Hongera kwa kufanya utafiti kwenye magereza yote nchi nzima, bora afugaye bata kuliko ajihusishaye na biashara haramu za bangi, meno ya tembo nk, sina hakika kama kuna sheria inawazuia askari kufuga mifugo katika maeneo yao ya makazi, lakini pia kuna watu wanatumia ofisi za umma kufanya biashara zao binafsi, unaweza kuusaidia umma wa watanzania kuwabaini hao kwa ujumla wao na kuwataja hapa badala ya kuhangaika na askari magereza wanaofuga kwalengo la kuzikimu familia zao kutokana na mishahara duni?
Si umesikia wabunge wanataka Tshs 420,000 kwa siku? Je yupi ni bora? Anaeiba kodi za watanzania kupitia mgongo wa katiba au askari magereza?
Kazi ni kwako.......