He's stupid as you ndio maana sikujua kama ni wakili kwa kipindi chote hicho maana hafanyi kazi zozote za kiwakiliNi wakili pia na tumeshakuonyesha, anything else..
😁😁He's stupid as you ndio maana sikujua kama ni wakili kwa kipindi chote hicho maana hafanyi kazi zozote za kiwakili
Mtaje alikua Mwenyekiti wa BAVICHA
Mie kitambo sana na nazungumzia miaka ya 2007/2008 na kuendelea nilimpa jina la “Pascal the Comedian”.Pascal is just a long winded babbling idiot who overrates himself and sometimes overrated by others who don’t know any better.
Bado sijamwona akijibu chochote kwenye uzi huu.
Ila akija kujibu, atakuja na maandishi mengi yasiyo na maana huku akiweka ma links kibao ya mada zake zingine zisizo na kichwa wala miguu.
I’ve never rated him.
Hata kwenye hiyo so called spinning hana ushawishi wowote ule.Mie kitambo sana na nazungumzia miaka ya 2007/2008 na kuendelea nilimpa jina la “Pascal the Comedian”.
Lakini niliona kitu ambacho yeye anacho kuwa ni uwezo mkubwa wa kufanya spinning and manipulation.
BICHWA KOMWE - 🤣🤣View attachment 3701049
Naam our beutiful JF BigMama 😁😎
Kwa kigeo hiki mzee Paschal is waaaay ahead of youHata kwenye hiyo so called spinning hana ushawishi wowote ule.
Hana good written communication skills.
Muda mwingi huwa anajirudia rudia tu.
Pia, anapenda sana kuchanganya lugha na akifanya hivyo huwa anakosea sana kwenye lugha ya Kiingereza.
I was a double major in college. One of my majors was communication arts with emphasis on electronic media [kiufupi, hata mimi ni trained journalist mwenye college degree].
I wrote for the college newspaper.
I had my own weekend radio show on the college’s radio station.
I shot and produced my own tv reports for the college’s tv station.
I interned at a major tv network when they still had their global headquarters in Atlanta.
When it comes to this communication business, I’m qualified to be a critic.
Jamaa hana ustadi wowote kwenye mawasiliano.
Utu uzima dawaView attachment 3701013
Wakuu, kalamu yangu leo inamwangazia mmoja wa nguzo imara za jukwaa hili na tasnia ya habari nchini, Wakili Msomi na Mwanahabari Nguli, Pascal Mayalla. Nikiwa kama shabiki wake mkubwa na mdau niliyeandika hadi makala za kiutafiti hapa jukwaani kuelezea jinsi alivyowahi kunyanyaswa na mifumo ya mamlaka kupitia "soft censorship," leo ninalazimika kuweka mezani uchambuzi wa nafsi mbili tofauti za mtu huyu mmoja.
Lengo langu si kumshusha thamani, la hasha! Nia yangu ni kutunza na kulinda heshima ya jina kubwa alilolijenga kwa jasho na damu kabla halijamomonyolewa na watu wasiomfahamu vizuri hapa jukwaani.
Pasco wa Masai Studio: Nguli wa Broadcaster na "Mpishi" vya Kitimoto
Tukirudi nyuma kidogo, jina la Pascal Mayalla lilibeba uzito wa kipekee kupitia Masai Studio, ambapo akishirikiana na wamiliki wenza wa studio hiyo kama Allyoki, walitengeneza historia ya kipekee ya habari nchini. Huyu alikuwa mwanahabari huru, mtayarishaji wa maudhui, na mtangazaji wa kwanza kabisa wa Talk Show ya kwanza ya runinga nchini—kipindi cha "Mada Moto" pale DTV mwaka 1995. Enzi hizo akiwa kijana mbichi asiye na majukumu ya kifamilia, akilipwa mishahara minono ya "six figures" kwa ushupavu wake!
Sisi kama hadhira tulimkubali bila masharti kwa sababu alisimama kama sauti ya kweli ya Muhula wa Nne wa Dola (The 4th Estate). Kilele cha uandishi na utangazaji wake kilionekana kupitia kipindi cha kihistoria cha Kitimoto kilichoruka DTV na Channel 10. Kipindi kile kilikuwa moto haswa, kiasi kwamba hata msemo wa mtaani wa kuitia nyama ya nguruwe jina la "kitimoto" ulizaliwa pale, kutokana na jinsi wanasiasa na mawaziri (kama akina Daniel Yona wa Wizara ya Fedha na Askofu Kakobe) walivyokuwa wanatolewa jasho jukwaani!
Kwenye kiti kile, Pascal alikuwa anawapika na kuwapakua wanasiasa bila uoga, akiongozwa na maswali ya mitego na utafiti mkubwa wa Masai Studio
Mabadiliko: Imekuwaje Mayalla wa Sasa Anatofautiana na Yule wa Masai Studio?
