wa kumuona Pascal Mayalla leo akiwa amenyooka na kesho akiononekana kama "chawa." Naomba niweke wazi mapema; lengo langu hapa si kumtetea au kumsafisha Pascal, la hasha! Lengo langu ni kupasua katikati na kuchambua aina hii ya uandishi wa kimkakati anayotumia, ambayo kwa lugha ya kitaalamu tunaita "Strategic Ambiguity" (Utatanishi wa Kimkakati).
Kwanini anafanya hivi? Kuna sababu kuu tatu za kiufundi:
Mosi, Pascal wa sasa anatumia uandishi wa aina hii kama Njia ya Kujihami Kisheria na Kiusalama (Survival Mechanism). Akijua fika kuwa mazingira ya sasa si rafiki na yana rungu la "kupotezana" au kufungiwa leseni (kama dhoruba ya Bodi ya Ithibati - JAB ya hivi karibuni inavyothibitisha), analazimika kuandika andiko linalotoa ishara mbili tofauti kwa wakati mmoja. Upande mmoja unaridhisha mfumo ili kulinda ugali na usalama wake (ndio maana unaona sura ya chawa), lakini ukiisoma hiyo hiyo "literature" yake kwa jicho la tatu, unakuta amepachika madongo mazito ya kiutafiti yanayoukosoa mfumo (upande uliowanyooka).
Pili, ni mbinu ya Kutega na Kupima Upepo (Probing the Waters). Pascal Mayalla ni mwanahabari mkongwe na mwanasheria anayejua saikolojia ya watawala. Anapotupa uzi uliokaa nusu-chawa na nusu-mwanaharakati, anakuwa anapima mipaka ya ustahimilivu wa mamlaka kwa wakati huo. Hii inamfanya aweze kurudi nyuma kisheria na kusema "Mbona mimi niliwasifu hapa?" pindi dola ikitaka kumshukia, huku akiwa ameshatupa ujumbe wake wa siri kwa jamii.
Tatu, na huu ndio ugonjwa mkubwa wa mbinu hii; inapoteza uaminifu (Credibility Dilemma). Ndio maana nimesema sipo hapa kumtetea, kwa sababu aina hii ya uandishi wa kigeugeu ("leo hivi, kesho vile") inamshusha thamani. Sisi kama walaaji wa maudhui ya Masai Studio hatukuzoea uandishi wa kuteleza kama sabuni. Ndio maana ninamsisitiza, kama amefikia hatua ambayo hawezi tena kusimama upande mmoja wa ukweli bila kupepesa macho kwa hofu ya familia na usalama, basi ni bora aweke kando kalamu ya habari. Arudi mahakamani akajitegemee kama Wakili Msomi ili kulinda ile heshima yake kubwa iliyobaki, kuliko kutuacha sisi wasomaji wake njia panda kila siku tukijiuliza leo Pascal amekula nini.
Nini mtazamo wako kwenye hii mbinu yake ya "Strategic Ambiguity", mkuu Excel VBA?
Hakika, shukranKweli kabisa mkuu ,karibu tena tusukume gurudumu la Max✊️
Big thumb P Pascal Mayalla wakati niko mdogo ulikuwa unanispire sana mkuu enzi za PPR kama sikoseiNaona mtagiwa anamwaga tu likes ndiyo kusema kakosa jibu?
Nadhani atakuwa anaandaa a voice from within
Big thumb P
View attachment 3701013
Wakuu, kalamu yangu leo inamwangazia mmoja wa nguzo imara za jukwaa hili na tasnia ya habari nchini, Wakili Msomi na Mwanahabari Nguli, Pascal Mayalla. Nikiwa kama shabiki wake mkubwa na mdau niliyeandika hadi makala za kiutafiti hapa jukwaani kuelezea jinsi alivyowahi kunyanyaswa na mifumo ya mamlaka kupitia "soft censorship," leo ninalazimika kuweka mezani uchambuzi wa nafsi mbili tofauti za mtu huyu mmoja.
Lengo langu si kumshusha thamani, la hasha! Nia yangu ni kutunza na kulinda heshima ya jina kubwa alilolijenga kwa jasho na damu kabla halijamomonyolewa na watu wasiomfahamu vizuri hapa jukwaani.
