PreGE2025 Patrick Asenga afukuzwa kwenye kikao Segerea kwa kupinga ajenda ya 'No Reforms No Election'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliokaa tarehe 14 April Mwaka 2025 Jimbo la SEGEREA kwa pamoja wamemfukuza aliyekua Mwenyekiti wao wa Jimbo hilo Bw. Patrick Asenga kwenye kikao kwa kuwa ni sehemu ya watu wanaopinga ajenda ya CHADEMA inayoitwa NO REFORMS NO ELECTION.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Kata mbalimbali za Jimbo hilo hawakuwa tayari kuendelea na Kikao wanamtuhumu kuwa amekosa uadilifu na hekima za uongozi hastahili kuwa sehemu ya Wanachama wa jimbo hilo.

Segerea wamekuwa na msimamo mkali juu ya wajumbe wote wanaopinga ajenda ya NO REFORMS NO ELECTION bila kujali vyeo vyao ikumbukwe Patrick Asenga ni Mweka Hazina wa Kanda ya Pwani lakini hiyo nafasi haikumsaidia mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu baada ya kuondoka kikao kikaendelea kwa utulivu na Wanachama wakapitisha ajenda za kikao.

View attachment 3304476
Wajumbe wenyewe choka mbaya sura zinaonyesha wana dhiki
 
Ukiangalia mandhari ya kikao na watu wenyewe......huoni uhai kabisa!! Pathetic!!!
 
Demokrasia ndani ya Chadema iko wapi? Mnataka watu wa ndiyooo tu?
Haki ya Mungu naapa, ikitokea hiki Chama kimeshika madaraka; basi ni wiki mbili tu tutaomba poo. Hii mentality ya kwamba mtu akiwapinga viongozi wa juu kwenye jambo flani ni msaliti na mamluki ni ya kijinga na kipumbavu sana inayowaharibia. Ajabu wao wanapigania mambo hayohayo wanayoshindwa kuyatekeleza. Wafuasi wa lissu, wakati wa uchaguzi, walianza kumtupia maneno yule mgombea wa tatu (nimemsahau jina) kuwa ametumwa eti. Watu wa ajabu kabisa, Cha kushangaza ni kwamba muda wote wapo mtandaoni hapa wakimtaja Mungu.....UNAFIKI!!
 
..kwa hiyo unachosema ni " No Reforms Then Election "?
Unaniwekea maneno mdomoni. Mimi ningesema "Elections followed by Reforms " kwa sababu najua hamna namna Reforms za maana zitafanyika kabla ya Elections. Itakuwa kama walivyoongeza neno Huru kwenye jina la Tume ya Uchaguzi ili kuwapa Tume Huru ya Uchaguzi mliyokuwa mnadai. Muda huu ningetafuta wagombea wabishi kama yule dada wa Dodoma, yule dada wa Chato, Sigrada, yule mama Mwakipesile aliyelala nje ya ubalozi na wengine ili kukinukisha kuanzia hatua za kuchukua fomu, kurudisha fomu, kupiga kura na kuhesabu kura. Ningewapa support kubwa Bawacha, Bavicha na Bazecha na matawi yote ya vyuoni na mitaani.

Amandla...
 
..Election followed by Reforms.

..No Reforms Then Election.

..Ni vigumu sana kueleweka ukizingatia yaliyotokea 2019, 2020, na 2024.
 
Ni rahisi sana ukizingatia matokeo hayo. Ukizingatia chaguzi hizo utajua kabisa kutegemea reforms 2025 ni ndoto za mchana. Ukisema No Reforms unajifunga pingu mwenyewe. Serikali ita call your bluff na kukuangalia uki flounder. Ukifanya fujo kuzuia uchaguzi utakuwa umehalalisha hatua zozote itakazochukua kuzuia fujo. Naona wajanja wameanza kutafuta namna ya kuweza kujichomoa kwenye shimo walilojichimbia.

