Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Mkubwa kumbe nawewe kuna watu wanakutia hasira japo huwaoni, JF ina wapumbavu wengi sana ndiomaana verified user wanapungua,
It's true, binadamu tunatofautiana viwango vya uvumilivu na ustahimilivu, kuna watu ukijikuta unatukanwa na vitoto vidogo, unaamua kuliko kujivunjia heshima bora uachane nayo, mimi mwenyewe niliisha amua kuachana na JF not once not twice, several times ila very unfortunately nikajikuta ni mraibu wa JF, nikashindwa!. Mtu yoyote akinitukana humu, hatua ya kwanza ni kumngongolia like, kisha namsamehe, kwa hoja kuwa hajui atendalo, hasira zinapoa maisha yanaendelea.
P
 
Asante sana othuman dan fodio , kila nikiliona jina lako nakumbuka Usman dan Fodio, ambae jina lake pia kuandikwa Uthman au Usuman, na kwa Kiarabu ni ʿUthmān Ibn Fūdī, alizaliwa December 1754, kijiji cha Maratta, mji wa Gobir, kwa kabila la wa Hausa na wa Sokoto, nchi yao akiitwa Hausaland ambayo sasa ni Nigeria, alikuwa ni kiongozi wa Sokoto na Fulani empire, alikuwa na nguvu fulani za mystic, powers, ndiye aliyeanzisha vita vya jihad kati ya mwaka 1804 hadi 1808, na kuifanya Nigeria kuwa ni nchi ya Kiislamu licha ya kuwa ndilo taifa la Africa linaloongoza kwa idadi ya Wakristu!, alikufa mwaka 1817, hivyo kila nikikutana na post yako yoyote, kwanza inakula like yangu!.

Hii JF ya sasa ina majitu majinga mengi, yasiyo na good thinking capacity, kama kila mtu mwenye akili nzuri atapaswa kuteuliwa nani wataleta maendeleo ya nchi hii?. Wanaoteuliwa waachwe wateuliwe, halafu sisi wengine, kama tuna akili nzuri, tuzitumie basi hizo akili zetu nzuri kuleta maendeleo kwenye taifa letu huku huku tulipo na sio mpaka tuteuliwe. Mfano mzuri ni mimi mwenyewe hapa nilipo namsaidia sana Samia kuliko hata ningeteuliwa nafasi yoyote!. Msaada wangu mkubwa kwa Samia, ni kumweleza kuwa everything happens for a reason!, hakuna kitu chochote kinachotokea bila sababu, hivyo ni watu wanache mimi nikiwemo ambao tunajua sababu za ni kwanini mtu wetu yule alitwaliwa!. Blaza ni karma ilikula kichwa!, hivyo tunawajibu wa kumsaidia Mama Samia kwa kumkinga asirudie makosa ya mtwaliwa kwa kugenerate bad karma ikaja kumponza na yeye akaishia... Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma hivyo kitendo tuu cha kutoa elimu ya karma kwa Rais Samia ni msaada mkubwa sana kwake kuliko ningeteuliwa kushika nafasi yoyote!.

Sio pengine huo ndio ukweli. Watu hawajui nimesoma shule moja primary na Dr. Mwinyi, shule hiyo watoto wa vigogo wote ndio tulikuwa nao kuanzia Nyerere, Kawawa, Malecela na mawaziri wote!. Dr Mwinyi alinitangulia darasa, sekondari Tambaza nimesoma class moja na mtoto wa Ben baadae Dr. Mwinyi akajoin Tambaza A level. Pia class yetu Tambaza tulikuwa na mtoto wa Nyerere.

Ilboru A level nimesoma darasa moja na mtoto wa Warioba. UDSM nimesoma na Riz-1. Nikitembelea Geita, Biharamulo, Katoro, nalala nyumbani kwa Magufuli!. Hivyo I'm a well connected person, ningetaka uteuzi ningelobby!.

Kuna watu wa ajabu ambao hatuzimikii kabisa teuzi zozote za ubwete. Mimi ni mmoja wa watu hawa!.
P
Bravo, ume dig deep bro. Especially the history of usman Dan fodio.

By the way una kitu bro.
 
Kawaida sana ukichovya anapochovya prof disco linakuhusu
Wala sidhani kama hata alichovya, kuna wanafunzi tulisoma chuo tukiwa na Ankara ya kutosha! Pale Block F kule juu kwenye single rooms, kuna denti demu nilimlipia room na kugharimia kila kitu including Flat screen, microwave and sikupata kitu!, sasa unapokuta na ticha mitaa ya Sinza, ticha anapigwa chini fasta, tatizo la Sinza huwezi kujiweka ukawa ni wewe tuu!.