Ukiangalia mwenendo wa sasa wa mzee wetu Pascal ndani ya JamiiForums na kwenye medani za uchambuzi, kuna utofauti mkubwa unaoacha maswali mengi. Yule mwanahabari aliyekuwa anashambulia kwa mbele, leo anaonekana kuwa mtu wa kujihami, kupiga siasa za kimkakati, na wakati mwingine kuandika kwa tahadhari kubwa inayozua hisia za "kusaka teuzi" au kuegemea upande fulani, jambo linalowapa fursa baadhi ya wana-jukwaa wasiomjua vizuri kumshushia heshima yake.
Ninajua vizuri—na sote tunajua—kwamba nyakati tunazoishi sasa kimuktadha si rafiki hata kidogo. Tuko katika mazingira ya kiserikali ambayo mara nyingi yameonyesha sura ya ukatili (ruthless) na isiyothamini utu wala uhuru wa mawazo.
Dhoruba hizi si geni kwake; hata huko nyuma amewahi kukumbana na misukosuko ya kunyang'anywa leseni na kufukuzwa ofisini kisa tu kuuliza swali gumu mbele ya wakuu wa nchi. Hata hivyo, kama mwanahabari anayewakilisha muhula wa nne, Pascal anapaswa kukumbuka kuwa dhoruba hizi ni sehemu tu ya wajibu wa mwanajeshi. Unapoingia vitani, unajua kabisa utakutana na milio ya risasi na dhoruba kali, lakini uaminifu wako unabaki kwenye kupigania ukweli mstari wa mbele.
View attachment 3701014
Ushahidi wa dhoruba hizi ni huu wa hivi karibuni wa Machi 2026, ambapo Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) ilimshushia rungu la onyo yeye na Wilberforce Ngoto kule Jambo TV. Kisa kikajulikana? Kisa ni uchambuzi wake wa kiutu na kisiasa juu ya hisia za viongozi na "makofi ya msibani". Mfumo ulimtaka athibitishe hisia za moyoni za kiongozi ndani ya saa 24! Hapa ndipo tunapoona jinsi Pascal wa sasa anavyolazimika "kukiri makosa" na kupiga magoti kidiplomasia kulinda ugali na usalama wa chombo cha habari, jambo ambalo lisingewezekana kwa yule Pasco wa Masai Studio.
Vita Kuu ya Tatu ya Dunia ya Nafsi Mbili
Nikifanya hitimisho la kiweledi, nina amani ya moto kusema kuwa: Ikitokea siku moja Pascal Mayalla wa Masai Studio akakutana uso kwa uso na huyu Pascal wa sasa mwenye kofia mbili (Uanasheria na Uandishi wa Habari), lazima kitazuka vita vikali sana vya kisaikolojia na kifalsafa. Yule wa Masai Studio atamshangaa huyu wa sasa kwa namna anavyozingatia sana kujilinda na mistari ya kijani na "uchawa wa kimamlaka" unaolazimishwa na mifumo, na huyu wa sasa atamcheka yule wa zamani kwa ukosefu wa mbinu za "kisayansi" za kijeshi na kisheria za kujilinda dhidi ya dhoruba za dola.
Mzee wangu Pascal, andiko hili linatokana na mapenzi mazito kwako. Kwa jinsi unavyoshambuliwa sasa na vijana wa kizazi kipya hapa jukwaani wasiojua kabisa historia na mchango wako, ninaamini kabisa ingekuwa heri ungalifanya kazi ya Uanasheria pekee mahakamani tujue kimoja, kuliko kuendelea kuona thamani ya nguli wa habari ikishushwa na kudhihakiwa hapa jukwaani na watu wasiojua ulipotoka.
Nawasilisha, wakuu. Mzee Pascal Mayalla, karibu uwanjani utupe neno lako.
Umeeleweka mkuu ila kwa Pasco ninavyomuona uandishi ni passion yake uko kwenye damu,na Sheria keake analazimisha tu sio fani yake.nakumbuka mwaka 2005 niliishi nae mabibo hostel akisoma Sheria, ghafla nikasikia alidisco,ilimchukua miaka zaidi ya kumi kuja kupata shahada yake ya sheria.najua elimu yetu Ina mauzauza mengi ila mzee wetu hawezi kuacha kuandika,ni kitu Kiko damuni,huku kwenye Sheria nikutengeneza CV tuMkuu mdukuzi, nakushukuru sana kwa mchango wako wenye mtazamo wa kiuhalisia (pragmatic approach) kuhusu maisha, majukumu ya kifamilia, na hatari za kiusalama katika nchi yetu kwa sasa. Huu ni mjadala wa kiutu na kiweledi, na hoja yako kuhusu uwepo wa mke na watoto wanaomtegemea ina uzito mkubwa kijamii. Hata hivyo, naomba nikupe majibu yangu kwa mitazamo miwili mikuu:
Mosi, hoja yako ya kwamba ana familia na nchi yetu ina hatari ya watu "kupotezwa" ndio hasa inayolipa nguvu andiko langu. Kama umesoma vizuri uzi wangu, nimesisitiza wazi kuwa Pascal wa sasa ana kofia mbili; ni mwanahabari lakini pia ni Wakili Msomi (Mwanasheria). Ushauri wangu kwake umesimama hapo—kama mazingira ya sasa si rafiki, kama mifumo ya uandishi wa habari inamnyonga na kumweka hatarini yeye na familia yake kiasi cha kumlazimisha kuandika "kifasihi" ili kujilinda, basi ni bora angeachana kabisa na tasnia ya habari na kubaki upande wa sheria pekee. Kufanya kazi ya uanasheria mahakamani kungempa heshima yake moja kwa moja kama msomi, kuliko kuendelea kubaki kwenye uandishi wa habari ambapo analazimika kushusha hadhi na thamani ya jina lake kubwa la enzi za Masai Studio ili tu kujilinda.
