Pascal Mayalla wa 'Masai Studio' akikutana na Pascal wa JamiiForums kutatokea Vita Kuu ya Tatu ya Dunia

Pascal Mayalla wa 'Masai Studio' akikutana na Pascal wa JamiiForums kutatokea Vita Kuu ya Tatu ya Dunia

Shukrani kwa kupotosha umma kiongozi. Pascal Mayalla ni Wakili na ameapishwa rasmi. Naomba nikusaidie kufahamu maana ya maneno haya mawili:
  • Mwanasheria: Ni mtu yeyote aliyesoma na kuhitimu Shahada ya Sheria (LL.B). Pascal alihitimu shahada hii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  • Wakili: Ni mwanasheria aliyepitia ngazi ya mafunzo ya vitendo (Law School of Tanzania), akafaulu, na kisha kuapishwa rasmi na Jaji Mkuu wa Tanzania kuwa Afisa wa Mahakama mwenye haki ya kusimama na kutetea wateja mahakamani.
Lini Mayalla alienda Law School? Lini mayala amekuwa Advocate?
 
Lini Mayalla alienda Law School? Lini mayala amekuwa Advocate?
1793299833931.png


nilikuwekea mtego unase sikutaka kuweka huu ushahidi mapema nilijua ungefanya utafiti kabla ya kujibu kwanini nimekujibu vile
 
Boss kusoma LLB kunakufanya uwe mwanasheria tu! And yes i know ni mwanasheria ila sio wakili

Au hujui tofauti ya mwanasheria na wakili?
Kwa Maslahi ya Taifa", mimi mwandishi wenu Pascal Mayalla, ni miongoni mwa mawakili wapya 335 walioapishwa wiki iliyopita na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, hivyo hii ni makala ya shukrani kwa Jaji Mkuu na uongozi wote na wanyakazi wa Mhimili wa mahakama wakiwemo wa kitengo cha mawakili, Asanteni sana
 
Pascal is just a long winded babbling idiot who overrates himself and sometimes overrated by others who don’t know any better.

Bado sijamwona akijibu chochote kwenye uzi huu.

Ila akija kujibu, atakuja na maandishi mengi yasiyo na maana huku akiweka ma links kibao ya mada zake zingine zisizo na kichwa wala miguu.

I’ve never rated him.
 
Hapo kwenye andiko ulini quote mimi au matawi ya juu wewe?
Hapa hatubishani ili kushinda, tatizo lako ulikua unabisha kitu ambacho siyo cha kweli ukakifanya kama cha kweli sasa angalia vizuri hata hapa unachanganya matawi ya juu alijua nilichokua nabisha na wewe akakujibu na mimi nikakazia hapo, ila kwako niliweka screenshot yenye picha ya Mayalla 👇👇
View attachment 3701147

nilikuwekea mtego unase sikutaka kuweka huu ushahidi mapema nilijua ungefanya utafiti kabla ya kujibu kwanini nimekujibu vile
Sikuwa najua ndio maana niliuliza
Siyo kweli kama ulikua unauliza kwasababu ulikuja na hili jibu 👇👇👇👇
Boss kusoma LLB kunakufanya uwe mwanasheria tu! And yes i know ni mwanasheria ila sio wakili

Au hujui tofauti ya mwanasheria na wakili?
Jinsi ulivyojibu hapa ulikua na uhakika kabisa Mayalla siyo wakili pamoja na mimi kukupatia screenshot ya makala yake na pia kukuwekea link ya chapisho lake la jamiiforums
 
Pascal is just a long winded babbling idiot who overrates himself and sometimes overrated by others who don’t know any better.

Bado sijamwona akijibu chochote kwenye uzi huu.

Ila akija kujibu, atakuja na maandishi mengi yasiyo na maana huku akiweka ma links kibao ya mada zake zingine zisizo na kichwa wala miguu.

