Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Unajuaje kakaa kimya? Mbona alishatoa taarifa?
Hivi umesahau Sokoine alifukuzwa kazi kwa kwenda kumuona Lissu hospitali?
Unafikiri naji katika Ubalozi atampa passport Lissu bila Rais Samia kusema?
 
Inaelekea watu bado wanafanya kazi kama awamu iliyopita...zama zile kutoa passport kwa mtu kama Tundu Lissu ni kujitafutia kutumbuliwa tu....taratitu zinaaply kwa wananchi wa kawaida tu...
Nina binti ya rafiki yangu,jina lake la mwisho ni jina ambalo mwendakuzimu alikuwa na ugomvi naye.
Amezungushwa pale uhamiaji kupata pass mpya mpaka akaomba msaada wa waziri mmoja ndio akafanikiwa.
Jamaa alipandikiza chuki na uoga mpaka chini na mbaya zaidi ni kuwa "business as usual" inaendelea.
 
Lissu kasema ameomba passport mpya na wamemzungusha?

Halafu, kama ulichodai ni kweli, kwa nini haya yanatokea chini ya Samia?
Una uhakika hayatokei? Lissu aliomba guarantee ya usalama wake tokea Samia anaingia, Mbona hajapewa?
Mbona hajalipwa haki zake za Bunge tokea Samia aingie madarakani?
Mbona Mbowe anateseka wakati sasa ni Samia?
Chuki zenu zinawafanya kushindwa hata kufikiri logically
 
1. Hakuna mtu anayeweza ku guarantee usalama wa mtu.

2. Samia anahusikaje na mambo ya kibunge? Masuala ya stahili zake za kibunge ni suala la mhimili mwingine. Au hatuna utenganisho kati ya mihimili yetu hiyo mitatu?

3. Kuhusu Mbowe, hilo nakubali.
 
Kuna watu walikuwa wanapinga ule mtindo watu kumlalamikia Magufuli kesi zao, walisema ni ushamba walipaswa kufuata taratibu kwa kupeleka malalamiko yao sehemu husika ila si ajabu hiki alichokifanya Lissu watakitetea.
 
Unataka wezi waeleze mbinu zao hadharani?
 
1. Hakuna mtu anayeweza ku guarantee usalama wa mtu.

2. Samia anahusikaje na mambo ya kibunge? Masuala ya stahili zake za kibunge ni suala la mhimili mwingine. Au hatuna utenganisho kati ya mihimili yetu hiyo mitatu?

3. Kuhusu Mbowe, hilo nakubali.
Mtu usalama wake ukiwa hatarini, nchi humps ulinzi. Samia alikataa kumpa ulinzi Lissu.

Samia ni business as usual kama Mwendazake tu.

Mnajifanya hamjui na hamuoni dhuluma ambazo Lissu kafanyiwa.

Kama Samia ha husiki na Bunge Kwanini aseme Ndugai alimwambia kesha lipwa haki zake zote?
 
Kama mange kimambi tu, ku renew hati yake ya kusafiria walimkataliaa katakataa, kuwa wizara imezuiwa kufanya hivyo , hadi awamu ya sita tena kupitia kwa rais ndio akapewa nyingine, sembuse LISU??iwe imepotea au imeibiwa vyovyote vile.
 
Kuna watu walikuwa wanapinga ule mtindo watu kumlalamikia Magufuli kesi zao, walisema ni ushamba walipaswa kufuata taratibu kwa kupeleka malalamiko yao sehemu husika ila si ajabu hiki alichokifanya Lissu watakitetea.
Unalinganisha hao na Lissu? Lissu iliamuluwa auawe na rais wa nchi. Ni mtu gani wa chini atakubali kumsaidia?

Hujui kwamba Balozi Sokione alipoteza kazi kwa kwenda tu kumsalimia Lissu hospitalini?

Acheni roho mbaya
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani...
Ukitaka kuelewa fanya jaribio la kutoa ndizi mbivu kwa wale "nyani" wanaoranda mto ruaha kuanzia daraja mbili kuelekea Ruaha Mbuyuni.
 
Ninaouwezo na sema SUU hapo ulipo uangalie nitakachokufanya unaona tumo humu kwa bahati mbaya tu kwasbaabu tunaandika jumbe. Ila uache upuuzi wako nitakachkufnya usijekujakulia humu.
Ona hili nalo linamtishia nani sasa?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Mtu usalama wake ukiwa hatarini, nchi humps ulinzi. Samia alikataa kumpa ulinzi Lissu.

Samia ni business as usual kama Mwendazake tu...
Ulinzi siyo guarantee ya usalama wa mtu. Hata Rais Biden wa Marekani, pamoja na ulinzi wake wote ule, bado anaweza akauwawa au kuumizwa.
 
Kama mange kimambi tu, ku renew hati yake ya kusafiria walimkataliaa katakataa, kuwa wizara imezuiwa kufanya hivyo , hadi awamu ya sita tena kupitia kwa rais ndio akapewa nyingine, sembuse LISU??iwe imepotea au imeibiwa vyovyote vile.
Sasa kama passport ya Lissu imepotea mwezi uliopita, ambayo ni ndani ya miezi 10 ya Rais Samia, shida iko wapi? Samia naye kawaelekeza watu wa ubalozi wamfanyie figisu Lissu?
 
Unalinganisha hao na Lissu? Lissu iliamuluwa auawe na rais wa nchi. Ni mtu gani wa chini atakubali kumsaidia?

Hujui kwamba Balozi Sokione alipoteza kazi kwa kwenda tu kumsalimia Lissu hospitalini?

Acheni roho mbaya
Roho mbaya gani tena mkuu mbona unaongea vitu vingine kabisa hapa? Wengine huku mtaani wanaotaka kuuliwa kama Lissu watamuonea wapi huko Samia kama alivyomuona Lissu?

Mimi sina tatizo na wale waliyokuwa wanaemkumalamikia Magufuli na wala sina tatizo na alichofanya Lissu wote wanataka wapate haki zao pengine wameshindwa kupata huko sehemu husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…