Pili, tukizungumzia suala la kuwa na familia kama sababu ya kupoteza msimamo, historia ya tasnia ya habari na harakati duniani na hapa nchini inatufundisha tofauti. Kuna watu wengi waliojenga na kubaki na misimamo yao thabiti tangu wakiwa vijana wabichi hadi wakawa na mke, watoto, na wajukuu, na bado hawakuyumbishwa na dhoruba za mifumo yoyote ya kimamlaka. Katika tasnia ya habari, uaminifu kwa ukweli na taaluma (editorial integrity) hauishii pale mwanahabari anapooa au kupata watoto; bali unakuwa sehemu ya urithi (legacy) anaowaachia hao watoto wake.
Ndio maana nasema, lengo si kumshusha thamani mzee wetu, bali ni kuhoji: Ikiwa ulingo wa habari umekuwa wa moto sana kiasi cha kutaka kuhatarisha usalama wa familia yake, kwanini asivue kofia ya uandishi na kuvaa joho la uanasheria pekee ili kulinda heshima ya jina lake?
maneno makali ya nini kiongozi?He's stupid as you ndio maana sikujua kama ni wakili kwa kipindi chote hicho maana hafanyi kazi zozote za kiwakili
Huyu wa sasa anajiita P.Yule wa masai studio ni Paskali huyu wa jamii forum ni Pasco 😄
Yule wa Masai studio alikuwa na uwezo mpaka wa kumuuliza waziri wa fedha Daniel yona kuwa yeye na Rais mkapa nani analipwa mshahara mkubwa?
Huyu wa jf hawez hata kumuuliza balozi wa nyumba kumi ana majukumu gani kwenye nyumba kumi zake 😄
Wabongo ukiwa na maneno mengi hata kama hamna points wanakuona muelewa. We wazungushe, wapeleke, warudishe, define hiki na kile basi.Pascal is just a long winded babbling idiot who overrates himself and sometimes overrated by others who don’t know any better.
Bado sijamwona akijibu chochote kwenye uzi huu.
Ila akija kujibu, atakuja na maandishi mengi yasiyo na maana huku akiweka ma links kibao ya mada zake zingine zisizo na kichwa wala miguu.
I’ve never rated him.
Mfano mzuri ni wa Professor wa kuokotwa jalalani na yule Prof Kiti, Dr Bash.Mara nyingi mtu anakuwa ni yule yule tu ila mazingira ndiyo yanabadilika na kumuonesha katika sura tofauti. Anavyo react tofauti katika mazingira tofauti.
Ila ile core character ya mtu, sisemi kuwa haibadiliki, ila kubadilika ni vigumu sana.
Ni rahisi zaidi kuona mtu kabadilika kwa kuwa wewe ulikuwa hujamuelewa vizuri kuliko kuona mtu kabadilika kwa sababu kabadilika kweli.
Ndiyo maana watoto wa mjini wanasema "Shika hela tujue tabia yako". Kwa sababu wanaamini kuna tabia nyingine utazificha kwa kuwa huna hela tu, ukipata hela ndiyo zinajulikana.
Yani inawezekana ulionekana mpole kwa sababu hukuwa na nguvu ya hela tu, ulivyopata hela kila mtu akajua kuwa kumbe ule upole wote ilikuwa kwa sababu huna hela tu, umepata hela wameona upande mwingine, kumbe wewe si mpole hivyo.
Kwa hiyo kuna tabia nyingine zinakuwa zimekaa tu latent, kama mbegu iliyokaa udongoni inasubiri mvua kuchipua. Ikipata mazingira mazuri ya mvua, inachipua.
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na tabia zake kazificha mpaka apate mazingira ya kuzidhihirisha, akipata mazingira yake ya kuzidhihirisha, anazidhihirisha.
Halafu nyie wa nje mkimuangalia, mnaona kabadilika. Kumbe yupo hivyo siku zote, alikuwa kaficha makucha tu.
Kumbe hajabadilika, mlikuwa hamjamfahamu vizuri tu.
BICHWA KOMWE umetoka mchicha sana hapaView attachment 3701049
Naam our beutiful JF BigMama 😁😎
Wabongo ukiwa na maneno mengi hata kama hamna points wanakuona muelewa. We wazungushe, wapeleke, warudishe, define hiki na kile basi.