Patandi maalum shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu wasiopatiwa lishe stahiki. Wanakula vyakula visivyoendana na afya zao serikali iimulike!!

Patandi maalum shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu wasiopatiwa lishe stahiki. Wanakula vyakula visivyoendana na afya zao serikali iimulike!!

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Shule hii ilijengwa ama ilianzishwa na rais john pombe magufuli ! Ni shule iliyobeba wanafunzi wenye ulemavu mchanganyiko ! Ukipata bahati ya kuitembelea unaweza kuangua kilio kulingana na Hali ya wanafunzi ilivyo ! Wako wasio sikia viziwi)wasioona vipofu) walemavu wa viungo wanaotembea kwa kutambaa na wanaotembea kwa machela maalum! Wapo wanaotoka udenda na wengine Wana ulemavu wa vichwa vikubwa ! Mchanganyiko huu unamaanisha wanahitaji lishe Bora kulingana na Hali zao ! Pia serikali imetenga bajeti kwa ajili ya shule kama hizi na hata wadau mbalimbali huwa wanaenda kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu pale ! Wanamichezo mashuhuri kutoka pande zote za ulimwengu wanaenda kutoa misaada patandi maalum! Jambo la kusikitisha na kuogofya ni aina ya chakula wanachopewa hao watoto unaweza kulia machozi ! Jicho langu limeshuhudia kwamba chakura kikuu ni makande yasiyoungwa chochote ! Chai isiyokuwa na sukari na mateso kadhaa wanayopatiwa wanafunzi hao ! Mkuu wa shule ya patandi maalum mwl janeth mollel jitahidi kusimamia lishe ya hao watoto ni mbaya mno na wengine sasa wanapata utapiamlo na kwashakoo! Plz isaidie jamii kwa kuwapa lishe Bora kama bajeti haitoshi itisha wadau tutachangia lakini chakura hicho sio rafiki kwa afya na aina ya ulemavu wa wanafunzi wako ,kama kuna ufisadi hapo unafanya laana itakuwa juu yako ! Afya za watoto hazipo sawa na nihatari sana
 
Back
Top Bottom