TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Sahihisha kichwa cha habari...mi nilidhani ni yeye kumbe mwili.
 
Alikuwa anapenda kuongea na vijana wengi na baadhi walikuwa wanamuuliza hili.....na alikuwa anawajibu bila kusita kwamba ataachaje kufanya majukumu ya kitaifa na wakati vijana hamjitambui? Kwa kiasi usemi wake una mantiki vijana wengi ni pumba + mashudu....angalia tu hata comments nyingi hapa jukwaani. Jokes all the time like small girls!!
 
Unatakiwa muda mwingine ufurahie maisha ili uweze kuishi miaka mingi, angalia kama Jakaya yuko na afya njema.
 
Huyu Mzee tumpe heshima yake anayostahili, ni rahisi kwa vijana ku joke na kutukana ila mchango wa Mhandisi Mfugale hapa Tanzania ni mkubwa sana kuliko hawa wanaombeza na ambao nina hakika wengi hawaufahamu mchango wake. Sasa tunataka tumsifu mzungu aliyetutawala au tumsifu huyu Mtanzania mwenzetu aliyefanya kazi inayoonekana tena kwa uadilifu na kwa jitihada kubwa??
 
Mwili wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale utaagwa leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo mwili utapelekwa nyumbani kwa mwendazake, Kimara Temboni, kisha Julai 3 utapelekwa Ifunda, Iringa, na kuzikwa huko Julai 5, 2021.
 
Jana nilikuwepo pale Benjamini Mkapa pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali, na waombolezaji wengine, kutoa heshima zetu za mwisho.
 
Aliyetoa hotuba kwa upande wa watoto nimeshindwa kuendelea kuisikiliza. Looh " Huyu mzee.... lah. Watoto tunao.
.
 
Huyu alipandishwa sana chat na JK. Alipokuwa kwa JPM akazidi kumpandisha chati na inasemekana akamgeuka hata JK. Sasa undani wa kifo chake ukoje? Mbona ilikuwa ghafla vile! Ni corona kweli ile?
 
Huyu alipandishwa sana chat na JK. Alipokuwa kwa JPM akazidi kumpandisha chati na inasemekana akamgeuka hata JK. Sasa undani wa kifo chake ukoje? Mbona ilikuwa ghafla vile! Ni corona kweli ile?
Unapo sema akamgeuka hata jk unamaanisha nini alimgeuka ktk mambo gani?
 
Jamani Mzee wa Msoga ni mstaafu sasa. Ameachana siku nyingi na siasa za moja kwa moja za kujibishana kisiasa majukwaani, tumuache ale pensheni yake na apumzike na wajukuu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…