Pasco wa Masai Studio: Nguli wa Broadcaster na "Mpishi" vya Kitimoto
Tukirudi nyuma kidogo, jina la Pascal Mayalla lilibeba uzito wa kipekee kupitia Masai Studio, ambapo akishirikiana na wamiliki wenza wa studio hiyo kama Allyoki, walitengeneza historia ya kipekee ya habari nchini. Huyu alikuwa mwanahabari huru, mtayarishaji wa maudhui, na mtangazaji wa kwanza kabisa wa Talk Show ya kwanza ya runinga nchini—kipindi cha "Mada Moto" pale DTV mwaka 1995. Enzi hizo akiwa kijana mbichi asiye na majukumu ya kifamilia, akilipwa mishahara minono ya "six figures" kwa ushupavu wake!
Sisi kama hadhira tulimkubali bila masharti kwa sababu alisimama kama sauti ya kweli ya Muhula wa Nne wa Dola (The 4th Estate). Kilele cha uandishi na utangazaji wake kilionekana kupitia kipindi cha kihistoria cha Kitimoto kilichoruka DTV na Channel 10. Kipindi kile kilikuwa moto haswa, kiasi kwamba hata msemo wa mtaani wa kuitia nyama ya nguruwe jina la "kitimoto" ulizaliwa pale, kutokana na jinsi wanasiasa na mawaziri (kama akina Daniel Yona wa Wizara ya Fedha na Askofu Kakobe) walivyokuwa wanatolewa jasho jukwaani!
Kwenye kiti kile, Pascal alikuwa anawapika na kuwapakua wanasiasa bila uoga, akiongozwa na maswali ya mitego na utafiti mkubwa wa Masai Studio
Mabadiliko: Imekuwaje Mayalla wa Sasa Anatofautiana na Yule wa Masai Studio?
Ukiangalia mwenendo wa sasa wa mzee wetu Pascal ndani ya JamiiForums na kwenye medani za uchambuzi, kuna utofauti mkubwa unaoacha maswali mengi. Yule mwanahabari aliyekuwa anashambulia kwa mbele, leo anaonekana kuwa mtu wa kujihami, kupiga siasa za kimkakati, na wakati mwingine kuandika kwa tahadhari kubwa inayozua hisia za "kusaka teuzi" au kuegemea upande fulani, jambo linalowapa fursa baadhi ya wana-jukwaa wasiomjua vizuri kumshushia heshima yake.
Ninajua vizuri—na sote tunajua—kwamba nyakati tunazoishi sasa kimuktadha si rafiki hata kidogo. Tuko katika mazingira ya kiserikali ambayo mara nyingi yameonyesha sura ya ukatili (ruthless) na isiyothamini utu wala uhuru wa mawazo.
Dhoruba hizi si geni kwake; hata huko nyuma amewahi kukumbana na misukosuko ya kunyang'anywa leseni na kufukuzwa ofisini kisa tu kuuliza swali gumu mbele ya wakuu wa nchi. Hata hivyo, kama mwanahabari anayewakilisha muhula wa nne, Pascal anapaswa kukumbuka kuwa dhoruba hizi ni sehemu tu ya wajibu wa mwanajeshi. Unapoingia vitani, unajua kabisa utakutana na milio ya risasi na dhoruba kali, lakini uaminifu wako unabaki kwenye kupigania ukweli mstari wa mbele.
View attachment 3701014
Ushahidi wa dhoruba hizi ni huu wa hivi karibuni wa Machi 2026, ambapo Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) ilimshushia rungu la onyo yeye na Wilberforce Ngoto kule Jambo TV. Kisa kikajulikana? Kisa ni uchambuzi wake wa kiutu na kisiasa juu ya hisia za viongozi na "makofi ya msibani". Mfumo ulimtaka athibitishe hisia za moyoni za kiongozi ndani ya saa 24! Hapa ndipo tunapoona jinsi Pascal wa sasa anavyolazimika "kukiri makosa" na kupiga magoti kidiplomasia kulinda ugali na usalama wa chombo cha habari, jambo ambalo lisingewezekana kwa yule Pasco wa Masai Studio.
Vita Kuu ya Tatu ya Dunia ya Nafsi Mbili
Nikifanya hitimisho la kiweledi, nina amani ya moto kusema kuwa: Ikitokea siku moja Pascal Mayalla wa Masai Studio akakutana uso kwa uso na huyu Pascal wa sasa mwenye kofia mbili (Uanasheria na Uandishi wa Habari), lazima kitazuka vita vikali sana vya kisaikolojia na kifalsafa. Yule wa Masai Studio atamshangaa huyu wa sasa kwa namna anavyozingatia sana kujilinda na mistari ya kijani na "uchawa wa kimamlaka" unaolazimishwa na mifumo, na huyu wa sasa atamcheka yule wa zamani kwa ukosefu wa mbinu za "kisayansi" za kijeshi na kisheria za kujilinda dhidi ya dhoruba za dola.
