Mwili wa aliyekuwa mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), mhandisi Patrick Mfugale umewasili katika viwanja vya hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuagwa.
Viongozi mbalimbali wamewasili katikahospitali hiyo akiwemo naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya, katibu mkuu wa Wizara hiyo, Joseph Malongo, mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri na wabunge mbalimbali.
Pia wapo viongozi mbalimbali wa Tanroads, wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini pamoja ndugu, jamaa na marafiki.
Kwa mujibu wa ratiba mwili wa Mfugale utapelekwa Uwanja wa ndege wa Dodoma saa 10:00 jioni kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam ambapo utaagwa tena katika ukumbi wa Karimjee kesho.
Mfugale alifariki dunia Jumanne Juni 29, 2021 saa 5 asubuhi katika hospitali ya Benjamin Mkapa.
PIA SOMA:
-
TANZIA - Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma
Source: Mwananchi