Aidha, msisahau kuwa mshindi akishatangazwa wa uchaguzi wa urais basically hamna recourse. Hakuna mamlaka itakayoweza kuubatilisha.

..Njia unayopendekeza ya " Reforms after Election " imeshajaribiwa na ndio imetufikisha hapa tulipo. Ndio njia iliyotumika 2019, 2020, na 2024.

..Ni afadhali tujitahidi katika " No Reforms No Election " kwa nguvu zetu zote tuone tutapata matokeo gani.

..Sasa hivi naona kama tunajikatisha tamaa wenyewe wakati ujumbe haujafika hata nusu ya nchi tayari mnasema serikali haita-respond.

..Tujitahidi ku-expose vurugu na unyama ambao wapinzani hutendewa wakati wa uchaguzi.

..Mambo mabaya sana yamekuwa yakitendeka lakini kwasababu hayajapigiwa kelele inavyostahili ndio maana kuna watu bado hawaoni ulazima wa hatua walizochukua Chadema.
 
Nyinyi ndio mmekata tamaa. No Reform No Election ni naive na itazimwa kirahisi tu. Inaonyesha kuwa mmepoteza moyo wa kupambania hicho mnachosema mnakitaka. Niambie ni presha ya aina gani CDM inaweza kuiwekea serikali mpaka inyanyue mikono. Mnadhani petition mtakazopeleka UN zitaifanya i apply presha kwa serikali. Au watu kama Robert Armstrong wataweka presha E.U. Mnasahau kuwa ajenda zinazosikilizwa ni Gaza, Ukraine na kidogo Sudan. Na zaidi yote nchi zote hizo zinajipanga namna ya kum survive Trump. Petition yenu itapokewa na ndio itakuwa mwisho wake. Kwa taarifa yako hayo unayotaka kuyapigilia kelele yanajulikana tayari na nchi za Magharibi. Unadhani balozi zao hazitoi taarifa? Ukweli ni kuwa Tanzania ni kidagaa katika the scheme of things.

Ninachoilaumu Chadema ni kuwa badala ya kuwa na strategy ya maana wanakazania kuchuma matunda yaliyo chini chini. Badala kufanya kazi ngumu na muhimu ya kukiunganisha chama chao wao ndio kwanza wanaendekeza mpasuko. CDM inaacha mbachao kwa msala upitao. Hizo rallissa tumeziona sana lakini at the end of the day hazitakuwa na effect yeyote. Kama ilivyokuwa kwa wakina Mrema, Mtikila n.k. Kinachonisikitisha ni kuwa huu mpango wenu utakaposhindwa hamtakubali responsibility ila mtajikita katika kutafuta wachawi na wasaliti.

..kunatakiwa pressure kabla ya uchaguzi, na baada ya uchaguzi.

..nikisoma maoni yako naona kama unaamini pressure kabla ya uchaguzi hazina maana, au hazitazaa matunda.

..G55 hawataki kushirikiana na chama kuweka pressure kabla ya uchaguzi, lakini wanataka chama kiwa-support katika kugombea.
 
Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliokaa tarehe 14 April Mwaka 2025 Jimbo la SEGEREA kwa pamoja wamemfukuza aliyekua Mwenyekiti wao wa Jimbo hilo Bw. Patrick Asenga kwenye kikao kwa kuwa ni sehemu ya watu wanaopinga ajenda ya CHADEMA inayoitwa NO REFORMS NO ELECTION.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Kata mbalimbali za Jimbo hilo hawakuwa tayari kuendelea na Kikao wanamtuhumu kuwa amekosa uadilifu na hekima za uongozi hastahili kuwa sehemu ya Wanachama wa jimbo hilo.

Segerea wamekuwa na msimamo mkali juu ya wajumbe wote wanaopinga ajenda ya NO REFORMS NO ELECTION bila kujali vyeo vyao ikumbukwe Patrick Asenga ni Mweka Hazina wa Kanda ya Pwani lakini hiyo nafasi haikumsaidia mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu baada ya kuondoka kikao kikaendelea kwa utulivu na Wanachama wakapitisha ajenda za kikao.

