Kwenye suala na maendeleo Mwanza inakimbia kwa kasi sana, nilikua na miezi kadhaa sijafika Mwanza leo nina wiki niko Mwanza kuna mabadiliko ya kimaendeleo makubwa sana yanayo onekana kwa macho si yakufikirika kuanzia barabara, hudumaza afya na makazi. Kati ya mikoa niliyowahi kufika Mwanza ndio mkoa wananchi wake wana makazi bora sana japo yapo maeneo yenye makazi duni kama Igogo na mabatini tena nahisi hizo tu ndio sehemu zenye makazi duni.
Kwenye afya kuna zaidi ya hospital 5 za kisasa ukianzia bugando ,sekou toure, kamanga hospt aghakan, Tanzanite hospt dispensary karibu kila mtaaa clinic za madactari bigwa zipo za kutosha.
Mwanza mjini watu wako busy na kazi wizi wa kishenzi shenzi wa kuchomoleana upo kwa kiasi kidogo sana, watu wako busy na maisha .
Anyway Mwanza imekua kiuchumi.