Tatizo kama hilo la disco la chuo, lilikuja kunikuta TBC!, napita mahali kumbe the top boss amejiweka!, kufunga kufungua nilikula summary Dismissals for insubordination!, haina appeal ni unafungasha you go!.
P
 
Mayalla ni very professional. Hilo liko wazi sema hata career yake ya uandishi wa habari angepata nchi yenye uhuru kama Kenya mfano angekuwa moja kati ya waandishi na wanahabari Bora.
Tatizo misingi ya serikali yetu haikumpa nafasi kudevelop zaidi ya kuwa chawa na green guard.
Simjui,hanijui but this mzee is so smart. Natamani siku moja nimuone kwenye nafasi kubwa akiongoza nchi.
Kama wachekeshaji,maslay queen na wasiojua lolote wameweza mayalla ndo aje ashindwe
He is professional but not very, hauwezi kuwa very professional kwenye uandishi wa habari huku moyoni mwako ukiwa umejaa chuki kwa makundi yenye mrengo tofauti na wewe, lazima taarifa zako zitakuwa za upande mmoja na hilo ndilo nimekuwa nikimfahamisha hawezi na hatakuwa Lakha mpya ambaye ni role model wake.
 
Nabii alietumwa kutufikishia ujumbe kwa walimwengu wote ni Nabii MUHAMMAD (S.A.W) na ndio Nabii wa mwisho, baada ya yeye hakuna tena.

Hivyo mleta mada acha kumkosea Mwenyezi Mungu, futa haraka hii mada.
 
Dah Mkuu Pascal Mayalla, Hakika tunajifunza Mengi Sana toka Kwako. Mungu Akubariki Sana. Hawa Watoto Wadogo Wadogo Wasamehe tu kwa sababu wewe Umeshakuwa Babu yao Wengine Kwahiyo zichukulie kama Matani na Kero za Wajukuu kwa Babu yao trust me siku Ukiondoka watakumiss sanaa. Na huwezi jua wao ndio wanaweza kukuombea huko uliko so let's take easy. Unajua thamani ya kitu isipoonekana wakati kipo, itaonekana tu wakati hakipo.

By the way, haya maandiko yako ni reference ya Miaka na miaka ijayo labda JF iwe shutdown ila ikiiendelea kuwepo basi vizazi na vizazi vitapitia maandiko haya.

Pia fikiria kuyaweka kwenye vitabu mkuu I think it will be a good thing.
 
..... Mfano lile swali langu kwa JPM kuhusu mikutano ya siasa, Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli ndilo limempelekea Rais Samia kuruhusu mikutano ya siasa!.

Unajua that day na mimi bahati nzuri nilikuwa nafuatilia live ile Press Conference pale Ikulu na nilishangaa sna Why the Late Aliku attack isivyo kawaida kabisa kwa ajili ya kumpiga lile swali.

Hivi Mkuu unahisi Shida hasa ilikuwa ni nini mpaka that Man akareact vile? Ni swali tu au kulikuwa na mengine behind the curtain?
 
Wala sidhani kama hata alichovya, kuna wanafunzi tulisoma chuo tukiwa na Ankara ya kutosha! Pale Block F kule juu kwenye single rooms, kuna denti demu nilimlipia room na kugharimia kila kitu including Flat screen, microwave and sikupata kitu!, sasa unapokuta na ticha mitaa ya Sinza, ticha anapigwa chini fasta, tatizo la Sinza huwezi kujiweka ukawa ni wewe tuu!.

Tatizo kama hilo la disco la chuo, lilikuja kunikuta TBC!, napita mahali kumbe the top boss amejiweka!, kufunga kufungua nilikula summary Dismissals for insubordination!, haina appeal ni unafungasha you go!.
P
Umenikumbusha mbali sana Block F block ya postgraduate ila nilitumia ujanja wa mjini nikiwa undergraduate nikapata room hilo block.hiyo ya kumendea mzigo wa boss imeoonza wengi sio wewe tu,tangu enzi za Yusuf na Farao ,pole sana ila lazima kuna kitu ulijifunza hapo
 
Hii ni moja ya issues... Usidhani tunamjadili mzee mayalla,tunachokijadili hapa ni kilichobebwa/ kilichomo ndani ya mayalla. Huyu ana uzoefu wa hali ya juu kwenye diplomasia,habari,usalama wa nchi,kuijua vyema katiba na sheria za nchi na uzoefu katika mambo ya utawala.
Tuseme ukweli mayalla ni kiongozi anayepotea kutokana na nepotism na poor governance ya viongozi wetu.
Jokate ameweza
Sabaya
Makonda
Ally happy
Chalamila
Nape
Kafulila
Mwana FA
Ety mayalla aje ashindwe. Huu ni uchawi kabisa. Sio bure.
Inawezekana ipo sehemu ana hudumu mkuu
 
Mkuu mdukuzi , kumbe wewe wa longi!, humu JF siku hizi kumejaa madogo hawachelewi kutukana, utadhani tunalingana nao!.

Duh kumbe tulikuwa tunaishi wote Mabibo!.

Hukunitendea haki kabisa Watanzania huwa tunasalimiana hata kama hatujuani, japo mimi ni kweli niliwahi kuwa maarufu, lakini sikuwahi ku behave ki super star, mimi ni mtu wa kawaida sana!.

Ni kweli niliingia UDSM kusoma LL.B, sikuwahi ku supp hata somo moja. Mwaka wa 4, mtihani wa mwisho kuna ticha mmoja akanifutia matokeo yangu ya UE kwa somo lake hivyo nikapigwa a technical DISCO for absconded!.

