Paskali Mayala, mbona huleti "analysis" ni nini zitakuwa athari kisiasa za uamuzi wowote kesi ya Mbowe?

Mkuu NewPage, asante sana kwa kuniuliza na kwa maoni yako, hili la hii kesi ya Ugaidi ya Mbowe, kwanza sikupenda kuijadili kesi ikiwa mahakamani kwenye commital proceedings ili tusiingilie uhuru wa mahakama kwa kufanya contept of the court.
Ila mimi kama mwandishi, nimeisha andikia makala, nyingi za kusaidia upatikanaji wa haki. Karibu pande hizi
Kwa hii stage kesi ilipofikia, hearing imemalizika sasa ni wakati wa mahakama kuamua kama Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu au la, kwa vile na mimi nilifuta tongotongo za Sheria pale UDSM, hivyo kabatini kwangu kuna LL.B (hons) ya UDSM imelala tuu, hivyo baadhi ya hoja za maoni yangu, zinaweza kusaidia.
1. Nimeshauri Mbowe asamehewe tuu bila masharti yoyote, kwa DPP kufuta hii kesi kwa nolle.
2. Kitendo cha rais Samia alipohojiwa na Salim Kikeke, lile jibu la rais kuhusu kesi hii, lilitosha kuimaliza there and then.
3. Mbowe kuomba msamaha hawezi itakuwa ni kama kukiri kosa la ugaidi, kuliko kukiri kosa anaona bora kesi iendelee ili mahakama ndio itamke ama ana hatia, ama hana hatia.
3. Katika usikilizaji wa upande wa mashitaka, umeonyesha hoja nyingi zenye makosa ya kisheria justify hii kesi kuwa dismissed.
4. Hata ikikutikana Mbowe hana hatia, mahakama kumtamka hawana kesi ya kujibu, au baada ya kusikiliza utetezi wao, mahakama kuwatamka not guilty, ni changamoto!. This is an embarrassment for the government hivyo kutamfanya Mbowe shujaa na kiukweli akiachiwa, sio tuu kutamfanya Mbowe shujaa, bali Mbowe na Chadema watasumbua sana!.
5. Hivyo ili kum contains Mbowe ni kumpa a case to answer na hata baada ya kujitetea atapewa a guilty verdict na kumpiga mvua kadhaa, ili kumshikisha adabu!.
6. Baada ya kula mvua, ndipo shujaa, mwokozi na mkombozi wa Mbowe ataibuka na msamaha wa rais, Mbowe ataachiwa akiwa mnyonge na hawezi kugombea post yoyote, he'll be done, finished, finito!.
Asante sana. Hilo la msamha wa Rais sikulifikiri na kwa mwelekeo wa kesi ulivyo mpaka sasa bado unaamini atakula Mbowe atakula mvua?
Kwa mwenendo wa kesi mpaka sasa kwa upande wa haki bin haki, Mbowe anatakiwa ashinde kesi kwa kipengele kinachoitwa "the benefit of doubt", kufuatia mashahidi wa Jamhuri, kujikanyaga kanyaga, hivyo mahakama kushindwa kuestablish kitu kinachoitwa "prima facie" by proving jinai beyond reasonable doubt, hivyo uamuzi wa haki bin haki, ama DPP aiokoe serikali kwa Nolle, au serikali inakwenda kushindwa, uamuzi huu utai embarrass sana serikali, na Mbowe kuibuka shujaa wa karne!, kwa kutoka kifua mbele mabega juu na atasumbua sana, hivyo ili to save government faces, and to contain him, utatolewa uamuzi wa kisiasa kuwa Mbowe ana kesi ya kujibu, na uamuzi ni kwa kumpiga mvua kadhaa, halafu baada ya muda mfupi, Mama atatoa msamaha wa rais, Mbowe ataachiwa kwa msamaha, atatoka amenyon'gonyea, huku ameinamisha kichwa chini, mabega chini, na hawezi kugombea chochote!.
P
 
Asante sana. Hilo la msamha wa Rais sikulifikiri na kwa mwelekeo wa kesi ulivyo mpaka sasa bado unaamini atakula Mbowe atakula mvua?
 
Utabiri wa Mayala unaweza ukawa na ukweli?
 
Du! Paskali kwa hii thread ninakufuatilia sana!
 
 
Kwa hiyo kakangu Paskali athari mojawapo kwa uamuzi wa kesi ya Mbowe ni kukufanya uwe mwanaCCM?
 
Pascal Mayalla ameishia kumsifia mamake tu eti kafanya maamuzi magumu anasahau NGUVU YA UMMA ndio imeifikisha sirikale ya mamake iliyopambana kutengeneza KESI YA MICHONGO na ikabuma na hatimae kukubali matokeo ya NGUVU YA UMMA
kikwetu MAYALA manake ni NJAAKALI😎😉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…