Tukisema sport suspension, hatumaanishi gari za mashindano. A sport-tuned suspension inakuwa ngumu, kwa Kiswahili rahisi ni kwamba haibonyei sana kama normal suspension. Hii inasaidia saana kama unaendesha gari kwenye race track au barabara zenye kona. Inapunguza body roll, handling inakuwa nzuri, hata steering inakuwa ngumu na mara nyingi zinakuwa chini sana. Hivyo ile wheel travel inakuwa ndogo.
Sasa inapokuwa ngumu, huwa haiwezi ku absorb shocks kama suspension ya normal au comfort. Kama umeshaendesha gari kama Altezza, au BMW3 series au Crown Athlete ukaweka sport mode utanielewa vizuri. Ukipita kwenye bonde unalisikia zaidi, hata ya Corolla. Ndio maana most people wanasema sport cars ziko uncomfortable sababu hawaelewi suspension zimekuwa tuned hivyo kwa malengo maalumu. Hizo gari unazosema wewe mfumo wake wa suspension ni tofauti. Maana handling sio lengo lake. Pia ni extremely uncomfortable humo ndani. Japo suspension zake sio sporty, maana zinatakiwa ku absorb bumps za kutosha.