Passo na rav4 kilitime mjapan kachemka

umeongea point mkuu unakuta gari imetembea kilometa 60,000 japan lakini haijapata shida lakini ikija bongo kilometa 2000 tu gari hoi. barabara zetu haziendani na haya magari coz unakuta ground clearance ni ndogo halafu gari inapita kwenye matuta na mashimo ya hatariii
 
Mkuu tufanye biashara,niuzie mimi hiyo passo
 
Hivi kama we ni mtu wa Lami tu hizi gari kumbe zinadumu sana hutaumiza kichwa kuchagua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha msingi ni kununua gari sahihi kwa matumizi sahihi. Rav4s zimetengenezwa kutumika kwenye barabara nzuri (on-road vehicles). Hata ile AWD yake lengo ni kusaidia kwenye snow tu na wala sio kwenda off-road. Sasa sisi uendeshaji wetu, na barabara zetu mara nyingi ni changamoto kubwa. Ukizingatia suspension set up ya Rav4 ni sporty kidogo, ndoa maana nyingi sio comfortable kivile ukiwa kwenye roughroad, so uwezo wake wa kuabsorb shorks za kwenye rough road ni kidogo. Ila ukijua matumizi yake, kidogo haitasumbua saana. Paso kwa kweli sina uzoefu nazo, ila kwa jinsi kalivyo kadogo, nafikiri hakafai kabisa kuwa molested.
 
Inamaana suspension za sport hazi absorb shocks.. Vipi zile gari za sport zinazokimbia offroad
 
Inamaana suspension za sport hazi absorb shocks.. Vipi zile gari za sport zinazokimbia offroad
Tukisema sport suspension, hatumaanishi gari za mashindano. A sport-tuned suspension inakuwa ngumu, kwa Kiswahili rahisi ni kwamba haibonyei sana kama normal suspension. Hii inasaidia saana kama unaendesha gari kwenye race track au barabara zenye kona. Inapunguza body roll, handling inakuwa nzuri, hata steering inakuwa ngumu na mara nyingi zinakuwa chini sana. Hivyo ile wheel travel inakuwa ndogo.

Sasa inapokuwa ngumu, huwa haiwezi ku absorb shocks kama suspension ya normal au comfort. Kama umeshaendesha gari kama Altezza, au BMW3 series au Crown Athlete ukaweka sport mode utanielewa vizuri. Ukipita kwenye bonde unalisikia zaidi, hata ya Corolla. Ndio maana most people wanasema sport cars ziko uncomfortable sababu hawaelewi suspension zimekuwa tuned hivyo kwa malengo maalumu. Hizo gari unazosema wewe mfumo wake wa suspension ni tofauti. Maana handling sio lengo lake. Pia ni extremely uncomfortable humo ndani. Japo suspension zake sio sporty, maana zinatakiwa ku absorb bumps za kutosha.
 
Mkuu isipoabsorb shock handling itakuaje rahisi?
 
Mkuu isipoabsorb shock handling itakuaje rahisi?
Mbona hapo juu nimeeleza kwa kirefu. Kwanza sijasema kwamba haiabsorb kabisa, nimesema ina absorb kidogo kulinganisha na normal suspension.

Ina handle vizuri sababu ina kuwa kama imekumbatia barabara which means inakuwa haina body rolls. Ina absorb kidogo sababu ina wheel travel ndogo kuliko normal suspension, na inakuwa ngumu. So hainepi nepi saana. Kwa kweli, kama hujaelewa mpaka sasa, mpaka uendeshe sport cars ndio utanielewa vizuri.
 
Ni katika kuuliza ili kufaham mkuu..
 
Ni katika kuuliza ili kufaham mkuu..
Okay, unajua sport cars, lengo lake kubwa ni kufurahia kuendesha. Ndio maana zinaitwa drivers cars, kuliko kutoa comfortability. So, ili kupata that feeling ya kuwa connected na barabara, kuna vitu huwa vinafanyika kwenye tuning ya gari. Kwanza kabisa, lazima urefu au height ya gari iwe lowered. Ndo maana unaona gari kama BMW 3 Series ziko chini. Kina Ferrari, Lamborghini hizo siongelei kabisa, maana ni kama zinagusa barabara kabisa.

Sasa ukishafanya hivyo, lengo ni kuhakikisha gari halilalii upande mmoja wakati unakata kona. So unaweza kata kona ya kulia then ukarudi kushoto na gari bado limetulia njiani. Vile ni fupi, na suspension hazinesi saana. Hii ndio tunaita handling. Sasa suspsion kuwa comfortable, inamaana ile coil spring yake, ni ndefu, ili iweze kunepa saana. So inapokata kona za ghafla, gari likinepa kushoto na kurudi kulia linakosa balance, so inakuwa rahisi kupinduka. Sawa na mtu mrefu na mfupi kwenye kupiga kona za ghafla.

Suspension ikiwa comfortable, gari inakuwa na grip kubwa, meaning inashika barabara saana. Sasa hii sio nzuri kwa sport cars, maana ikishika barabara inamaanisha gari linakuwa halikimbii saana au linatumia nguvu kubwa kukimbia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…