Passo na rav4 kilitime mjapan kachemka

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana jf,
Katika magari mabovu passo na kilitime rav4 zinaongoza kuharibika reki End na shock Up za mbele, niliagiza passo kukabiriana na hali ya mafuta, lakini gari hili baada ya miezi mitatu ikaanza kugonga nikapeleka kwa fundi nikaambiwa ninunue full staring system ambayo used ni laki 3, sikutaka used nikaenda Toyota nikaambiwa laki tano. Fundi kaniambia nisisumbuke kwani hii inajazwa na inatulia, kweli ikatulia mwezi, Kwa sasa ni mbovu kuliko mwanzo. Mwenye uzoefu na spare nafuu anisaidie vyuma vimetaiti.
 
Kuna baadhi ya magari hua yanapata shida sana kweke kuhimili huu ubovu wa 'barabara' zetu....zimekua designed for njia za japan huko mijini (njia nzuri uki compare na za kwetu) ...Ni vizuri ukanunua mpya ukafunga at least unaweza kaa nayo kwa mda mrefu zaidi
 
Passo sio gari basi tu mi nlikinunua kipya kama wewe ili kusave mafuta.kilichonipata sintosahau ki-gari kinagonga balaa.Nikaambiwa stering lake imekufa nkanunua mpya bado vile vile.kukiuza sasa pia ukawa mziki nkaamua kufanya biashara ya kuvunja.Nikampa passo Dalali nkamuongezea na pesa akanipa NOAH
 
Tunasingizia magari ya watu lakini hatuongelei core problems. Shida kubwa Tanzania ni miundombinu, hatuna miundombinu ya kuzitumia hizi gari ni basi tu.

Ni wangapi wanatoka home straight to work bila kucheza na korogesheni? Unakuta mtu anaishi ndani huko 6km away hadi afike lami gari imeumia balaa.

We simply don't have proper roads.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…