Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Natumaini watakuja wajuvi watakupa Msaada unaohitaji . kilichonishangaza ni kukimbia ufugaji wa kuku kwa sababu ya changamoto . je kwenye bata hutakimbia tena
 
Natumaini watakuja wajuvi watakupa Msaada unaohitaji . kilichonishangaza ni kukimbia ufugaji wa kuku kwa sababu ya changamoto . je kwenye bata hutakimbia tena
NImejaribu kidogo ndani ya mda mfupi sikuona changamoto yoyote, kwanza wakihatamia wanatotoa mayai karibia asilimia 90, kuhusu usafi wa banda ... wao mda wote wanahitaji kuwa kwenye sehemu yenye minyoo wanakula.... kuhusu magonja sijaona wakiugua .... kuhusu soko ndo sijajua likoje?
 
Komaa na unachokijua na ambacho una uzoefu nacho.Ufugaji wa bata nao utakutoa resi kama hutakuwa na ujasiri wa kupambana na changamoto.

Kumbuka hakuna biashara isiyo na changamoto !!
Ninachokijua ndo hicho kimenitoa berenge ..
 
mkuu fanya hvi ,nenda duka la binadamu omba vidonge vya antibiotics rangi mbili (pink and black) ,chukua maji kidogo kama 1/1 liter (nusu ya robo) koroga unga wa hivyo vidonge kwenye maji hayo masafi, chuku sirinji jaza yale maji, chukua kifaranga kimoja kinyweshe angala matone (5drops) .Zingatia haya hiyo 1/8ltr kwa vidonge 3 na kwa vifaranga 6-8. mm nilifiwa sana na vifaranga tena wengine wanakufa wakiwa na mwezi tayari. Hii dawa pia inatibu ndui niliitumia kutibu vifaranga vyangu vya bata mzinga. All the best. Vifaranga wapewe angalau siku ya 3 baada ya kuzaliwa, kama umechelewa wape hata sasa hivi.
 
Mkuuu pole na majukumu.MImi ni mfugaji wa bata ila nafuga bukini na perkin.Nikushauri hao bata wa kawaida hasa akiwa na watoto hakikisha wanakula chakula kidogo na kisiwe kingi sana wakila sana wanaweza wakafa kkwa ulafi then hakikisha unatenga maji yao vizuri na ubadilishe kila baada ya masaa sita au kila siku.tatu hakikisha banda ni safi ili kuzuia magonjwa.Bata hawahitaji joto la ziada boss maana hawa ni ndege maji
 
mkuu fuga bata bukini mkuu wanalipa sana mkuu
mimi nimewafuga for 11 years now bata mmoja analisha wenzake 20 kwa mwaka mzima
 
mkuu fuga bata bukini mkuu wanalipa sana mkuu
mimi nimewafuga for 11 years now bata mmoja analisha wenzake 20 kwa mwaka mzima
Safi sana! sokoni ana bei gani .. nawe uko wapi unipatie mbegu?
 
Km inawezekana naomba tutajie changamoto kubwa ulizokutana nazo utakua umetusaidia sisi wenye ndoto za kufuga baadae
 
Mimi bata wangu nawatibu kwa kuwaweka katika banda safi muda wote, chakula na maji safi.
 
Adui mkubwa wa vifaranga wa bata ni panya. Katika miezi miwili ya mwanzo jitahidi kuwaweka kwenye banda ambalo haliwezi kabisa kuingiza panya. Panya ana uwezo wa kuua vifaranga zaidi ya 10 kwa wakati mmoja akiwatoboa macho.
Ili kusaidia wakue haraka jaribu kuwapatia chakula cha kuku cha starter kwa hiyo miezi miwili ya mwanzo.
Pole kwa hasara iliyo kukumba.

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
 
Mjasiriamali huwa ni "risk taker" hivyo pambana tu na hivyo changamato za kuku. Kama una soko la uhakika nakuomba usiache kufuga kuku.
yote kwa yote shikamoo Tutor B
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…