Issue ilikuwa hivi, yule ticha ananijua, tulikutana mitaani mitaa ya Sinza kwenye mambo yetu yale, denti ukampita ticha, ticha akamaind hivyo akafuta matokeo yangu na kupigwa disco!.

Nikafuatilia matokea ya external examiners somo lake nina A!. Nikaapeal kwa dean by then ni Dr. Ibrahim Juma. Ticha alipoulizwa kwanini amenifutia matokeo, akamwambia dean amefuata almanac ya UDSM ili uweze kufanya UE, lazima uwe umehidhuria course work 60%. Ticha akamwambia dean hajawahi kuniona kwenye somo lake hata mara moja, akasisitiza namjua Pasco na sijawahi kumuona darasani kwangu.

Mimi nikajitetea darasa tuko wanafunzi 400!, utajuaje kama nipo au sipo?. Nikamwambia hata siku ile anauliza swali class na kuniita kwa jina, sikuitika kwasababu nilikuwa sina jibu na sio kweli sijahudhuria somo lake!.

Dean Dr. Juma akaamuliza, jee ame miss hata course work moja?. Sijamiss!. Dipo dean akampiga masomo mawili
1. Uthibitisho wa mwanafunzi kuhudhuria lecture ni kupitia attendance register na sio kuangalia sura eti unamjua na hujamuona!. Jina langu kwenye attendance register, lipo vipindi vyote!.
2. Prospectus ya chuo kwa Mwanafunzi ambaye hajahudhuria 75% anatakiwa kuwa barred na kuzuiwa ku sit for EU, mimi was not barred, mwanafunzi akiisha sit for UE na matokeo yatatoka, hawezi kufutiwa matokeo yake, hivyo nilishinda appeal, nikapata LL.B yangu with honours!.

Siko TV yoyote siku hizi. Mimi ni freelance hivyo naingia TV yoyote.

Asante ila sii kweli kuwa hakuna mwana JF anayenifikia, if tuna manabii kibao! Tanzania tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!

Asante nimekusikia, mtu akiisha kuwa Mkatoliki mzuri, hawezi kufungua kanisa.

Mimi ni mpinzani wa kuchanganya dini na siasa Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Ukiisha ita ni pepo la utambuzi hizo ni nguvu za giza, ila pia ni ngumu kubaini maono fulani kama yanatoka kwa Mungu au kwa shetani, mfano hapa, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
Nimecheza hapo pia wewe na mwalimu wako na namna prof Ibrahimu juma alivyo maliza mkasa huo na namna ulivyo pambania haki yako ,lakini pia nimecheka unaposema ulipoitwa jina lako kujibu swali hukuitika kwa kuwa hukuwa na majibu ya swali.
 
Wala sidhani kama hata alichovya, kuna wanafunzi tulisoma chuo tukiwa na Ankara ya kutosha! Pale Block F kule juu kwenye single rooms, kuna denti demu nilimlipia room na kugharimia kila kitu including Flat screen, microwave and sikupata kitu!, sasa unapokuta na ticha mitaa ya Sinza, ticha anapigwa chini fasta, tatizo la Sinza huwezi kujiweka ukawa ni wewe tuu!.

Tatizo kama hilo la disco la chuo, lilikuja kunikuta TBC!, napita mahali kumbe the top boss amejiweka!, kufunga kufungua nilikula summary Dismissals for insubordination!, haina appeal ni unafungasha you go!.
P
Nanukuu

"Tatizo kama hilo la disco la chuo, lilikuja kunikuta TBC!, napita mahali kumbe the top boss amejiweka!, kufunga kufungua nilikula summary Dismissals for insubordination!, haina appeal ni unafungasha you go!.
P"


Kuna watu hujigeuza miungu watu binafsi Mimi siwezi fanya unyama huo Bora awe mke ila hawara😊😊

Bora hata angekuita akakupa...
ULTIMATUM (a threat when you tell someone that if they don't undertake a specific action, they'll face a consequence)
 
Mkuu KUTATABHETAKULE , haijawahi kuwa hiyo, ilikuwa ukimaliza LL.B, lazima u petition kwa CJ ndio uwe wakili na sio ukimaliza tuu tuu unakuwa wakili direct. Hii ndio sababu imenicheleweshea kuupata uwakili. Ukiwa ni mtaka haki mno sometimes it's not good, kuna vitu vingine ni haki yako you just have to let them go, hilo mimi nimeshindwa.
Nimemaliza chuo kabla ya utaratibu wa law School, nikakabidhiwa LL.B yangu enzi za law School. Nikapetition nikakataliwa eti Degree inahesabika from the day it was conferred to you na sio mwaka uliohitimu!. Kiukweli ilikuwa kazi!, mpaka kuupata huu uwakili!. Acha tuu ni wind up huku kwenye media, ndipo niuanzie uwakili na kiukweli kwa jinsi nilivyo mbishi, kuna kazi inakuja!.
P
Kila la kheri Mkuu.
 
Back
Top Bottom