View attachment 3304476
Fukuza kabisa hiyo mbuzi jinga kabisa
 
..kunatakiwa pressure kabla ya uchaguzi, na baada ya uchaguzi.

..nikisoma maoni yako naona kama unaamini pressure kabla ya uchaguzi hazina maana, au hazitazaa matunda.

..G55 hawataki kushirikiana na chama kuweka pressure kabla ya uchaguzi, lakini wanataka chama kiwa-support katika kugombea.
Mimi naamini hazitazaa matunda mnayotegemea based on history.
G-55 hawakatai pressure ya no reforms, wanachokataa ni kuiunganisha no elections.
Mimi naamini wako tayari sana kushirikiana kuweka presha kuhusu reform maana ndicho wamekuwa wanakipigania siku zote. Chama chao kimekuwa heavy handed dhidi yao badala ya kuwapa heshima wanayo stahili. Ukisema kuwa utashiriki hakukuzuii hapo baadae kujitoa kwenye uchaguzi. Lakini ukisema haushiriki mapema ni vigumu kugombea kama hali itabadilika. Sasa hivi CCM wanaweza kupitisha sehemu kubwa ya reforms mnazodai kwa sababu CDM haimo kwenye picha. Na hamtaweza kusema kuwa mnataka kugombea kwa sababu reforms mlizotaka zimetekelezwa. Mtaambiwa tu mmechelewa. Na mkienda Mahakamani kesi itaamuliwa 2029. Hili Mbowe angelistukia mapema sana.

..Na kushiriki bila Reforms kutazaa matokeo mazuri? Mbona ushahidi wa yaliyotokea 2019, 2020, na 2024, hautoi picha nzuri?
 
Na usiposhiriki kwa sababu hamna reforms mtapata matokeo mazuri? Mwaka 2015, Jecha alifuta uchaguzi Zanzibar alipoona wapinzani wanaweza kushinda. CUF wakagomea uchaguzi wa marudiano, Shein akatangazwa mshindi na CCM ikaunda serikali. Hii ndio maana wazaliwa wa CUF, ACT-WAZALENDO hawataki kusikia neno kugomea uchaguzi. BTW, Marekani na EU walionyesha wazi kusikitishwa kwao kwa kitendo cha Jecha lakini walishirikiana na serikali ya Shein.

Funzo hapa ni kuendelea kupigana mkiwa ndani ya system. Mkiwaachia CCM itakula kwenu. Ndicho wanachosema wakina Mrema. Wasikililizeni badala ya kuwatukana.

Amandla...
 
Chama cha PRI kilitawala Mexico kwa miaka 71 mfululizo ndio kikashindwa uchaguzi. Wapinzani wake hawakukata tamaa. Nyinyi mnataka kususa baada ya kushindwa miaka mitano tuu. Rais wa sasa wa Zambia amefungwa, amedhulumiwa uchaguzi lakini aliendelea kupambanu. Leo ndie Rais wa Zanzibar. Kulikuwa na UNIP, KANU lakini leo ziko wapi. India Congress Party kiko wapi? Chama cha Banda kiko wapi?

Amandla...
 
Funzo hapa ni kuendelea kupigana mkiwa ndani ya system.
Kwa nini waendelee "kupigana ndani ya system'; kwani hapawezi kuwepo mapigano nje ya hiyo system?
Kwanza hiyo unayo iita system maana yake ni nini? Kuna system zaidi ya wananchi wanao elewa haki zao?

System ni wananchi wenye uelewa, ndio watakao amua hatma ya nchi hii.
Unapojivisha joho la kupinga bila hata ya kufikiri maana ya kupinga kunakuondolea hali ya kuwa na mawazo yenye mizani ya fikra.
 
Back
Top Bottom