Pato la kila Mkoa: Dar es Salaam yazidi kuongoza ikifuatiwa na Mwanza, Njombe na Katavi zashika mkia

Pato la kila Mkoa: Dar es Salaam yazidi kuongoza ikifuatiwa na Mwanza, Njombe na Katavi zashika mkia

Miaka 15 badae hii nchi yote tutakua tumeizunguka wasukuma, ardhi ya nchi tutakua tumechukua yakutosha. Maamuzi makubwa ya nchi yatatokana na sisi tunamtaka nani. Blessed Lakezone
Mtakapo maliza kuizunguka nchi yote na kuchukua ardhi ya kutosha nchi mtaipa jina gani?
 
Ni kipi kinafanya Mbeya kuwa na pato kubwa kupita Arusha?
We jamaa bwana ,unasikitisha Sana ..Bustan ya Eden iko Mikoa ya Kusini ..Mbeya kiujumla inaongoza kwa uzalishaji wa nafaka mseto Tzn hii Sasa sijui unataka nini kingine.Niongeze volume?
 
Mwanza nyie mshindani wenu ni Mbeya ,hakuna kitu Mwanza City itashindana na Dom..

Dom size yake kwa sasa ni Dar tuu,huu ni ukweli mchungu

Mwanza nyie mshindani wenu ni Mbeya ,hakuna kitu Mwanza City itashindana na Dom..

Dom size yake kwa sasa ni Dar tuu,huu ni ukweli mchungu
Nikuambie tu ni hivi hayati magufuli alipoitanga Dadoma kuwa jiji watu wengi walipinga coz Dodoma ilikuwa haijakizi viwango vya kuwa jiji lakini Rais wetu mpendwa hayat magufuli alilazimisha sasa kuficha aibu ilibidi kuwalazimisha tamisemi kupika data za uongo ili kuwaaminisha watu kuwa Dodoma ilistahili kuwa jiji na pia limeweza kuyapiku majiji makubwa kama Mwanza, nakuambia nje ya Dar sehemu nyingine zina safari ya miaka 1000 kufika mahali Mwanza ilipo.
 
Subiri watoe orodha ya mikoa maskini kisha rudi tena hapa na hizo tambo!!! Hapa nazungumzia orodha inayoelezea hali ya umaskini kwa Watanzania na sio hizi data ambazo ni pesa za mabeberu!!!

Mkoa kama Kilimanjaro usiutarajie kutokea juu kabisa kwenye orodha ya mikoa yenye pato kubwa kwa sababu hakuna larger investments kama zilizo kwenye mikoa yenye madini!!

That applies to Arusha as well.

Lakini tukija kwenye orodha ya mikoa maskini kama nilivyotafsiri hapo juu, hapo lazima utazikuta Kilimanjaro na Arusha zikiwa angalau kwenye Top 5... WHY? Kwa sababu shughuli nyingi za mikoa hiyo, pesa zinaingia moja kwa moja kwenye mifuko ya watu na hivyo ku-define kiwango cha umaskini/utajiri!

Hapo juu naona kizaizai amehoji kutokuwapo kwa Iringa! Kama ilivyo kwa Arusha na Kilimanjaro, ndivyo ilivyo kwa Iringa! Kwenye orodha ya mikoa maskini kama nilivyo-define hapo juu, lazima Iringa itaonekana "tajiri" kwa sababu ni mkoa unaotegemea sana kilimo, na pesa yake inaenda moja kwa moja kwenye mifuko ya watu!!

But also don't forget... investments kubwa za Arusha ni pamoja na utalii ambao umeathirika sana!! Na pia Mererani haipo Arusha bali Manyara lakini pato la watu upitia Merelani huwa linaenda Arusha!

Kuweka kumbukumbu sawa, gesi ikishaanza kuchimbwa, halafu kampuni za uchimbaji gas zikajisajili Lindi kama ndio mkoa wao wa kikodi, basi msishangae kuanzia hapo orodha ikisema "Lindi inaongoza, na Dar es salaam ndo inafuata"!! Watu watapinga kwa sababu hawafahamu logic ya hizi takwimu!!
Sawa sawa
 
Ofisi ya taifa ya takwimu imetoa pato la kila mkoa nchini Tanzania, mkoa wa Dar es salaam wazidi kuongoza ukifuatiwa na Mwanza.

Mikoa ya Katavi na Njombe imeshika mkia kwa kua na pato dogo sana ukilinganisha na mikoa mingine.

Kwenye kumi bora kanda ya ziwa imeingiza mikoa 3, Mwanza, Shinyanga na Geita kwa jumla ya Trilioni 25 sawa na mkoa wa Dar es Salaam.

Kanda ya kaskazini, pato la mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ndio inafikia pato la mkoa wa Mwanza. Utajiri wa Arusha, Kilimanjaro na Tanga ni sawa na utajiri wa Mwanza na Shinyanga.

Kwa Takwimu za NBS, ukitoa Dar, kanda inayofuatia kwa utajiri ni anda ya ziwa, ikifuatiwa na Kaskazini huku Kusini kwa Lindi, Mtwara na jirani yao Pwani wakishika mkia.

Kanda ya nyanda za Juu kusini Mbeya inawabeba ila imezungukwa na mikoa choka mbaya kama Katavi na Njombe hivyo kuchangia kanda hiyo kuonekana ni choka mbaya mbavu za mbwa.

Watu wa Mara tukomae tuiondoe kilimanjaro ama Ruvuma hapo juu tuingie top 10.

Dodoma🦍🦍
 
We jamaa bwana ,unasikitisha Sana ..Bustan ya Eden iko Mikoa ya Kusini ..Mbeya kiujumla inaongoza kwa uzalishaji wa nafaka mseto Tzn hii Sasa sijui unataka nini kingine.Niongeze volume?
Kumbe mnategemea kilimo cha mpunga peke yake ndo mje mje mpambane na mikoa ya kanda ziwa yenye rasilimali lukuki, kama kilimo, ufugaji, uvuvi na madini pia viwanda😂😂😂
 
Kumbe mnategemea kilimo cha mpunga peke yake ndo mje mje mpambane na mikoa ya kanda ziwa yenye rasilimali lukuki, kama kilimo, ufugaji, uvuvi na madini pia viwanda😂😂😂
Una matatizo Sana ,unajua kusoma ? Au tatizo ni uelewa? Kama ni mpunga si Morogoro angekuwa juu ya Mbeya?
 
Nikuambie tu ni hivi hayati magufuli alipoitanga Dadoma kuwa jiji watu wengi walipinga coz Dodoma ilikuwa haijakizi viwango vya kuwa jiji lakini Rais wetu mpendwa hayat magufuli alilazimisha sasa kuficha aibu ilibidi kuwalazimisha tamisemi kupika data za uongo ili kuwaaminisha watu kuwa Dodoma ilistahili kuwa jiji na pia limeweza kuyapiku majiji makubwa kama Mwanza, nakuambia nje ya Dar sehemu nyingine zina safari ya miaka 1000 kufika mahali Mwanza ilipo.
Kwa hiyo kila mwaka wanapika? Mbona Mbeya imewapiku nazo zimepikwa? 😁😁🤭🤭

Hamna kitu huko watu wako hoi kwa umaskini.
 
Back
Top Bottom