Mzee wangu Pascal, andiko hili linatokana na mapenzi mazito kwako. Kwa jinsi unavyoshambuliwa sasa na vijana wa kizazi kipya hapa jukwaani wasiojua kabisa historia na mchango wako, ninaamini kabisa ingekuwa heri ungalifanya kazi ya Uanasheria pekee mahakamani tujue kimoja, kuliko kuendelea kuona thamani ya nguli wa habari ikishushwa na kudhihakiwa hapa jukwaani na watu wasiojua ulipotoka.
Nawasilisha, wakuu. Mzee Pascal Mayalla, karibu uwanjani utupe neno lako.
Nadhani jibu ni moja tu "He knows what he is doing"Mara nyingi mtu anakuwa ni yule yule tu ila mazingira ndiyo yanabadilika na kumuonesha katika sura tofauti. Anavyo react tofauti katika mazingira tofauti.
Ila ile core character ya mtu, sisemi kuwa haibadiliki, ila kubadilika ni vigumu sana.
Ni rahisi zaidi kuona mtu kabadilika kwa kuwa wewe ulikuwa hujamuelewa vizuri kuliko kuona mtu kabadilika kwa sababu kabadilika kweli.
Ndiyo maana watoto wa mjini wanasema "Shika hela tujue tabia yako". Kwa sababu wanaamini kuna tabia nyingine utazificha kwa kuwa huna hela tu, ukipata hela ndiyo zinajulikana.
Yani inawezekana ulionekana mpole kwa sababu hukuwa na nguvu ya hela tu, ulivyopata hela kila mtu akajua kuwa kumbe ule upole wote ilikuwa kwa sababu huna hela tu, umepata hela wameona upande mwingine, kumbe wewe si mpole hivyo.
Kwa hiyo kuna tabia nyingine zinakuwa zimekaa tu latent, kama mbegu iliyokaa udongoni inasubiri mvua kuchipua. Ikipata mazingira mazuri ya mvua, inachipua.
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na tabia zake kazificha mpaka apate mazingira ya kuzidhihirisha, akipata mazingira yake ya kuzidhihirisha, anazidhihirisha.
Halafu nyie wa nje mkimuangalia, mnaona kabadilika. Kumbe yupo hivyo siku zote, alikuwa kaficha makucha tu.
Kumbe hajabadilika, mlikuwa hamjamfahamu vizuri tu.
Sema uandishi umenyooka kama P mwenyewe vile 😂.View attachment 3701013
Wakuu, kalamu yangu leo inamwangazia mmoja wa nguzo imara za jukwaa hili na tasnia ya habari nchini, Wakili Msomi na Mwanahabari Nguli, Pascal Mayalla. Nikiwa kama shabiki wake mkubwa na mdau niliyeandika hadi makala za kiutafiti hapa jukwaani kuelezea jinsi alivyowahi kunyanyaswa na mifumo ya mamlaka kupitia "soft censorship," leo ninalazimika kuweka mezani uchambuzi wa nafsi mbili tofauti za mtu huyu mmoja.
Lengo langu si kumshusha thamani, la hasha! Nia yangu ni kutunza na kulinda heshima ya jina kubwa alilolijenga kwa jasho na damu kabla halijamomonyolewa na watu wasiomfahamu vizuri hapa jukwaani.
Pasco wa Masai Studio: Nguli wa Broadcaster na "Mpishi" vya Kitimoto
Tukirudi nyuma kidogo, jina la Pascal Mayalla lilibeba uzito wa kipekee kupitia Masai Studio, ambapo akishirikiana na wamiliki wenza wa studio hiyo kama Allyoki, walitengeneza historia ya kipekee ya habari nchini. Huyu alikuwa mwanahabari huru, mtayarishaji wa maudhui, na mtangazaji wa kwanza kabisa wa Talk Show ya kwanza ya runinga nchini—kipindi cha "Mada Moto" pale DTV mwaka 1995. Enzi hizo akiwa kijana mbichi asiye na majukumu ya kifamilia, akilipwa mishahara minono ya "six figures" kwa ushupavu wake!
