Kwa kweli hili jambo huwa linanisikitisha sana , nchi yetu ni ya Kidemokrasia lakini tumezidiwa maarifa mpaka na wanyama wa kufugwa nazungumzia ( Ng'ombe, Kondoo na Mbuzi)
Ng"ombe wakitaka kumpata kiongozi wao madume hupigana kweli kweli watavunjana pembe, watatoana mpaka damu anayeshinda huonekana.
Kondoo hupigana vichwa kweli kweli anayesikia kizunguzungu huwa ameshindwa uongozi
Mbuzi pamoja na kuwa na akili mbovu huwa mabeberu wanapigana mpaka wanatoana damu na kuvunjana mapembe.
Inakuwaje sisi Watanzania tumekuwa na akili za hovyo kama huna uadilifu kaa pembeni sio hizi mambo za kutumia watu kujusafisha au kutumia majolica na vyombo vya ulinzi na usalama kwa manufaa yako.
Hii ni mbaya kupita ubaya wenyewe.