I’ve never rated him.
Mkuu Nyani Ngabu, umepiga teke la uso bila urembo na kwa kweli inabidi ninyoshe mikono juu; huenda kweli tuligeuzwa mazuzu (fooled) na tukaingizwa chaka zama doomed hizo.
Mwishoni mwa miaka ya 90, kwa sababu ya uhaba wa runinga na kiu ya kuona kijana mzawa anayehoji watawala kwenye Kitimoto, tulichanganya kati ya "kuwepo hewani" (presence) na "kuwa na kina cha uchambuzi" (substance). Tulitengeneza hadithi ya "ushujaa" kumzunguka mtangazaji kwa sababu tu sote tulikuwa hatujui mambo vizuri kipindi kile cha ukiritimba wa habari.
Hata hili rungu la juzi kati wakati anasifiwa na umma alipomuuliza hayati Magufuli kuhusu Katiba Mpya, binafsi sikumuona kama shujaa hata kidogo. Baadhi ya watu walishangilia tu ule ujasiri wa kutaja neno "Katiba Mpya" mbele ya kamera, lakini kiuhalisia lile swali halikujibiwa kabisa bali liliambulia majibu ya kejeli ya "muhimili uliochimbiwa chini zaidi." Mwanahabari makini haishii tu kuuliza swali ili aonekane shujaa, bali anatafuta majawabu ya msingi.
Leo hii, intaneti ikiwa wazi na upeo wa wana-jukwaa ukiwa umekua, ile taswira ya ubonge wake inavunjika vipande vipande na kuonekana kama mchezo wa kubahatisha uliokosa pa kujificha. Ngoja tuone kama atakuja na lile gazeti la ma-links uliyolitabiri au la.
 
nawasiwasi sana huu uzi mleta uzi huwezi fanana kiasi hicho matamshi ya mzee pasco kiasi hicho kwenye uzi harafu useme unamwandika
 
nawasiwasi sana huu uzi mleta uzi huwezi fanana kiasi hicho matamshi ya mzee pasco kiasi hicho kwenye uzi harafu useme unamwandika
Mkuu kina kirefu, naomba unifafanulie vizuri unamaanisha nini hasa unaposema huoni utofauti wa matamshi kati yangu na mzee Pascal Mayalla. Ikiwa unadhani kuwa mimi niliyeanzisha uzi huu ni akaunti mbadala (ID fake) ya mzee Pascal Mayalla anayejiandika mwenyewe hapa, basi ninalazimika kukujibu kuwa unahitaji kutathminiwa upya uwezo wako wa kiutambuzi na kiuchambuzi.
Inaonekana kabisa hujasoma au hukufuatilia mfululizo wa hoja zangu za kupinga (rebuttals) nilizowahi kuzishusha kwa hoja nzito kwenye nyuzi za mzee Pascal huko nyuma hapa jukwaani. Yeyote anayemfahamu vizuri Kijana wa Ifoza, uandishi wangu wa kihistoria, na jinsi ninavyopingana na hoja zake kwa kutumia mifano thabiti, hawezi kamwe kufanya makosa makubwa namna hiyo ya kunifananisha na mtindo wa uandishi wa mzee Pascal.
Mtindo wangu wa kimantiki, mpangilio wa hoja, na lugha ya kiuchambuzi niliyoiweka hapa iko mbali sana na uandishi wake wa kimkakati na wa tahadhari anaoutumia kwa sasa.
Karibu sana kwenye hoja za msingi za uzi huu, na tuachane na hisia za kufikirika zisizo na ukweli wowote.


 
Sio kwamba mzee pasko anadhihakiwa, anachekwa hapana. Wanachojaribu kuongea na kusema kama (mtu) amechagua rangi ahakikisha amesimama kweli kulingana na rangi aliyo-ichagua.
 
Hapa hatubishani ili kushinda, tatizo lako ulikua unabisha kitu ambacho siyo cha kweli ukakifanya kama cha kweli sasa angalia vizuri hata hapa unachanganya matawi ya juu alijua nilichokua nabisha na wewe akakujibu na mimi nikakazia hapo, ila kwako niliweka screenshot yenye picha ya Mayalla 👇👇
🙄
Siyo kweli kama ulikua unauliza kwasababu ulikuja na hili jibu 👇👇👇👇

Jinsi ulivyojibu hapa ulikua na uhakika kabisa Mayalla siyo wakili pamoja na mimi kukupatia screenshot ya makala yake na pia kukuwekea link ya chapisho lake la jamiiforums
Kusoma LLB hakukufanyi uwe wakili na hiyo ndo ilikuwa hoja yangu na iko hivyo uiname au ulale
 
Back
Top Bottom