Sisi kama hadhira tulimkubali bila masharti kwa sababu alisimama kama sauti ya kweli ya Muhula wa Nne wa Dola (The 4th Estate). Kilele cha uandishi na utangazaji wake kilionekana kupitia kipindi cha kihistoria cha Kitimoto kilichoruka DTV na Channel 10. Kipindi kile kilikuwa moto haswa, kiasi kwamba hata msemo wa mtaani wa kuitia nyama ya nguruwe jina la "kitimoto" ulizaliwa pale, kutokana na jinsi wanasiasa na mawaziri (kama akina Daniel Yona wa Wizara ya Fedha na Askofu Kakobe) walivyokuwa wanatolewa jasho jukwaani!
Kwenye kiti kile, Pascal alikuwa anawapika na kuwapakua wanasiasa bila uoga, akiongozwa na maswali ya mitego na utafiti mkubwa wa Masai Studio
Mabadiliko: Imekuwaje Mayalla wa Sasa Anatofautiana na Yule wa Masai Studio?
Ukiangalia mwenendo wa sasa wa mzee wetu Pascal ndani ya JamiiForums na kwenye medani za uchambuzi, kuna utofauti mkubwa unaoacha maswali mengi. Yule mwanahabari aliyekuwa anashambulia kwa mbele, leo anaonekana kuwa mtu wa kujihami, kupiga siasa za kimkakati, na wakati mwingine kuandika kwa tahadhari kubwa inayozua hisia za "kusaka teuzi" au kuegemea upande fulani, jambo linalowapa fursa baadhi ya wana-jukwaa wasiomjua vizuri kumshushia heshima yake.
Ninajua vizuri—na sote tunajua—kwamba nyakati tunazoishi sasa kimuktadha si rafiki hata kidogo. Tuko katika mazingira ya kiserikali ambayo mara nyingi yameonyesha sura ya ukatili (ruthless) na isiyothamini utu wala uhuru wa mawazo.
Dhoruba hizi si geni kwake; hata huko nyuma amewahi kukumbana na misukosuko ya kunyang'anywa leseni na kufukuzwa ofisini kisa tu kuuliza swali gumu mbele ya wakuu wa nchi. Hata hivyo, kama mwanahabari anayewakilisha muhula wa nne, Pascal anapaswa kukumbuka kuwa dhoruba hizi ni sehemu tu ya wajibu wa mwanajeshi. Unapoingia vitani, unajua kabisa utakutana na milio ya risasi na dhoruba kali, lakini uaminifu wako unabaki kwenye kupigania ukweli mstari wa mbele.
View attachment 3701014
Ushahidi wa dhoruba hizi ni huu wa hivi karibuni wa Machi 2026, ambapo Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) ilimshushia rungu la onyo yeye na Wilberforce Ngoto kule Jambo TV. Kisa kikajulikana? Kisa ni uchambuzi wake wa kiutu na kisiasa juu ya hisia za viongozi na "makofi ya msibani". Mfumo ulimtaka athibitishe hisia za moyoni za kiongozi ndani ya saa 24! Hapa ndipo tunapoona jinsi Pascal wa sasa anavyolazimika "kukiri makosa" na kupiga magoti kidiplomasia kulinda ugali na usalama wa chombo cha habari, jambo ambalo lisingewezekana kwa yule Pasco wa Masai Studio.
Vita Kuu ya Tatu ya Dunia ya Nafsi Mbili
Nikifanya hitimisho la kiweledi, nina amani ya moto kusema kuwa: Ikitokea siku moja Pascal Mayalla wa Masai Studio akakutana uso kwa uso na huyu Pascal wa sasa mwenye kofia mbili (Uanasheria na Uandishi wa Habari), lazima kitazuka vita vikali sana vya kisaikolojia na kifalsafa. Yule wa Masai Studio atamshangaa huyu wa sasa kwa namna anavyozingatia sana kujilinda na mistari ya kijani na "uchawa wa kimamlaka" unaolazimishwa na mifumo, na huyu wa sasa atamcheka yule wa zamani kwa ukosefu wa mbinu za "kisayansi" za kijeshi na kisheria za kujilinda dhidi ya dhoruba za dola.
