Mkuu
mdukuzi , kumbe wewe wa longi!, humu JF siku hizi kumejaa madogo hawachelewi kutukana, utadhani tunalingana nao!.
Duh kumbe tulikuwa tunaishi wote Mabibo!.
Hukunitendea haki kabisa Watanzania huwa tunasalimiana hata kama hatujuani, japo mimi ni kweli niliwahi kuwa maarufu, lakini sikuwahi ku behave ki super star, mimi ni mtu wa kawaida sana!.
Ni kweli niliingia UDSM kusoma LL.B, sikuwahi ku supp hata somo moja. Mwaka wa 4, mtihani wa mwisho kuna ticha mmoja akanifutia matokeo yangu ya UE kwa somo lake hivyo nikapigwa a technical DISCO for absconded!.
Issue ilikuwa hivi, yule ticha ananijua, tulikutana mitaani mitaa ya Sinza kwenye mambo yetu yale, denti ukampita ticha, ticha akamaind hivyo akafuta matokeo yangu na kupigwa disco!.
Nikafuatilia matokea ya external examiners somo lake nina A!. Nikaapeal kwa dean by then ni Dr. Ibrahim Juma. Ticha alipoulizwa kwanini amenifutia matokeo, akamwambia dean amefuata almanac ya UDSM ili uweze kufanya UE, lazima uwe umehidhuria course work 60%. Ticha akamwambia dean hajawahi kuniona kwenye somo lake hata mara moja, akasisitiza namjua Pasco na sijawahi kumuona darasani kwangu.
Mimi nikajitetea darasa tuko wanafunzi 400!, utajuaje kama nipo au sipo?. Nikamwambia hata siku ile anauliza swali class na kuniita kwa jina, sikuitika kwasababu nilikuwa sina jibu na sio kweli sijahudhuria somo lake!.
Dean Dr. Juma akaamuliza, jee ame miss hata course work moja?. Sijamiss!. Dipo dean akampiga masomo mawili
1. Uthibitisho wa mwanafunzi kuhudhuria lecture ni kupitia attendance register na sio kuangalia sura eti unamjua na hujamuona!. Jina langu kwenye attendance register, lipo vipindi vyote!.
2. Prospectus ya chuo kwa Mwanafunzi ambaye hajahudhuria 75% anatakiwa kuwa barred na kuzuiwa ku sit for EU, mimi was not barred, mwanafunzi akiisha sit for UE na matokeo yatatoka, hawezi kufutiwa matokeo yake, hivyo nilishinda appeal, nikapata LL.B yangu with honours!.
Siko TV yoyote siku hizi. Mimi ni freelance hivyo naingia TV yoyote.
Asante ila sii kweli kuwa hakuna mwana JF anayenifikia, if tuna manabii kibao!
Tanzania tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!
Asante nimekusikia, mtu akiisha kuwa Mkatoliki mzuri, hawezi kufungua kanisa.
Mimi ni mpinzani wa kuchanganya dini na siasa
Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?
Ukiisha ita ni pepo la utambuzi hizo ni nguvu za giza, ila pia ni ngumu kubaini maono fulani kama yanatoka kwa Mungu au kwa shetani, mfano hapa,
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P