Mzee wangu Pascal, andiko hili linatokana na mapenzi mazito kwako. Kwa jinsi unavyoshambuliwa sasa na vijana wa kizazi kipya hapa jukwaani wasiojua kabisa historia na mchango wako, ninaamini kabisa ingekuwa heri ungalifanya kazi ya Uanasheria pekee mahakamani tujue kimoja, kuliko kuendelea kuona thamani ya nguli wa habari ikishushwa na kudhihakiwa hapa jukwaani na watu wasiojua ulipotoka.
Nawasilisha, wakuu. Mzee Pascal Mayalla, karibu uwanjani utupe neno lako.
Nilimuambia wewe ni muandishi wa habari wakili msomi, njoo na facts and figures, njoo na analysis, njoo na vitu vyenye mantiki.Naona mtagiwa anamwaga tu likes ndiyo kusema kakosa jibu?
Nadhani atakuwa anaandaa a voice from within
Big thumb P
Ushauri wa kujenga🙏Nilimuambia wewe ni muandishi wa habari wakili msomi, njoo na facts and figures, njoo na analysis, njoo na vitu vyenye mantiki.
Voices from within hata kichaa anayo yake.
Yani voices from within haiwezi kukosea kwa sababu mtu anajifungua tu kuandika hadithi yoyote anayotaka kuandika yeye. Ni kama mtu ambaye anajiwekea kinga asibanwe kwa swali lolote.
Ukimuuliza habari hii umeipata wapi, anakwambia ni "Voices from Within" tu 😂😂
Halafu muhabari mrefu, una meander all over like the Irrawady in the monsoon season.
How are you going to engage with that?
Does he thought?Nadhani jibu ni moja tu "He knows what he does"
Moja kati ya waandishi na wachambuzi nguli kuwahi kutokea Tanzania.
Kuna mada pia huwa anazizungumzka Ironically kumuelewa inahitaji ujifanye mnafiki kidogo wa ubongo wako
Mkuu Kiranga, my highest regards to you. As always, you have brought a heavyweight philosophical and psychological argument to the table regarding human core character and the role of environment in triggering latent traits. Your analogy of "hand a person money to reveal their true behavior" and the seed waiting for the rain to sprout is a masterful level of analysis.I am going to be brutally honest. I told Pascal some of this openly already.
The problem with Pascal is that he is all over the place. He is not logically consistent.
This often happens with people who mix core principles. For example, a staunch Catholic adherent who matches and mixes his liberal social justice ethics with Catholic principles of toxic positivity level of forgiveness and utopian optimism, could come across as confusing and confused as Pascal. Without even being a sycophant.
I am giving him the benefit of the doubt and discounting any nefarious self serving motives here.
If you take someone like Jenerali Ulimwengu, regardless of whether you agree with him or not, he is logically consistent. One can analyze him and tell you what he stands for.
Pascal is not that logically consistent.
To the extent that serious minds analysing his record since the days of "Kiti Moto" all the way to the Magufuli answer "Muhimili uliochimbiwa chini zaidi" all the way to his sad "Samia's useful idiot" days at JF, one will fail to see a consistent message, or even a desirous growth. In fact this is like retrograde motion.
So this is what leads me to ask, was he all that to begin with?
Or was he mediocre from day one, it is just that we have low standards and did not have a free enough press to have variety and depth and discernment? Plus, maybe we did not know any better ourselves back then?
I mean I used to watch Peter Jennings, but I could never even start to compare Peter Jennings to Pascal.
That we had to go with him because we had just gotten the TV stations (not counting the sleepy TVZ), we needed local content, we needed to cheer for any youthful change that was probing the right questions, we did not even have any insight to who Pascal Mayalla was, what did he really stand for, nor did we care to ask, since he was our very own Walter Cronkite?
One does not simply take such a huge fall from grace unexpectedly like bird shit without a logical explanation. And Pascal does not need to be Samia's "useful idiot". And he is not a sycophant, because sometimes he dishes out fair criticism, unless that is well calculated for effect, which is a doubtful and such a conspiracy theory angle.
So he is contradicging himself to such a deep extent that sometimes I think he genuinely believes in what he says.
Which makes him Samia's useful idiot.
But was he always so, and that it took someone as birdrained as Samia to get us to see that?
Mkuu Gunner11, nakuelewa sana pindi unapozungumzia matumizi ya busara ili kujilinda wewe mwenyewe na wale wanaokutegemea katika mazingira ya sasa. Huo ni uhalisia wa maisha na mbinu ya kujihami.Hakika sometimes unaachana na ukweli, unatumia busara kufikisha hoja zako for the betterment of you na wale wanaokutegemea